Majina saba ya askari walio uwawa Sudan

Duh polisi tena? Ni polisi hawa wa IGP Mwema ama ni Military Police (MP) wa Gen. Mwamunyange?

Katika operation kama hizo polisi na mageleza wachache wanakuwepo. Huyo ni polisi wa Afande Mwema...
 
Majina ya askari saba wa Tanzania waliokufa kwenye shambulio la ghafla mjini Darfur yamepatikana.

2.png

Askari hao waliokufa ambao walikuwa kwenye vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa huko nchini Sudan ni :-
1. Sajenti Shaibu Othuman,
2. Koplo Oswald Chaula,
3. Koplo Mohamed Juma,
4. Koplo Mohamed Chikilizo,
5.
Pte. Rodney Ndunguru,
6. Pte. Peter Werema,
7. Pte. Fortunatus Msofe.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kwenye mtandao ni kwamba askari hao walikwenda kujaribu kumwokoa mwenzao (ambaye hakutajwa) ambaye alisemekana kutekwa na vikosi vya waasi nchini humo.

Wakati wakijiandaa, ghafla walizingirwa na askari hao waasi na kisha kushambuliwa kwa risasi hadi kufa.

Haikufahamika hali ya askari huyo ambaye alidaiwa kutekwa kama bado yu hai ama ni miongoni mwa waliokufa.

Mungu azilaze roho za askari wetu mahali pema peponi, Amina.

hilo jina la blue limenishtua sana.Nafuatilia kujua kama huyu ndiye ninayemfahamu au kuna makosa katika uandishi.So sad news indeed.
 
Hii ni habari mbaya. Nawapa pole Watanzania wenzangu na familia za marehemu kwa ujumla. DARFUR ni eneo la hatari, nashukuru nilikwenda huko na kumaliza kazi yangu salama some 2 years back.

Tiba
 
This is a sad news; nawapa pole familia za marehemu wote, JWTZ na Watanzania wenzangu kwa pigo hili. Moyo wangu ulishtuka kwani nina dadangu ambaye yuko huko kwa kazi hii. Mungu azilaze pema roho za marehemu na kuwafariji familia.
Khaa!! Mzee Mwanakijiji kwani hao sio kaka zako?

:disapointed:
 
usisikitike na waislamu jisikitikie mwenyewe. Uislam hupigania haki,na hao wamekufa wakipigania haki kwa wazee,watoto,wanawake na vilema vinavyotokana na majeshi ya waasi kuangamiza watu wasio na hatia. hao ni peponi moja kwa moja hasa ukizingatie kwa mwezi huu
Nasikitika nahao waislam
mauti yamewakuta katika mwezi mtukufu Wa ramadhani walitakiwa wafanye
ibada
 
This is a sad news; nawapa pole familia za marehemu wote, JWTZ na Watanzania wenzangu kwa pigo hili. Moyo wangu ulishtuka kwani nina dadangu ambaye yuko huko kwa kazi hii. Mungu azilaze pema roho za marehemu na kuwafariji familia.

Pole sana mzee, kwa kuwa nakuaminia sana kwa busara, hebu tuambie AMANI HUA INALINDWA!!!!?
 
Hii ni habari mbaya. Nawapa pole Watanzania wenzangu na familia za marehemu kwa ujumla. DARFUR ni eneo la hatari, nashukuru nilikwenda huko na kumaliza kazi yangu salama some 2 years back.

Tiba

Uliweza kuilinda amani!!!!
 
Pole sana mzee, kwa kuwa nakuaminia sana kwa busara, hebu tuambie AMANI HUA INALINDWA!!!!?

JK rudisha jeshi nyumbani!
Hatupati chochote huko zaidi ya sifa ya kuitwa"polisi wa Africa"!Nchi zingine waki calculate na wakikokotoa kama hamna any economic gains hawapeleki jeshi!

Rais wangu JK pls warudishe vijana home!
 
Polis konstebo mohamedi
Tambua uwepo wa marehemu wafuatao Koplo Oswald Chaula,Pte Peter Werema,Pte Rodney Ndunguru,Pte Fortunatus Msofe.Koplo Kimaro, Afande Massawe na Konstebo Shirima walikuwa eneo lengine la kazi.Mungu azilaze mahala pema roho za marehemu
 
Majina ya askari saba wa Tanzania waliokufa kwenye shambulio la ghafla mjini Darfur yamepatikana.

2.png

Askari hao waliokufa ambao walikuwa kwenye vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa huko nchini Sudan ni :-
1. Sajenti Shaibu Othuman,
2. Koplo Oswald Chaula,
3. Koplo Mohamed Juma,
4. Koplo Mohamed Chikilizo,
5. Pte. Rodney Ndunguru,
6. Pte. Peter Werema,
7. Pte. Fortunatus Msofe.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kwenye mtandao ni kwamba askari hao walikwenda kujaribu kumwokoa mwenzao (ambaye hakutajwa) ambaye alisemekana kutekwa na vikosi vya waasi nchini humo.

Wakati wakijiandaa, ghafla walizingirwa na askari hao waasi na kisha kushambuliwa kwa risasi hadi kufa.

Haikufahamika hali ya askari huyo ambaye alidaiwa kutekwa kama bado yu hai ama ni miongoni mwa waliokufa.

Mungu azilaze roho za askari wetu mahali pema peponi, Amina.

Wapumzike kwa amani, taifa na dunia kwa ujumla itawakumbuka daima kama mashujaa wa kimataifa na wazalendo waliojitolea kulinda amani. R.I.P makamanda
 
Upumbavu upi? unayafurahia mateso wanayoyafanya wanajeshi huko Mtwara?

Usilihukumu Jeshi letu loote kwa matukio ya Mtwara tu, ambayo hata hivyo msemaji mkuu wa jeshi aliyakana (ishara ya kuwa wanajua kuwa si mazuri na yanakera) bali jaribu kukumbuka pia jeshi hili linavyowajibika kwa wananchi patokeapo maafa kama vile mafuriko, kuvunjika madaraja nk hata wananchi walipoteseka kwa kukosa huduma za afya kutokana na migomo ya madaktari Jeshi hili liliwajibika, huwezi jua kama katika hao waliokufa waliwahi kuwajibika kuwahudumia wananchi wakati wa maafa, sasa ukiwasema vibaya kwa sababu ya wanajeshi wachache washenzi wa kule Mtwara huoni itakuwa si kuwatendea haki? Kuhusu kwenda Sudan, hilo ni jukumu la kimataifa la kijeshi, wakifanya vizuri ni heshima kwa nchi yetu, tusisahau hata sisi tulipopata matatizo ya uasi 1964 wanajeshi kutoka nje (Nigeria na Uingereza kama sikosei) walikuja kulinda amani hapa kwetu, na walifanikiwa kuweka mambo sawa, ni
jukumu la kiungwana sana. Naungana na familia za marehemu mashujaa hao kuomboleza vifo vyao, pamoja na kukerwa sana na matukio ya Mtwara, bado nina Imani sana na JWTZ, tofauti kabisa na Jeshi letu la Polisi linalotumiwa vibaya kabisa na wanasiasa na wenyewe kukosa uadilifu.
 
Duh polisi tena? Ni polisi hawa wa IGP Mwema ama ni Military Police (MP) wa Gen. Mwamunyange?

Yes, Askari wa jeshi la Polisi.Kwa mafunzo ya Kipolisi ya Tanzania askari kama FFU(kikosi maalum) wanafundishwa mambo mengi ya Kijeshi hivyo si ajabu kushiriki operation kubwa.

Hata hivyo kwenye UN peace keeping Polisi hujumuishwa maana kuna mambo mengine ya kiulinzi yanahitaji Polisi.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Mkuu, naamini Ng'wanangwa ameliweka vizuri hili. These people have died for the cause which Tanzania believe it is worthy fighting for and so they have died for the country.

Watanzani tuliulizwa lini na wapi na nani kama tuwapeleke ugenini kaka na dada zetu wenye silaha kwenye mgogoro tunaolazimisha kutuhusu!!!!!?

Ni mashujaa tu kwa kuwa wamefia zinapopigwa bunduki, lakini sababu ya kufa kwao hawakuisomea, yaani mwwnzio anaweza kukushambulia lakini wewe huruhusiwi hii ni kuwapeleka ndugu zetu wauwawe. WARUDISHENI NYUMBANI WALIONUSURIKA.
 
Poleni makamanda wetu.Mungu awape moyo wa uvumilivu ndugu na jamaa zao.
 
Ulichokiandika hapa siyo mahali pake nafikiri ungesubiri kutoa machungu yako kwa sasa tuungane na ndugu na jamaa kwa ajili ya kuwaombea hawa hata wewe kuna mabaya unayoyafanya. Hawa walienda kuwakilisha taifa na wala hawakutumwa na wanasiasa. SIYO KILA KITU SIASA NDUGU
Hapo kwenye red marehemu haombewi mtu anajiombea mwenyewe akiwa hai.
 
Wapumzike kwa amani jamani, so sad
Mungu awape nguvu familia za marehemu
 
Back
Top Bottom