Majina ya waliopewa siku 90 na CCM kujiuzulu ni hawa hapa

Get lost. This is the blood and soul of CCM.
remove them and you are sure the life of CCM is over!!!
CCM's HEART BEAT is Rostam Aziz
CCM breath through Edward Lowasa
All the others are just the systems of life in CCM.

kwanza atakaye press hawa waondoke ameshajitakia death sentence
 
Pia alisema wamekubaliana kuzunguka kueleza ukweli wa Muswada wa Mabadiliko ya Katiba, ili kuondoa upotoshaji unaofanywa na wapinzani. source- Mwananchi la leo
Yaani JK bado anaamini kuwa muswada ni mzuri ila unapotoshwa?
Kama CCM wanazunguka nchi nzima kwa suala hilo kwanini kamati ya bunge ya sheria na katiba nayo isizunguke Tanzania nzima ikikusanya maoni? Kwa nini inaishia dodoma DSM na Zanzibar tu?
 
Haya ndiyo madhara ya kukopi na kupasti,mtu aliyekufa anawezaje kupewa siku 90!au mnataka afufuke!mtoa mada hujafanikiwa kufikisha ujumbe wako!pole sana mkuu!!
 
Orodha ya Mafisadi (List of Shame)​
B. USHIRIKI KATIKA KUTOA MAAMUZI YA KIFISADI

11. RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE


Rais Jakaya Kikwete amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Desemba 2005. Kabla ya kuwa Rais, Mheshimiwa Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo Nje na Uhusiano wa Kimataifa kuanzia 1995 hadi 2005, Waziri wa Fedha 1994 hadi 1995 na Waziri wa Maji, Nishati na Madini kuanzia mwaka 1990 hadi 1994. Kama Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mheshimiwa Kikwete alishiriki moja kwa moja katika kusaini mikataba mibovu ya madini na makampuni ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limeendelea kupoteza utajiri mkubwa na kuinyima Serikali uwezo wa kifedha wa kuhudumia wananchi. Kwa mfano, mnamo tarehe 10 Aprili 1990, Major Jakaya Mrisho Kikwete aliingia mkataba wa madini ya kampuni ya SAMAX Limited ambapo kampuni hiyo ilipewa leseni ya kuchimba dhahabu katika eneo la Lusu, Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora. Matokeo ya mkataba huo, maelfu wa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu waliokuwa eneo hilo waliondolewa kwa nguvu na vikosi vya FFU na bila ya kulipwa fidia yoyote. Hadi leo wananchi hao hawajalipwa fidia yoyote licha ya miaka zaidi ya kumi ya kufuatilia haki zao. Baada ya kutwaa utajiri wa dhahabu wa eneo hilo, SAMAX Limited iliuza eneo hilo kwa kampuni ya Ashanti Goldfields ya Ghana kwa dola za Marekani milioni 253. Ashanti Goldfields nao wakauza eneo kwa kampuni ya Resolute Limited ya Australia kwa kiasi kisichojulikana cha fedha za kigeni. Resolute Limited ndio waliojenga na wanamiliki Mgodi wa Dhahabu wa Golden Pride ulioko eneo la Lusu, Nzega hadi sasa na ambao ulifunguliwa mwezi Novemba 1998. Mnamo tarehe 5 Agosti 1994 Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete aliingia tena mkataba na kampuni ya madini Kahama Mining Corporation Ltd., kampuni tanzu ya kampuni ya Sutton Resources ya Canada. Ijapokuwa mkataba huu unaonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, mwezi Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation wakisaidiwa na vikosi vya FFU walivamia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na kuwaondosha kwa nguvu watu takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo. Baada ya kutwaa eneo hilo kwa nguvu za kijeshi, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni 280. Leo hii Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika.
 
Haya ndiyo madhara ya kukopi na kupasti,mtu aliyekufa anawezaje kupewa siku 90!au mnataka afufuke!mtoa mada hujafanikiwa kufikisha ujumbe wako!pole sana mkuu!!

Umeona hayo mabano na alama ya kuuliza? Kulikuwa na tetesi kuwa henda Balali hajafa. Temea mate kaka kama inauma.
 
HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM), imetangaza safu mpya ya uongozi wa juu wa chama hicho watakaoongoza Sekretarieti yake na Kamati Kuu (CC) huku vigogo wengi wakianguka na kisha kutoa siku 90 kwa watuhumiwa wa ufisadi kujiondoa wenyewe NEC ya chama hicho vinginevyo watawajibishwa.

Katika uteuzi huo, Wilson Mkama amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Yusuf Makamba. Mkama atasaidiwa na Naibu Makatibu Wakuu (Bara na Visiwani), John Chiligati na Vuai Ali Vuai. Katibu mpya wa Itikadi na Uenezi ni Nape Nnauye, huku, Mwigulu Mchemba akichaguliwa kuongoza Idara ya Fedha na Uchumi. Mkuu wa Oganaizesheni ni Asha Abdallah Juma na Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Januari Makamba.

Waliochaguliwa kuunda Kamati Kuu ni Abdulrahman Kinana, Zakia Meghji, Dk Abdallah Kigoda, Pindi Chana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera, Constancia Buhiye, William Lukuvi na Steven Wassira.

Kwa upande wa Zanzibar, waliochaguliwa ni Dk Hussein Mwinyi, Dk Maua Daftari, Samia Suluhu Hassan, Shamsi Vuai Nahodha, Omar Yusuf Mzee, Profesa Mbarawa Mnyaa na Muhammed Seif Khatib..........................................

Source: Mwananchi ya leo
Swali la kujiuliza ni je,hii ni ngozi mpya au ni re-cycling? Unachukua material za vitu vya zamani unatengeneza bidhaa mpya. Zinang'ara ndiyo, lakini uimara wake ni wa wasi wasi.
 

lowassa.gif
mkapa.gif
rostam.gif
karamagi.gif
mkono.gif
ruta.gif
mgonja.gif
mramba.gif
chenge.gif
balali.gif
 
duh, kama itakua hivyo basi CCM itakufa. ikumbukwe hiyo ndio roho ya CCM. ikumbukwe kua hao ndo mihimili ya chama kiuchumi na kisiasa.so CCM kwaheriiiiiiiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom