Majina ya katikati ya kizungu ya Wachagga!

Godliving, straton, livingstone, wolfgang, wellington, elton, witness, goodluck, godbless, ruth, temperature, lovenesss



..................Dad:D

Hata temperature?? cjawahi ckia ... Hapa umeongeza chumvi
 
wachaga watu wa shule na dini ndugu yangu hatuwezi kushindana nao maana hata sekta ya biashara wamekamata wenyewe
 
Jamani nimesikia televisheni ya Ikulu tena ya bwana mkubwa huko Ikulu dodoma imepitiwa na vibaka vipi ndugu zangu kuna ukweli wa hilo
 
Godson,Godfrey, Hope, Sweet, Malaika......
Bila kusahau majina ya kilatini na/au ya watakatifu mfano Cordulla,Epifany,Theresia,Hortensia, Veronica, Maria,Anna, Marigareta, Hyasinta, Prosper, Gudila Elizabeth, Thecla, Celementine,Joseph, Valentine, Athanasi, Maximilian, Faith......., na yale ya kilugha Kindokyakosembe, Meku, Kindondeichi, Ukiwawoko, Mafurunja, Aikaruwa......n.k.
 
Pia kuna jina la kichaga Hamashold! Hutaamini ..ni yuke KM wa Un wakati ule!! tena hili ni jina la ukoo!

Sijui kwa nini Wachaga wanamind sana majina ya Kizungu!

Kwani hakuna majina mazuri ya Kiafrika yanayomtukuza Mungu?
 
Yakiwa ya kizungu, si ya wachagga.
Yakiwa ya wachagga, si ya kizungu.
 
Duu! Haya.
Hawa wanatumia haya ya maneno ya kizungu lakini ujumbe wao ni uleule sawa na warundi na Wanyarwanda hapo jirani, Tusengimana, Tugilimana, Ayumva, Bigilimana, Asanteyezu, Tushimimana, Ishimweimana.
Poowa tu!
 
Suala siyo majina ya kizungu dada, yaangalie yalivyo na yalivyolenga, John siyo sawa na Godlove, Celine siyo sawa na Happiness, Esther na Hopeful si sawa!!! Upo??
 
Suala siyo majina ya kizungu dada, yaangalie yalivyo na yalivyolenga, John siyo sawa na Godlove, Celine siyo sawa na Happiness, Esther na Hopeful si sawa!!! Upo??

Hicho haswa ndicho kilicholengwa,Lakini baadae kuna walioanza kuingiza majina kama Stanford, na mengine ya kikristo,. na wengine kuwabeza wachagga kuwa wanapenda majina ya kizungu.
 
Nilikuwa napitia hii mada nikagundua nick names zipi ni za watu wa eneo gani/kabila gani. Majina mengine ya kilugha..., we acha tu! Heri ya hayo ya kizungu.
 
Back
Top Bottom