Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,305
- 12,968
Vifo hivi viwakumbushe wanajeshi wetu kwamba watanzania wote ni ndugu na kwamba sote ni mavumbi na mavumbini ni lazima tutarudi. Mateso wanayoyafanya wanajeshi kwa raia wa Mtwara ni ya kinyama!!! Si ya kiutu hata kidogo!!! Ni bahati mbaya kwamba jeshi letu linatumiwa vibaya na wanasiasa!!! Mungu aturehemu sote na roho za wanajeshi hawa zipumzike kwa amani!!
Kweli kabisa ndugu yangu. Askari wetu wamezoea kuwageuza wananchi ngoma kwa kuwapiga na kuwaua bila sababu. Pamoja na ruhusa waliyopewa na waziri mkuu wakumbuke kuwa nao ni binadamu, wananchi wanapoumia na kusoneneka kutokana na mateso wanayoyapata kutoka kwa askari na wao kama binadamu yanapowafika hayo machungu ni yale yale. Hata waziri mkuu naye pamoja na amri zake akumbuke kuwa na yeye ni binadamu na ana ndugu ambao asingependa wapigwe au wauawe bila hatia kama inavyotokea Mtwara na kama ilivyotokea Arusha, Iringa, Morogoro na Ruvuma. Waziri mkuu angekuwa hata na chembe ndogo ya aibu angeomba radhi kwa kutoa kauli ile yenye ukakasi. R.I.P wanajeshi wetu mliouawa bila hatia.