CLONEY
Senior Member
- Apr 3, 2012
- 104
- 29
Wana JF habari za leo mi noimekuwa nakereka na majibu yanayokuwa yanatolewa bungeni na mawaziri yaani kusoma tu utekelezaji wake ni mdogo sana ulikinganisha na wanavyosoma halafu ni kama uniform kwasababu majibu yaliyotolewa mwaka jana ulkiuliza leo yatasemwa yale yale kama wimbo halafu yako kisiasa sana kwani yanapendeza kuyasikiliza na yanatia moyo lakini kwenye utekelezaji jamani mpaka naona kichefu chefu mfano leo wamegusia tena kuboresha nyumba za askari wetu majibu yamekuwa ni hayo hayo kila inapoulizwa hivi kweli kama wangekuwa wanajibu na kutekeleza hivi kweli leo bado tungekuwa tunaambiwa serikali inafanya mpango wa kuboresha makazi ya askari wake hadi lini?hakuna mengine ya kujadili kuhusu askari hao?haya hao wazamani bado je hao wanaoajiriwa kila mwaka?na wimbo huo utaisha lini?
NB:gharama zinazotumika kutekeleza shughuli za bunge, majibu yanayoyotolewa ukilinganisha na utekelezaji wake yaani tutaendelea kwenda kwa mwendo wa kinyonga au kupiga li gwaride kila mwaka na watu wachahe wataendelea kuneemeka kwa kula mali za umma kama tunavyoshuhudia kwenye halmashauri zetu.