Majina saba ya askari walio uwawa Sudan

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,697
8,843
Majina ya askari saba wa Tanzania waliokufa kwenye shambulio la ghafla mjini Darfur yamepatikana.

IMG_0036.JPG

IMG_0058.JPG

Askari hao waliokufa ambao walikuwa kwenye vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa huko nchini Sudan ni :-
1. Sajenti Shaibu Othuman,
2. Koplo Oswald Chaula,
3. Koplo Mohamed Juma,
4. Koplo Mohamed Chikilizo,
5. Pte. Rodney Ndunguru,
6. Pte. Peter Werema,
7. Pte. Fortunatus Msofe.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kwenye mtandao ni kwamba askari hao walikwenda kujaribu kumwokoa mwenzao (ambaye hakutajwa) ambaye alisemekana kutekwa na vikosi vya waasi nchini humo.

Wakati wakijiandaa, ghafla walizingirwa na askari hao waasi na kisha kushambuliwa kwa risasi hadi kufa.

Haikufahamika hali ya askari huyo ambaye alidaiwa kutekwa kama bado yu hai ama ni miongoni mwa waliokufa.

Mungu azilaze roho za askari wetu mahali pema peponi, Amina.
WOUNDED+TZ+PEACEKEEPERS+AT+NYALA+PAKISTAN+LEVEL+III+HOSPITAL.jpg

VISITING+A+WOUNDED+UN+PEACEKEEPER.JPG
UNAMID+20130714+Albert+Gonzalez+Farran+JSRVisitKhorAbeche+360.JPG
JW-+Dafur.jpg
Darfur-jw.jpg
UNAMID+20130719+Albert+Gonzalez+Farran+JSRVisitKhorAbeche+217.jpg
UNAMID+20130719+Albert+Gonzalez+Farran+JSRVisitKhorAbeche+240.jpg
UNAMID+20130719+Albert+Gonzalez+Farran+JSRVisitKhorAbeche+262.jpg
UNAMID+20130715+Hamid+Absulsalam+RepatriationCoffinsElFasher.jpg
 
attachment.php

Vifo hivi viwakumbushe wanajeshi wetu kwamba watanzania wote ni ndugu na kwamba sote ni mavumbi na mavumbini ni lazima tutarudi. Mateso wanayoyafanya wanajeshi kwa raia wa Mtwara ni ya kinyama!!! Si ya kiutu hata kidogo!!! Ni bahati mbaya kwamba jeshi letu linatumiwa vibaya na wanasiasa!!! Mungu aturehemu sote na roho za wanajeshi hawa zipumzike kwa amani!!
 
Roho za marehemu zipate rehema kwa Mungu na wapumnzike kwa amani
Kwa wale majeruhi tunaomba mwenyezi Mungu awajalie kupona kwa haraka na awapunguzie maumivu
 
Nasikitika nahao waislam mauti yamewakuta katika mwezi mtukufu Wa ramadhani walitakiwa wafanye ibada
 
Inatia uchungu kweli kwa hawa ndugu zetu kupoteza maisha, kinachosikitisha ni pale fedha wanazotakiwa kulipwa wanejeshi hawa viongozi wa juu wanazifanyia ubadhirifu tukumbuke yule kiongozi wa juu wa jeshi mwenye tuhuma za kuhifadhi fedha uswiss na fedha zenyewe ni malipo kwa wanajeshi waliokuwa katika ulinzi wa amani kama hawa ambao leo wamepoteza maisha yao.hii inasikitisha tena saana.
 
This is a sad news; nawapa pole familia za marehemu wote, JWTZ na Watanzania wenzangu kwa pigo hili. Moyo wangu ulishtuka kwani nina dadangu ambaye yuko huko kwa kazi hii. Mungu azilaze pema roho za marehemu na kuwafariji familia.

very sad indeed
 
Inatia uchungu kweli kwa hawa ndugu zetu kupoteza maisha, kinachosikitisha ni pale fedha wanazotakiwa kulipwa wanejeshi hawa viongozi wa juu wanazifanyia ubadhirifu tukumbuke yule kiongozi wa juu wa jeshi mwenye tuhuma za kuhifadhi fedha uswiss na fedha zenyewe ni malipo kwa wanajeshi waliokuwa katika ulinzi wa amani kama hawa ambao leo wamepoteza maisha yao.hii inasikitisha tena saana.
Ni kweli mkuu,ngoja tuone kama watazisaidia familia zao.Maana that's what's important now.
 
Ndugu zetu wa kwenye majeshi , KIFO kiwe ni sehemu ya kutukumbusha kuwa sisi wote tutakufa, ni vema tuwatendee vema wenzetu raia , nawaombea marehemu hao wapate pumziko la milele la amani na Taifa letu liendelee kuwa na amani, utu na umoja.
 
Kuna ushahidi gani uliotumika kueleza jinsi walivyoshambuliwa..? au kuna walionusurika kufa...?
R.I.P our beloved Tanzanians.
 
kama Vipi warudi tu nyumbani, haiwezekani wao washambuliwe halafu wazuiwe kujibu mapigo.!!!!!
 
ndiyo. wametoka Tanzania, wameifia Tanzania.

Mkuu mbona unajibu kwa haraka haraka hivyo?si tunaeleweshana mkuu?

Ninavyoelewa hao ni mchango wa Tanzania UN,kwahiyo mission yao inaratibiwa na UN.

Sisi kama Tanzania hatuna mission ya kusapoti upande wowote huko Darfur Sudan.

Labda tuseme wameifia freedom and justice,lakini si Tanzania,unless uniambie walikuwa wakiipigania Tanzania,mipaka yake ama interests zake.

Na ndiyo maana wengine tunataka kuona wanafamilia wao wanakuwa taken care of kwasababu nasikia kuna malipo ambayo wakubwa wanayakinga.
 
attachment.php

Vifo hivi viwakumbushe wanajeshi wetu kwamba watanzania wote ni ndugu na kwamba sote ni mavumbi na mavumbini ni lazima tutarudi. Mateso wanayoyafanya wanajeshi kwa raia wa Mtwara ni ya kinyama!!! Si ya kiutu hata kidogo!!! Ni bahati mbaya kwamba jeshi letu linatumiwa vibaya na wanasiasa!!! Mungu aturehemu sote na roho za wanajeshi hawa zipumzike kwa amani!!

Hayo maneno uliyoandika hapo chini ni upumbavu na kukosa akili kuliko pitiliza.
Rest in peace askari wetu. Mmekufa kishujaa
 
Back
Top Bottom