Majina ya waliopewa siku 90 na CCM kujiuzulu ni hawa hapa

kwa hiyo hata Benjamini mkapa mnatarajia ataondoka kamati kuu?????????
ccm wanatuzuga hawana lolote
 
Hebu mnisadie Gray Mgonja kwa nini yumo humo na inakuwaje Zakhia Hamdani Meghji ambaye alidai Balali alimdanganya juu ya EPA hayumo? Meghji kipenzi cha JK ndiye aliyejifunga kibwebwe na kujitosa Bungeni kutetea majengo pacha ya BOT huku akijua ni ufisadi ambao CCM ilinufaika katika chaguzi za 2005?

If Balali (deceased) na Mgonja wamo basi Meghji ni lazima awe kinara wao........................................otherwise that is not accountability but witch-hunt...................
 
Hebu mnisadie Gray Mgonja kwa nini yumo humo na inakuwaje Zakhia Hamdani Meghji ambaye alidai Balali alimdanganya juu ya EPA hayumo? Meghji kipenzi cha JK ndiye aliyejifunga kibwebwe na kujitosa Bungeni kutetea majengo pacha ya BOT huku akijua ni ufisadi ambao CCM ilinufaika katika chaguzi za 2005?

If Balali (deceased) na Mgonja wamo basi Meghji ni lazima awe kinara wao........................................otherwise that is not accountability but witch-hunt...................
time will tell lazima Meghi na Mkapa tuwape mabango yao au tuichafue CC nzima ya ccm ili waache kuwadanganya watu.The two are too corrupt.
 
Orodha ya Mafisadi (List of Shame)​
B. USHIRIKI KATIKA KUTOA MAAMUZI YA KIFISADI

11. RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE


Kwa mfano, mnamo tarehe 10 Aprili 1990, Major Jakaya Mrisho Kikwete aliingia mkataba wa madini ya kampuni ya SAMAX Limited ambapo kampuni hiyo ilipewa leseni ya kuchimba dhahabu katika eneo la Lusu, Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora. Matokeo ya mkataba huo, maelfu wa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu waliokuwa eneo hilo waliondolewa kwa nguvu na vikosi vya FFU na bila ya kulipwa fidia yoyote. Hadi leo wananchi hao hawajalipwa fidia yoyote licha ya miaka zaidi ya kumi ya kufuatilia haki zao. Baada ya kutwaa utajiri wa dhahabu wa eneo hilo, SAMAX Limited iliuza eneo hilo kwa kampuni ya Ashanti Goldfields ya Ghana kwa dola za Marekani milioni 253. Ashanti Goldfields nao wakauza eneo kwa kampuni ya Resolute Limited ya Australia kwa kiasi kisichojulikana cha fedha za kigeni. Resolute Limited ndio waliojenga na wanamiliki Mgodi wa Dhahabu wa Golden Pride ulioko eneo la Lusu, Nzega hadi sasa na ambao ulifunguliwa mwezi Novemba 1998. Mnamo tarehe 5 Agosti 1994 Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete aliingia tena mkataba na kampuni ya madini Kahama Mining Corporation Ltd., kampuni tanzu ya kampuni ya Sutton Resources ya Canada. Ijapokuwa mkataba huu unaonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, mwezi Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation wakisaidiwa na vikosi vya FFU walivamia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na kuwaondosha kwa nguvu watu takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo. Baada ya kutwaa eneo hilo kwa nguvu za kijeshi, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni 280. Leo hii Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika.


Hivi huu MGODI sindio KIGWANGALA alikuwa anatikisa KIBERITI?
KAISHIA WAPI?
 
Safari moja uanzisha nyingine...kuanza kuenguana kamati kuu na halmashauri kuu ndo hatua ya kwanza kuelekea kuvuliwa uanachama, na hiyo ndo safari ya kifo cha CCM. Mungu ailaze mahali pema peponi...!! Amen.
 
Haya ndiyo madhara ya kukopi na kupasti,mtu aliyekufa anawezaje kupewa siku 90!au mnataka afufuke!mtoa mada hujafanikiwa kufikisha ujumbe wako!pole sana mkuu!!

kwa ccm yawezekana,mbona marehemu ametunukiwa shahada pale UDOM??Na sheria inasema mtunukiwa aliyehai ndo anastahili,serikali ya ccm imekubali marehemu kupata shahada!!
 
Mchezo mchezo mchezo siku tisini mchezo kimewashinda nini kuwafukuza sasa? Hivi gamba la nyoka linachukua siku ngapi kuvuka? Hicho ni kiini macho cha CCM hao ndo roho ya CCM wakiondoka hakuna chama. Tatizo lao waliweka pesa mbele badala ya mapenzi ya dhati kwa chama. POLENI WANA CCM> Kazi kwenu.:A S-key:
 
Hii habari inashangaza nani kawapa huo muongozo wa kujiuzulu na ni kwa sababu gani na kwanini ni legelege wengine wameshaaga dunia???

Hizi habari ni za kweli? Au ndio Uandishi Dondoso wa Sekta ya Habari nchini kwetu?
 
ongeza
sumaye
magufuri
meghji
mwandosya
mkapa
gachuma

usimsahau Ridhiwani......................hivi chadema yangia lini ikawa msemaji wa ccm....................au ******* yameenea hadi huko chadema???????????
 
Orodha ya Mafisadi (List of Shame)​
A. USHIRIKI WA MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI
[h=2]10. BENJAMIN WILLIAM MKAPA[/h]
mkapa.gif


Benjamin William Mkapa alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 hadi 2005 alipomaliza kipindi chake cha pili. Ufisadi wote ulioelezewa katika waraka huu ulitokea wakati wa utawala wa Rais Mkapa na anawajibika nao moja kwa moja ama kwa kuubariki au kwa kuunyamazia. Zaidi ya hayo, kuna ushahidi unaoonyesha kwamba wakati akiwa madarakani Rais Mkapa alishiriki moja kwa moja au kwa kutumia ndugu na/au washirika wa karibu wa familia yake katika ufisadi mkubwa na uliolipotezea taifa fedha nyingi. Kwa mfano, wakati akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mkapa alitumia wadhifa huo kuhakikisha kwamba kampuni iitwayo Tanpower Resources Limited inamilikishwa asilimia 85 ya hisa za kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd. inayochimba mkaa wa mawe huko Kiwira Mkoani Mbeya. Hisa zilizobaki asilimia 15 zinamilikiwa na Serikali. Tanpower Resources Ltd. ni kampuni iliyoanzishwa kwa ajili ya kuinuifaisha familia ya Rais Mkapa na washirika wake wa karibu. Taarifa za BRELA zinazonyesha kwamba wakurugenzi wa Tanpower Resources Ltd. ni Anna Mkapa, mkewe Rais Mkapa, Nicholas Mkapa, mtoto wa Rais, Bwana Joseph Mbuna, wakili wa kujitegemea na baba mkwe wa Nicholas Mkapa, Daniel Yona, Waziri wa Nishati na Madini wakati wa utawala wa Rais na bwana Joesph Mapundi. Baada ya Tanpower Resources Ltd. kutwaa umiliki wa Kiwira Coal Mines Ltd. kwa nguvu za Ikulu ya Rais Mkapa, iliingia mkataba na Shirika la Ugavi wa Umeme nchini TANESCO wa kujenga mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mkaa wa mawe na kuiuzia umeme TANESCO. Mkataba huo utainufaisha kampuni ya Kiwira Coal Mines Ltd., na kwa hiyo Rais Mkapa, familia na washirika wake wa karibu kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 271 kwa wakati wote wa mkataba.
 
mbona ufisadi wa lowassa, karamagi na rostam haukuwekwa hadharani kwenye wasifu wao?

mfano ni huu hapa...................
Orodha ya Mafisadi (List of Shame)
A. WALIOSHIRIKI MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI
[h=2]9. EDWARD LOWASSA[/h]
lowassa.gif
 
kuweka picha ya mtu na kudai ni fisadi bila kumworodheshea tuhuma zake ni kutomtendea ubinadamu.......
Orodha ya Mafisadi (List of Shame)
A. WALIOSHIRIKI MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI
[h=2]7. NAZIR KARAMAGI[/h]
karamagi.gif
9






Orodha ya Mafisadi (List of Shame)​
A. WALIOSHIRIKI MOJA KWA MOJA KATIKA VITENDO VYA UFISADI
[h=2]8. ROSTAM AZZIZ[/h]
rostam.gif
 
Back
Top Bottom