Majina gani haya; Uwanja wa Taifa, Timu ta Taifa,....

Kichankuli

JF-Expert Member
Dec 18, 2008
887
189
Hivi kweli hatuna majina katika nchi hii ya Watanganyika na Wazanzibar yenye makabila lukuki na vivutio kibao kiasi kwamba tunarudia kulitumia jina ambalo halina utambulisho wowote kwa nchi hii. Eti "Uwanja wa Taifa", taifa gani hilo; Iraki au Zimbabwe!!!, mara kumi hata huo uwanja mpya ndo tungeuita Uhuru. Hebu tuangalie wenzetu:

1) Kenya -wana Uwanja uitwao Kasarani, Nyayo, n.k.
2) Uganda-Nakivugo
3)Uingereza-Wembley

Sasa sisi tumekazania majina yasiyo na utambulisho; Uwanja wa Taifa, Timu ya Taifa, Shirika la Bima la Taifa, Shirika la Nyumba la Taifa, Benki ya Taifa ya Biashara, Televisheni ya Taifa TVT (afadhali hapa ujio wa Tido ulileta mabadiliko na kuwa Tanzania Brodcasting Corporation).

Yumkini hii ndo sababu hata hii timu yetu haifanyi vizuri kutokana na kuwa na jina lisilojitambulisha. Aidha yawezekana ndo maana hata Taasisi za nchi hii kama vile NBC hutolewa kwa bei chee kwa wageni kwa vile hata wao huonekana kama sehemu ya taifa.

Nashauri Wizara inayohusika na michezo ingeanzisha lau shindano la kufikiria na kubuni jina ambalo lingefaa kwa uwanja mpya uliokabidhiwa jana kwa Rais Kikwete pamoja na jina la Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom