Majibu ya Sitta kwa Dr Slaa: Asema Dr Slaa Mnafiki, Dikteta

Huyu mzee kichekesho kweli kweli. Amesema aliombwa agombee URAIS kupitia CDM akakataa. HAH HAH , then akaombwa tena ijiunge na CCJ . Hivi yeye mbona yuko hivi? Mara CCJ mara CDM mara CCM na sasa utasikia siju ADC sijui. Ama kweli mbabaishaji ni mbabaishaji tuuu.

Kuna taarifa kuwa ana mkono wake ADC akishirikiana kwa ukaribu na Hamad Rashid Mohd
 
Tofauti na watu wengi wanvyochukulia mambo kwa mtazamo wa kichama chama
Lakini sisi tunaochukulia mambo kwa jicho la uhalisia Mh Sita amejibu vyema kama mtu aliyekomaa kisiasa

Tatizo lililopo hapa JF ni kwamba wengi wetu ni wanazi wa CDM hatuoni hatusikii na kuthibitisha hilo hata Sita angejibu kwa kuuomba radhi uongozi wa CDM bado comments zetu zingekuwa ni hizi hizi tu, mnafiki,mroho wa madaraka nk nk kwasababu tu Sita ni CCM

Hapa swala la msingi la kujiuliza ni je kama kweli Sita alikuwa anazima mijadala,fisadi,mroho wa madaraka na tuhuma zote alizotupiwa na Dr na wana JF, je hawakulijua hilo akina Dr hadi wakubaliane naye awe mgombea wao wa urais?
Au baada ya kuwatosa kama Dr salaa alivyothibitisha kwenye madai yake ndio wamemuona fisadi.

Kama CDM walifikia kuwa tayari kumpisha kiti cha urais kilaini hatuoni hii ni sababu Sita anaona CDM hakuna safu kubwa hadi wanaanza kuvizia kurubuni viongozi makini toka vyama vingine

Hivi sasa mijadala mingi humu JF inakosa nguvu na kuwa ya upande mmoja tu, watu wanataka kusikia mabaya ya CCM na mazuri ya CDM tu, kwenda kinyume na hapo wewe ni msaliti na hufai kwenye hii jamii

Tujadili kwa jicho la upande wapili pia kama nilivyoainisha hapo juu
Maana sasa isije ikawa hata hoja za msingi zinazohitaji mjadala zikazimwa kwakuwa tu CCM ni mafisadi
Teh teh...mchangiaji hujaangalia kwa makini mambo yanayomzunguka 6.Hayo maneno anayoshutumiwa nayo si CDM pekee,CCJ,CCM na hata Watu wengine wanaohisi alikuwa kiutaka Uwaziri mkuu wa Lowasa.Wote hao wana life experience na eveidences.

Suala la kurubuniwa au kuonekana kuwa makini, hata mimi nilikuwa mshabiki mkubwa sana wa siasa zake na utendajiw ake bungeni.Hata alipoondolewa kwa njia ambayo hatukuridhika niliumi ana kulaumu sana.Huyu mzee alitread issue ya richmond kwa haraka na kwa vile ilikuwa ndio issue hot basi alipata nafasi ya kufaidika nayo kisiasa.Hata watu wa mataifa mengi ambao nipo nao karibu walikuwa wakimtaja katika vijiwe vya Coffee kuwa anaonyesha mwelekeo wa kusaidia bunge kuwajibisha serikali.Na hii ilifanya wapeleke ripoti njema katik nchiyao kuwa wasisimamishe misaada kwa vile kuna makundi ya kizalndo kila sehemu yanayopigana na rushwa.Kwa hiyo kusimamisha misaada kungewavunja moyo hawa wazalendo.Lakini kwa matamshi ya Dr. Slaa, Mpendazoe na hata zake mwenyewe ni wazi kuwa Issue alizizimisha ila richmond aliipenda kwa vile ingemmaliza mtu anayemwogopa sana katika kinyanganyiro cha urais n apengine kuutaka uwaziri mkuu wake.Ni wazi kuwa sifa alizopata hati richmond zilimganya hata yeye mwenyewe awe too naive, aamini kuwa nae ni sehemu ya wapiganaji.Na hapo ndipo alipovuta interest za CDM , kama CDM walishamwekea nafasi ni kwamba CDM hakuna tamaa ya madaraka.Sasa mzee akiwa na CCJ na CCM huku anaongea na CDM tayari akili yake ilishajisahau na kulewa sifa akidhani ni nobel na hivyo kufanya hizi blunders.

Kwa haraka utaona kuwa 6 hakuwa akijiamini,hakuwa na hakika kama ama CCJ au CDM wanaweza take off haraka na kumhakikishia urais ndipo akaona akae mguu mmoja nje mmoja ndani.Kama vile watu wanaopenda anzisha makampuni huku wakitegemea kuwa yatajengwa na wengine yakifanikiwa ndio waache kazi na kuingia kuvuna,ikifa waachane nayo.huku ni kuwa opportunist.Mbaya 6 alijiweka pabaya zaidi baada ya kujua hayo hayajajulikana wazi ila akafanya makosa ya kulazimisha cdm wayaseme hayo na kuhatarisha hatima yake kisiasa hata ndani ya CCM.Hayo ni makosa yake na anapaswa kujutia mwenyewe.

Sijui kwa kiasi gani sita ataweza silence haya mambo kwani hata akishinda CCm itamtosa tuu kwani atakuwa keshachafuka sana.n ahivyo kuwa si asset tena zaidi ya liability.Ni bahati kwa CCM kwani kajitoa mhanga mwenyewe na hivyo wana CCM wengine hawahitaji kuingia majukwaani kushindana na wapinzani.

Sasa mzee anakanusha kuwa hakusema kuwa mbowe hana taaluma ningine zaidi ya U-DJ ,sasa anaongelea kuwa alisema ni mchango wake katik burudani hauwezi sahaulika.Sidhani kama watu hata wamesahau hilo na huku zipo reference kibao.Mzee kajiweka katik spin, na kila mtu anamzungusha,kajiweka katika mazingira ya kukimbizana na matukio.kajiweka katik vita binafsi na kila kiongozi wa CDM na wa CCM. wakati vita kamili ni kati ya CDM na CCM mwisho wa siku.sasa fikiria hao viongozi wote wapokezane kumtandika atakuwa na hakika gani ya kupata ridhaa ya CCM kumchagua?Na hata wakimchagua tayari atakuwa na makovu ya viongozi wa CDM +wapinzania wake nadani ya CCM, ukiweka na makovu ya CCM tayari atakuwa amesafisha njia kwa CDM.

Kosa ni mzee hakuweka tahadhari na exit door,kwa kila jambo.sasa akijitoa ni kuwa kashindwa, na akiendelea anakwenda malizwa na kudhalilishwa.

Sioni njia nyepesi ya mzee kutoka.Pengine aanze kujijengea misimamo na aisimamie huku akiangalia upepo unavyokwenda ili ajenga exit plan toka katika haya malumbano.
 
Sitta bora ungenyamaza mzee wangu. Maana unanuka ccm sasa unanyea kambi na huku utakimbilia wapi? Jiulize kiswali kidogo ikiwa ulienguliwa kwenye uspika na ccm wakasema wanataka mwanamke sasa huo urais ni ccm ipi itakupa? Vipi mbona hoja zako hazina huchambuzi wa kina? Mzee vipi issue yako ya kulishwa sumu swahiba wako imefikia wapi?
Ngoja dr aje akujerui sasa umeyataka mwenyewe
 
Hata hivyo nimefarijika kuwa alikuwa tayari kuingia chadema, ndio maana akasoma katiba yake na kujifanya hakuridhishwa nayo. Mara alitaka kwenda ccj, kweli huyu ni mroho wa madaraka
 
Hata hivyo nimefarijika kuwa alikuwa tayari kuingia chadema, ndio maana akasoma katiba yake na kujifanya hakuridhishwa nayo. Mara alitaka kwenda ccj, kweli huyu ni mroho wa madaraka
ha ha...nadhani pia hiyo katiba aliisoma hata kabla ya kuongea nao.katiba zinapatikana hata kwa watu wasio wanachama.Sasa kwanini asiikatae kabla ya kuongea ,baadaya ya kuongea inamaada kuwa kilichomsinda si katiba ni mazungumzo.Au hata tamaa yake iliyomnyima ondoka katik bwawa la hela za CCM.
 
Hata hivyo nimefarijika kuwa alikuwa tayari kuingia chadema, ndio maana akasoma katiba yake na kujifanya hakuridhishwa nayo. Mara alitaka kwenda ccj, kweli huyu ni mroho wa madaraka

kwa ufupi, HAJITAMBUI
 
Ni kweli ni kundi dogo ila linajaribu kujitutumua. Kama unataka kuwa mfuasi wa hili kundi think twice, read their impact on the ground then predict the future.
Dont be easly captured by mob psychology, think and decide individualy.
Wacha umma uamue kwa manufaa yake yenyewe na sii kuipa umma nini iamue, hayo si maamuz ya umma, mwisho wa siku umma lazima utakugeuka baada ya kugundua wanayoyasimamia si yao bali ni mawazo yako/yenu umepandikiza kwao ili waamue kama yao ilhali si yao ni yako. Baada ya kugundua maumiv na gharama walizolipa na si maamuz yao lazima hasira zao zitakugeukia na hapo itakuwa maamuzi ya umma. Remember "un enemy of the people" read this book u'l know the future of what happen on the ground today.
 
Wewe nae mwepesi kweli! Yan ndio haya maneno ya kutete mtu?

Jana kamsifu slaa na kumponda Mbowe
leo kamponda slaa

huyu mtu ana msimamo gani?

Hakuna pahala alipomponda mbowe unless hujasikia wala kusoma alichosema,najua watz wengi hatuna kusema,kukusaidia tu ni kwamba kuhusu mbowe alichofanya mzee six ni kuelezea mchango wa mhe.mbowe katika tasnia ya burudani akiwa ni mdau mkubwa sana wa mambo ya burudani,na kwa mliochelewa kuja Dar es salaam mpaka baada ya kubebewa na mbeleko ya kuja kujiunga chuo kikuu ni kwamba mboe na mambo ya burudani za disco hawakukutana barabarani bali amekulia kwenye hayo mambo,sasa nivigumu kutaja cv ya mbowe bila ku mention uhusiano wake na mambo ya disco kwani ndio iliyomkuza kabla ya kuingia kwenye politics,huo ndio ukweli hata kama tunahisi haipendezi kwa mwenyekiti wetu kuonekana ni mtu wa disco,na wala si dhambi,kuna rais wa madagascar ANDRY RAJOLINA yeye alikua dj kabla lakini leo ndio rais wa madagascar kwa kuwa urais hausomewi.Hiyo haina haja watu wa chadema kujisikia unyonge kutokana na mwenyekiti wenu kuwa mtu wa disco.
 
Tofauti na watu wengi wanvyochukulia mambo kwa mtazamo wa kichama chama
Lakini sisi tunaochukulia mambo kwa jicho la uhalisia Mh Sita amejibu vyema kama mtu aliyekomaa kisiasa

Tatizo lililopo hapa JF ni kwamba wengi wetu ni wanazi wa CDM hatuoni hatusikii na kuthibitisha hilo hata Sita angejibu kwa kuuomba radhi uongozi wa CDM bado comments zetu zingekuwa ni hizi hizi tu, mnafiki,mroho wa madaraka nk nk kwasababu tu Sita ni CCM

Hapa swala la msingi la kujiuliza ni je kama kweli Sita alikuwa anazima mijadala,fisadi,mroho wa madaraka na tuhuma zote alizotupiwa na Dr na wana JF, je hawakulijua hilo akina Dr hadi wakubaliane naye awe mgombea wao wa urais?
Au baada ya kuwatosa kama Dr salaa alivyothibitisha kwenye madai yake ndio wamemuona fisadi.

Kama CDM walifikia kuwa tayari kumpisha kiti cha urais kilaini hatuoni hii ni sababu Sita anaona CDM hakuna safu kubwa hadi wanaanza kuvizia kurubuni viongozi makini toka vyama vingine

Hivi sasa mijadala mingi humu JF inakosa nguvu na kuwa ya upande mmoja tu, watu wanataka kusikia mabaya ya CCM na mazuri ya CDM tu, kwenda kinyume na hapo wewe ni msaliti na hufai kwenye hii jamii

Tujadili kwa jicho la upande wapili pia kama nilivyoainisha hapo juu
Maana sasa isije ikawa hata hoja za msingi zinazohitaji mjadala zikazimwa kwakuwa tu CCM ni mafisadi

Mzee unapoteza muda,akili na busara zako nyingi ulizonazo kuyasema hayo,watu wa chadema wengi ni illiterate hawatakueewa zaidi y kukimbilia kukukejeli na kukutukana,mzee sitta katoa hoja za msingi sana kwa watu walioelimika wamemuelewa kirahisi sana tena katumia maneno mepesi akijua kabisa ni watu wa aina gani ana deal nao ambao wanachukua muda mrefu sana kuelewa
 
Katika safari ya ukombozi mengi yanaweza semwa, kubwa ni suala la kukatishana tamaa. Kwa wapiganaji kwao kila tendo ni hatua ya kuelekea ukombozi. Mvua ije, jua liwake- bado vita ni lazima isonge mbele. Walio katika safu ya ukombozi ni wakati wa kusonga mbele, kujibizana na watu ambao wameshachoka ni kupoteza muda.
 
Hii kali ana haki ya kuzungumza lakini anaona anaenda nje ya mstari hivi kuongoza lazima utoe viongozi kwenye chama chako? Haiwezekani kabisa kuteua au kumchagua mtu ambae hajihusishi kwenye vyama kuwa kiongozi mahali fulani, hata kama katiba inalazimisha hivyo hakuna namna ya kubadilisha tukawa na mfumo bora zaidi wa kuchagua viongozi? Hizi fikra mgano zinaturudisha nyuma.
 
Nimesoma maelezo ya Siita na sasa naamini kweli mzee huyu Mnafiki bora hata asingejibu tuhuma za Dr.Slaa kwa sababu zimedhihirisha wazi kwamba MNAFIKI..

Kwanza hata kama Chadema walimfuata na kumuomba yeye agombee urais na sio wazo lake, ile kuchukua nafasi tu ya kufikiria, kukaa na kuongea na watu wako kuhusu nafasi hiyo tayari kunamweka ktk Unafiki maana alifanya haya kinyume cha maadili ya uongozi. Inaonyesha anaweza kununuliwa kwa kupewa ahadi ya cheo.. Swali kwake kwa nini alipofuatwa na CCM haku report mchezo ule kwa Uongozi wake wa chama iusipokuwa amekaa pembeni na kufikiria kujiengua chama kilichompa madaraka makubwa ya uongozi..

Halafu nikirudi ktk swala la ELIMU na AFYA bure huyu mzee alikuwa ktk serikali ya Mwalimu Nyerere na maajabu kiitikadi alikubali uwezekano wa Elimu na Afya bure. zaidi ya hapo zipo hotuba zake mwenyewe zilizoashiria uwezekano wa kutoa huduma hizi bure.. Inakuwaje leo huyu huyu mtumishi wa seirkali ya Mwalimu hadi JK leo anasema haiwezekani na haamini kama ni kazi ya serikali kutoa huduma hizi bure, kwa maana hiyo anasema ELIMU sio Human right na hivyo kupingana itikadi ya chama chake mwenyewe na muda wote alotumikia ilikuwa uongo na kuikarifu nafsi yake. Hakuna human right inayokuja kwa gharama ya mhitaji hata siku moja.. Unless yeye anaweza kutuambia ni wakati ganichama chake kimeichukua elimu kama ni human rightna msingi wa ujenzi wa Taifa. Mzee wangu Sitta sijui nani amekushauri kutoa majibu haya ambayo kwa uhakika yamekushusha vibaya sana.. yaani tofauti kabisa na jinsi nilivyojkuwa nikikuchukulia ama kwa kiasi fulani sikupenda jinsi Dr.Slaa alivyomwaga ugali...

Mkuu Mkandara kuwa kiongozi au mwanachama wa chama fulani hakukuondolei haki yako kisheria kujadili, kutaka kuhama au kuanzisha chama kingine
Hihi si kigezo cha unafiki au usaliti mkuu, maadam kama kila kinachofanyika nyuma ya pazia kingewekwa hadharani kwenye siasa sidhani kama kuna mwanasiasa ungemuamini kwa kigezo hicho
Rejea tu ni mara ngapi Dr Slaa amesema alifuatwa na CCM wakati wa kampeni? Au Lema nk

Kuhusu elimu na afya ma blah blah zingine kuwa bure alichosema sita hakumaanisha haiwezekani kabisa hapana, alichomaanisha ni kwamba CDM inawahadaa wananchi wakati haioni huo mpango wao kama unatekelezeka kwa maana hawatoi muainisho wa mapato zaidi ya kukimbilia maliasili tu kama kigezo cha huduma bure

Wengi wetu tunapenda kukimbilia mifano ya Nyerere tumetia pamba masikioni na tujitia upofu hatutaki kuona wala kusikia kuwa siasa zile zilishindwa kwa asilimia 200 kama sio mia

Binafsi naamini hakuna kosasa lolote kwa Sita kujadili na kuona wapi panamfaa kisiasa kama anaona alipo hapaja mridhisha, na akiona anakoombwa aende ni afadhali alipo then anauhuru huo pia kama alivyofanya
 
Last edited by a moderator:

Mzee wewe inaonekana una taaluma ya ualimu,unajitahidi kuwasaidia hawa vilaza wa chadema lakini bahati mbaya sana ni watu ambao hawako tayari kujifunza na kuelewa,hawa ni aina ya wanafunzi wanaoamini katika kukariri mambo ili tu wafaulu mtihani,hawako tayari kuelimika..kwa watu wa aina hii chadema ina safari ndefu sana..lakini umetimiza wajibu wako wa kutoa elimu kaka,thanx.

Slaa na genge lake wanachotakiwa kufanya ni kujibu hoja za sitta hususan hii ya vyanzo vya vitakazowezesha utekelezaji wa elimu na amtibabu bure kitu ambacho kama watu mnakumbu kumbu mzee sitta alianza kukihoji toka wakati wa uchaguzi kipindi slaa na genge lake walipokua wakitanga tanga kila kona ya tanzania kutafuta kura kwa ghilba hii,lakini mpaka leo slaa kashindwa kujibu ikiwemo ile ya kushusha bei ya mfuko wa cement kufikia shs ngapi sijui...hii ya kutuambia sijui flani hafai hata kugombea ukatibu kata iko very cheap unless ije kama kisherehesho cha kisiasa tu baada ya kuwa hoja za msingi za mzee six zimepata majibu.
 
Hakuna pahala alipomponda mbowe unless hujasikia wala kusoma alichosema,najua watz wengi hatuna kusema,kukusaidia tu ni kwamba kuhusu mbowe alichofanya mzee six ni kuelezea mchango wa mhe.mbowe katika tasnia ya burudani akiwa ni mdau mkubwa sana wa mambo ya burudani,na kwa mliochelewa kuja Dar es salaam mpaka baada ya kubebewa na mbeleko ya kuja kujiunga chuo kikuu ni kwamba mboe na mambo ya burudani za disco hawakukutana barabarani bali amekulia kwenye hayo mambo,sasa nivigumu kutaja cv ya mbowe bila ku mention uhusiano wake na mambo ya disco kwani ndio iliyomkuza kabla ya kuingia kwenye politics,huo ndio ukweli hata kama tunahisi haipendezi kwa mwenyekiti wetu kuonekana ni mtu wa disco,na wala si dhambi,kuna rais wa madagascar ANDRY RAJOLINA yeye alikua dj kabla lakini leo ndio rais wa madagascar kwa kuwa urais hausomewi.Hiyo haina haja watu wa chadema kujisikia unyonge kutokana na mwenyekiti wenu kuwa mtu wa disco.
@KIM mkuu wangu tafadhali.. usianze matusi wakati humjui Mbowe wala historia nya Club Bilcanas toka wakati wa Mbowe Club. Freeman hakuwahi kuwa DJ wala kuanzisha biashara hiyo bali aliikuta tayari imesimama. Freeman alikuja rithi tu mirathi hiyo baada ya baa yake kufariki kati ya mwaka 1984 au 85 hivyo kuendeleza kile alichokiacha baba yake.

Mbowe hakuwahi kuwa mwenyeji Dar watu wengi walikuja mfahamu baada ya kurudi kutoka Moshi baada ya kuhitimu masomi ya kifato cha sita pengine unamchanganya Freeman na Charles. Hata hivyo Mbowe alipomaliza masomo yake aliajiriwa Benki kuu na Hata hiyo Bilcanas ilikuja funguliwa mwaka 1989 au 90 na ikimilikiwa na Freeman (Owner) wakati Mbowe Club ipo toka mwaka 1980. Kwa hiyo bado kuna tofauti kubwa sana baina ya Freeman Mbowe na Andry Rajou (Rajoline) pamoja na hayo yote msifikirie ma DJ ama wanamuziki hawakusoma.

Mtu anaweza kumaliza University akawa DJ,VJ, Tv Anchor ama Commentator wa kipindi cha Muziki, reality show, Michezo ypte haya sii dhambi wala kutokuwa na uwezo. Hizi mila chafu za zama za kina Sitta kufikiria muziki ni Uhuni wakati inawapa watu ajira na uwekezaji na yeye akiwa teja ni unafiki mkubwa sana..Akome na Unafiki kapata malipo yanayostahili Unafiki..
 
Majibu yangu kwa utetezi wa Nane:
Safu nyembamba ya uongozi
Tunahitaji kuwaza namna ya kumpata ni Raisi na Makamu wake tu. Wengine wote yaani mawaziri wanatokana na wabunge ambao haujarishi wametoka chama gani. Raisi atawateua kwa utashi wake kwa mujibu wa katiba yetu ya sasa. Swali kwa Nane: Unamaanisha nchi hii haina watu wakutosha kuwania na kushinda viti vya ubunge Tz hii kama sio matusi kwa wa-Tz?
Viongozi wengine wote wanabaki kama walivyo sasa maana nafasi zao si za kisiasa. Wengine ni wataalamu ambao wamesomea utaalamu wao, CDM au CCM kutawala hakuwaondolei utumishi wao

Mengineyo yote:
Yote naona ni bla bla tu hamna la maana alilo onge lenye kufaa kujibiwa

Ushauri
Mtiriliko wa hotuba ya Slaa unaonyesha kuwa Nane huna msimamo na kwamba wewe ni bendera fuata upepo. Chadema kimeshanuka, usipokaa sawa na CCM kitakunukia zaidi awamu inayokuja 2015 isipokuwa ukienda kuwaomba msamaha wana CCM na kuahidi hutorudia tena. Hata hivyo hata wakikusamehe sidhani kama watarudia kukupa madaraka makubwa kama uliyopata kupewa.
 
JK jembe bwana, huwezi kulinganisha na hawa waropokaji

Ni upepo tuu utapita.....siasa zina waropokaji, ila wengine wanaropoka maneno yoyote,wengine wanaropoka maneno yanayotoka katika set ya maneno sahihi.

Ndio maana kila mtu kuna muda anaropoka kama ana hasira au msisimko wowote.Ila kuna wanaotukana na kukufuru n akuna wanaoongea maneno ya kuonya na kuelekeza ila kwa sauti yenye hisia fulani.
 
Siasa za mkizi raha sana.Mpaka hapa 6 akisimama CDM wanaweza mnyamazisha kwa kauli fupi kwa mfano huu:-

-Huyu tunamjua kwa umbea.

-Umbea umeshakuwa ugonjwa sugu wa huyu mzee.

-Hembu akarekebishe hutuba yake na kutoa sehemu zenye umbea halafu aje.

-Sasa hivi anaongea akiwa chama gani tena?

-zote hizi ni jitihada za kutuonesha kuwa anastahili tumfikirie tena?Pole mzee umeshachezea bahati.

-Hongera mzee .Bado una ndoto za siasa?

+............
 
@KIM mkuu wangu tafadhali.. usianze matusi wakati humjui Mbowe wala historia nya Club Bilcanas toka wakati wa Mbowe Club. Freeman hakuwahi kuwa DJ wala kuanzisha biashara hiyo bali aliikuta tayari imesimama. Freeman alikuja rithi tu mirathi hiyo baada ya baa yake kufariki kati ya mwaka 1984 au 85 hivyo kuendeleza kile alichokiacha baba yake.

Mbowe hakuwahi kuwa mwenyeji Dar watu wengi walikuja mfahamu baada ya kurudi kutoka Moshi baada ya kuhitimu masomi ya kifato cha sita pengine unamchanganya Freeman na Charles. Hata hivyo Mbowe alipomaliza masomo yake aliajiriwa Benki kuu na Hata hiyo Bilcanas ilikuja funguliwa mwaka 1989 au 90 na ikimilikiwa na Freeman (Owner) wakati Mbowe Club ipo toka mwaka 1980. Kwa hiyo bado kuna tofauti kubwa sana baina ya Freeman Mbowe na Andry Rajou (Rajoline) pamoja na hayo yote msifikirie ma DJ ama wanamuziki hawakusoma.

Mtu anaweza kumaliza University akawa DJ,VJ, Tv Anchor ama Commentator wa kipindi cha Muziki, reality show, Michezo ypte haya sii dhambi wala kutokuwa na uwezo. Hizi mila chafu za zama za kina Sitta kufikiria muziki ni Uhuni wakati inawapa watu ajira na uwekezaji na yeye akiwa teja ni unafiki mkubwa sana..Akome na Unafiki kapata malipo yanayostahili Unafiki..
\

Bwana mkandinga unachanganya mambo pengine kutokana na kuzidiwa na mapenzi kupita kiasi,unaweza kuonyesha kwa ku quote ni wapi mzee sitta amaeonyesha kudharau kazi ya u dj au ni wapi mimi ama mzee sitta tumesema kwa kuandika kwamba free aliwahi kuwa Dj?

mzee sitta kwa mfano alichosema mchango wa bwana mbowe kwenye mambo ya burudani hauwezi ukadharauliwa wakati unataja cv yake.

Na kuhusu elimu unaweza kunisaidia kujua kiwango cha elimu ya mbowe na mambo aliyosomea?
 
Back
Top Bottom