Majina ya rangi uzijuazo kwa Kiswahili

Rangi ya ugoro,jani la mgomba,rangi ya fedha,kijani,kijani kibichi,samawati,zambarau,yapo mengi tu kiongozi.
 
Kiswahili ni lugha ya Kibantu, na lugha (nyingi) za Kibantu, kwa asili, zinaelekea kuwa na maneno matatu tu yanayoeleza dhana ya rangi:
1. Rangi nyeupe,
2. Rangi nyeusi, na
3. Rangi nyekundu.

Kama unazungumza lugha mojawapo ya Kibantu, jaribu kutafuta majina ya rangi, na utakutana na maneno ya rangi hizi tatu tu.

Katika Kiswahili, maneno mengine yanayotaja rangi tumekuwa tukiyapata kwa: (i) kutohoa kutoka lugha nyingine, kama vile Kiarabu na Kiingereza, na (ii) kwa kutumia analojia, yaani, kufananisha rangi husika na ile ya kitu fulani (kama vile chungwa, kahawa, zambarau, majani, udongo, ugoro, damu ya mzee, n.k.).

Kwa maneno yenye asili ya Kibantu, utaona kuwa maneno hayo yanaoana vizuri na sarufi ya lugha ya Kiswahili kwani yanatokea kama vivumishi vya kawaida tu vya neno 'rangi' (tazama <rangi nyeupe>, <rangi nyeusi>, <rangi nyekundu>; linganisha na <rangi nzuri>, <rangi mbaya>, <rangi nyingi>).

Lakini kwa maneno yanayoeleza rangi ambayo yametoholewa au yanatumia utaratibu wa analojia, utaona kuwa tunahitaji kutumia kihusishi <ya> ili kuhusisha 'rangi fulani' na 'kitu fulani', kama vile:
4. Rangi ya bluu (na sio rangi bluu),
5. Rangi ya kijani (na sio rangi kijani),
6. Rangi ya zambarau (na sio rangi zambarau),
7. Rangi ya samawati (na sio rangi samawati) n.k.

Kwa wazungumzaji tulio wengi, kanuni hizi (za kutumia au kutotumia <ya>) tunazijua lakini hatujui kwamba tunazijua! Kwa wanaojifunza Kiswahili ukubwani, inawabidi wajifunze kanuni zote hizi. Utawasikia wengine wakisema <Hii nguo ina rangi ya nyekundu.>.

kula LIKE mkuu!! nimependa ulivyoielewa kozi ya falsafa ya mwafrika!!
 
Green - kijani
orange - hudhurungi (siyo grey)
grey - kijivu
yellow - manjano
white - nyeupe
gold - dhahabu
red - nyekundu

kuna rangi inaitwa "chanikiwiti" sikumbuki ni rangi gani kwa kizungu
Hudhurungi ni Orange au rangi ya gold
 
Purple = Zambarau (matunda ya mizambarau au mawengewenge)
sky blue = samawati/ blue bahari
brown = Hudhurungi/damu ya mzee/udongo
dark green - kijani kibichi
grey - kijivu
khaki = majani makavu
red rose = Waridi jekundu
yellow = njano
silver = fedha
black =nyeusi


White je?
 
Vipi hizi?

Nyeusi
Kijivujivu
Majivu
Fedha
Udongo
Kahawia
Chokoleti
Kutu
Shaba
Hudhurungi
Ukaria
Marungi
Zambarau
Urujuani
Nili
Buluu
Samawati
Feruzi
Kijani
Zaituni
Zumaridi
Chanikiwiti
Ndimu
Manjano
Mahindi
Dhahabu
Kaharabu
Machungwa
Nyekundu
Waridi
Pinki
Lulu
Mtindi
Nyeupe

https://sw.wikipedia.org/wiki/Rangi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom