Majina ya simu za Kichina

Halafu wachina wanatengeneza bidhaa kulingana na uwezo wa mteja. Ndio maana wanafanya biashara dunia nzima. Pengine waTz wengi hawana uwezo wa kununua simu na bidhaa nyingine za mswiss, mjerumani, mwingereza, n.k, ila za mchina special kwa nchi fukara km tz.
Kigezo kikubwa ni uwezo wa mteja mkuu.

Manake naona watu wanafanya kama kila kitu cha mchina ni feki kitu ambacho sio kweli.

Hizo feki wanauziwa watu ambao hawana uwezo wakununua originalna zipo nyingi kwa vile wateja wa haina hio wapo wengi pia.
 
Hapana Mkuu! Samsung na LG wametoa simu zenye line mbili original. Ila Nokia na kampuni zingine sina hakika.
Hizo Samsung za laini mbili zenyewe zinauzwa zinauzwa Afrika na India pekee ulaya na amerika wala hamna kitu kama hicho.
 
Alafu watengenezaji sijui wote walikuwa madj maana ringtones ni full kelele
 
kwa Nokia *#0000# inakupa ni aina gani ya Nokia, Kama ni Feki aileti kitu
 
kwa Nokia *#0000# inakupa ni aina gani ya Nokia, Kama ni Feki aileti kitu
Sasa hivi wajomba wanaweka kitu kama hicho so usije ukajidanganya nimeshuhudia kwa macho yangu n97 ikisoma hizo namba nikajagundua kwenye player hawana real player wao wana player yao ya kawaida tu ila wangeweka real player ningeingizwa mjini jamaa alikuwa anataka laki nne ya fasta wakati simu original inauzwa laki 9 hadi m1
 
Wametoa pia jamii ya iphone inafanana kila kitu ila tofauti ni jina imeandikwa PHONE badala ya iPHONE. wezisana hawa sijui kwanini makampuni hayawashitaki hawa au sheria za hati miliki za majina na makampuni zokoje

Wanayo nyingine inaitwa iPhcne. Wameiandika kwa kutumia fonts fulani, ukiangalia haraka haraka unaona kama iPhone. Pia niliona Phillps ambayo unaweza ukafikiri ni Phillips. Lakini ukienda kule kwao, hizo simu fake zina maeneo maalum ya kuuzwa. Huwezi ukaingia kwenye maduka ya serikali na makampuni makubwa uzikute hizo. Hizo zinauzwa sehemu maalum ambazo wachuuzi kutoka third world ndio wanaenda kuchukua vitu vya bei rahisi.
 
Wanayo nyingine inaitwa iPhcne. Wameiandika kwa kutumia fonts fulani, ukiangalia haraka haraka unaona kama iPhone. Pia niliona Phillps ambayo unaweza ukafikiri ni Phillips. Lakini ukienda kule kwao, hizo simu fake zina maeneo maalum ya kuuzwa. Huwezi ukaingia kwenye maduka ya serikali na makampuni makubwa uzikute hizo. Hizo zinauzwa sehemu maalum ambazo wachuuzi kutoka third world ndio wanaenda kuchukua vitu vya bei rahisi.

mwezi uliopita nilinunua simu za wachina 2 moja inaitwa Yutong na nyingine Nokio.
uncle wangu ana brand za electronic appliances kama PANASOANIC, SONV, SANSUNG, WIZIO, YAHAMA, TECHMICS...mchina kaazi kweli kweli
 
Wametoa kitu nokia N8 kama wewe sio mjanja hauwezi kugundua kuwa ni ya mjomba mchina angalia juu kuna sehemu ya kuingizia pini ya mini hdmi ukiona wamebandika kilebo tu ujue hiyo sio yenyewe maana hawa jama wamejaribu kuigeza os ya n8 kabisa ukiingia kichwa kichwa umepigwa na bei zake ni laki na nusu na laki mbili wakati original inaanzia laki sita hadi 1milion
Kuna jamaa anatembeza mitaani anauza eti laki moja unusu ,ilibidi nishangae sana haiwezekani simu inayouzwa zaidi ya laki saba iuzwe chee namna hiyo,jamaa muuzaji akawa anadanganya eti kapata msiba na mtu kimfaache chake so ameona apate hasara sababu ya shida,nikajua huo ni uongo nilipojaribu kugusa screen haisogei kama simu orijino ni kama Iphone screen huwa haisogei(slide),tulimpombana kuwa huyo ni mchina akakiri kuwa ni kweli tumpe elfu hamsini,akaambulia makofi kwa kutaka kutapeli watu,bure aghali jamani tuwe makini na mbuzi wa kwenye gunia(vitu vya mkononi)
 
za kichina zipo poa sana.mimi mwenyewe natumia simu ya kichina inaitwa G-TIDE.Naipenda sana hasa mida ya asubuhi ikipiga alarm ya kukuamsha lazima uamke maanake mlio upo poa sana.
 
Simu za ki-cheinizi zipo poa kwani manjonjo yake mengi ya ukweli. Ni simu unazoweza kuibia musiki katika simu ya mwingine kama kaacha bluetooth on.yapo hayo ma blacklist,whitelist,voice effect sema tu kila kitu kinaubaya wake na uzuri wake.mfano ugumu wa kuifanyia internet setting na mengineyo loh! Unaweza kulia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom