Kwanini maeneo haya yalipewa majina ya hivi?

Afrika sana : Kuna yule mama anayeuza vitenge al maaruf kama Africa Sana
Sinza Mori: Kuna baa inayoitwa Mori
Sinza kwa Remmy: Alikuwa anakaa Remmy Ongala
Sinza Palestina: Kuna hospitali ya wapalestina sasa hivi ni ya Kata
Mwenge: Kikosi cha sanaa na JWTZ
Salasala: Ni kama ilivyo kwa Ilala
Bunju: Kulikuwa na soko la samaki, wengi walikuwa ni samaki aina ya Bunju
Goig : Getting Old Is Growing ni makao makuu ya NGO ya wazee
Makonde: Kulikuwa na uwanja wa Wamakonde wakicheza ngoma pale
Jogoo: Kiwanda cha sembe chapa Jogoo
Mabibo: Maarufu kwa Matunda ya Mikorosho (Mabibo)
Oysterbay: Oyster ni aina ya shells za baharini, zilikuwa zinapatikana kwa wingi
Shekilango: Mzee maarufu alikuwa anaitwa Shekilango
Ilala: Kutokana na Makaburi ya Kiislam, wakienda zika wanasema La Ila Illah
Ilala Boma: Ofisi ya mkuu wa wilaya Ilala, Bomani
Makumbusho: Kijiji cha Makumbusho
Victoria: Kulikuwa na Jengo linaitwa Victoria House
Mikocheni: Ni aina ya mimea inayoitwa Mikoche ilikuwa mingi
Samaki wabichi: Mzee Choggo alikuwa anauza samaki wa maji baridi - samaki wabichi
Tangi Bovu: Kulikuwa na tangi la maji la chuma lililoharibika kwa kutu
Kariakoo: Ilikuwa kambi ya wapagazi, carrier corps.
 
Ila kweli husband wako drphone yupo deep sana na anawakilisha vyema ila akirudi home nite umuulize amejuaje maana za maeneo yote haya isije ikawa ndio small house zake zote zimo humo. Asante


ss ndugu unaingilia wizara ya mambo ya ndani utaharibu hali ya hewa
 
Keko Magurumbasi
Magomeni
Afrika sana
Sinza Mori
Sinza kwa Remmy
Sinza Palestina
Mwenge
Mbezi Louis
Africana
Kijitonyama
Ubungo Kibangu
Ubungo Maziwa
Manzese
Tandale
Temeke
Kunduchi
Kimanzichana
Mbagala
Salasala
Kibamba
Kibamba Magarisaba
Kibaha
Buguruni
Kinondoni
Madale
Bunju
Boko
Tegeta
Goig
Makonde
Jogoo
Mabibo
Masaki
Oysterbay
Gongo la mboto
Ukonga
Kipawa
Chanika
Kigamboni
Mwanakwerekwe
Mkunazini
Mbagala Charambe
Shekilango
Sinza Mugabe
Sinza Mapambano

Chang’ombe
Ilala
Ilala Boma
Kurasini
Makumbusho
Victoria
Mikocheni
………..na maeneo mengineyo wenye kujua maana yake waweke hapa tuelimike na kujua maana ya sehemu tunazoishi


GOIG - Ni ikifupisho cha "Getting Old Is to Grow". Hapo kuna kituo cha wazee ambao wanajishughulisha na kazi mbalimbali (pale Mbezi Beach).

MAKONDE - Kwa siku za nyuma kidogo (miaka ya '90) kulikuwa na Wamakonde wakichonga Vinyago. Kwa sasa wamehamia pale Mwenge (sam Nujoma rd).

SHEKILANGO - Huyu alikuwa ni waziri enzi za Mwalimu, barabara hiyo imepewe jina kwa kumbukumbu yake, kama ilivyo kwa AH Mwinyi rd ama Bibi Titi rd ama Nyerere rd.

SINZA MUGABE - Hapo kuna shule ya msingi Robert Mugabe, kama kumbukumbu ya mpigania uhuru wa Zimbabwe.

ILALA BOMA - Hapa kuna ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ilala (kimsingi ofisi nyingi- kama si zote--za wakuu wa wilaya zinaitwa Bomani)

MAKUMBUSHO - Hapa kuna nyumba za ukumbusho za asili za makabila mbalimbali ya Tanzania, mnakaribishwa kupatambelea ili mjue historia ya nchi hii.

Idimi

 
Samaki wabichi kuna mtu alikuwa anauza samaki fresh pale, wengi walienda kununua kwake na wakapafanya jina Samaki wabichi. Mwanzoni kilikuwa ni kituo cha msaada kwa daladala, kwa sasa ni kituo maarufu tu isipokuwa kwa makonda wabishi ambao hukifanya kituo cha kupakia lakini sio kushushia abiria.

Leka,
Huyu mama rasta bado yupo Mbezi Beach ila alishaacha kuuza samaki, anamiliki baa, ila kwa sasa kahamia pale Super, kituo kimoja kabla hujafika Makonde. Anaitwa Nguse (aka Ngusekela).
 
Nimegonga sana bra
Bado kuna maeneo kama
Tegeta Kibaoni
Lufungira
Mtoni Kwa Aziz Ally
Temeke Mikoroshoni
Tabata Bima
Tabata Aroma
Tabata Segerea
Tabata Kisukulu
Tabata Kimanga
Manzese Uzuri


rudi nyuma pitia post gonga thanks tunaendelea
 
Sinza shekilango...ni jina la mmoja wa waliokuwa viongozi kabla na baada ya uhuru wa Tanganyika alikuwa akiitwa Hussein Shekilango nasikia huyu bwana alifariki kwa ajali ya ndege kaskazini mwa Tanzania na Mwl. Nyerere kwa heshima na kumbukumbu ya Shekilango akaagiza ile barabara ipewe jina lake!

E bwana mkuu,Mzee Shekilango bado yupo hajafa.
 
Ina maana kuwa hamjui maana ya sehemu mnazoishi??? ajabu kweli hii

Sipo Mwanangu pale Faya Zama zile palikuwa panaitwa Mwembe Mawazo kulikuwa na kituo cha kwenda Bwagamoyo(sasa Bagamoyo) sasa kulikuwa kuna miembe miwili mikubwa sana na palikuwa ndio stand ya mabasi yakwenda huko bwagamoyo na sasa baada ya kuing'oa na kujenga Kituo cha Faya sasa panaitwa Faya.

Mungu akubariki.
 
Tabata
Kulikuwa na Mwarabu anafuga ng'ombe wa maziwa, ikawa ameajiri watu wa kuuza maziwa yake huko mjini (kariakoo). Sasa walikuwa wakimdai malipo jamaa anashindwa kusema utapata pesa yako, akawa anasema "u-tabata", basi watu wakaanza kumwita tabata. Tangu hapo hadi leo kunaitwa tabata.
 
Back
Top Bottom