Majibu ya Jack Zoka yana utata!

Status
Not open for further replies.

Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,780
3,208
Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen la leo naibu mkurugenzi wa Usalama wa Taifa aliyetuhumiwa na CDM jana kuwa yeye anasimamia operesheni ya kuangamiza viongozi wake amejitokeza na kutoa majibu yafuatayo;

But in a quick rejoinder, Mr Zoka dismissed the allegations, saying that Chadema officials were just playing politics and he would ignore them since he was not a politician but a civil servant working for a State organ.
“Dragging my name into their claims is sheer nonsense…. all these people are doing is play politics by way of looking for easy punching bags. I’m doing my work as guided by principles and procedures,” Mr Zoka said



maswali ya kujiuliza;
1. Kanuni zinasema je kuhusiana na ni nani anapaswa kuongea na vyombo vya habari
2. Ametoa wapi mamlaka ya kutoa tamko kama kanuni hazimpi ruhusa
3.Kwanini kajitokeza haraka hivyo wakati Mkuchika ambaye ni waziri wake kasema kuwa jambo hilo ni kubwa na haliwezi kusemewa semewa ghafla.

Ninavyoona huyu jamaa anaharibu heshima ya Idara , na ndio maana CDM wanaweza kuipata mipango yake na kuiweka hadharani ,
 
Huyu Zoka ni mara ya pili anajitokeza na kujibu tuhuma za Chadema. Nakumbuka mara ya kwanza ilikuwa ni baada ya uchaguzi wa 2010.
 
Kwani hii nchi ya Usalama wa Taifa? kwanini hawa watu wanatuona wananchi ni wajinga kiasi hicho?
Huyu ZOKA ni nani yeye nchi hii zaidi upumbavu wa kidunia anaoufanya? KUNA SIKU NAYE atakuwa marehemu tu, MUNGU YUKO
 
Kimsingi hajakataa kuagizwa kufanya kazi hiyo, bali amesema anafanya kwa kufuata STK(Sheria, Taratibu na Kanuni!)

There you are PakaJimmy,
Kwakuwa hajakanusha kupokea maelekezo ya kufanya kazi maalum ya kuwa-limboka viongozi wa Chadema basi bado hiyo statement haitoshi kumkwamua katika tuhuma hizo.

Kwakuwa hata RO mkurugenzi mkuu wa TISS naye anafanya kazi ofisi hiyo hiyo ya state organ kama zoka anavyodai, kwanini asituhumiwe yeye ambaye ndiye boss badala yake naibu wake ndiye atuhumiwe? hapa inaonekana zoka ndiye kichaka cha uhalifu ndani ya TISS.
 
Last edited by a moderator:
Kwani hii nchi ya Usalama wa Taifa? kwanini hawa watu wanatuona wananchi ni wajinga kiasi hicho?
Huyu ZOKA ni nani yeye nchi hii zaidi upumbavu wa kidunia anaoufanya? KUNA SIKU NAYE atakuwa marehemu tu, MUNGU YUKO

bad language.... uko upande wa chadema na ndio maana unasilikiza na kuamini ya upande mmoja tu
 
Tuhuma zilizoelekezwa kwake ni ngumu mno ukizingatia unyeti wa chombo husika.zoka kusema kwa wepesi hivyo nukukiri kwamba hiyo mipango alikuwa anairatibu sasa amejkurupushwa na sasa ameshindwa kujibu
 
Jack Nzoka asifikiri ataendelea kutesa watu kwa style hiyo hiyo milele lakini ipo siku atakuja kujuta milele
 
Tuhuma zilizoelekezwa kwake ni ngumu mno ukizingatia unyeti wa chombo husika.zoka kusema kwa wepesi hivyo nukukiri kwamba hiyo mipango alikuwa anairatibu sasa amejkurupushwa na sasa ameshindwa kujibu
ni ngumu kama lingekua taifa makini...otherwise ni upepo tu
 
Yeye ni mtumishi waserikali katumwa kuua basi ataua, hiyo ndiyo maana yake kajibu vizuri sana.
 
Kama kweli anaijua kazi yake, atuambie ilikuwaje ndege ya kijeshi imetoka nchi nyingine ikaja ikabeba Twiga na kuondoka bila serikali kujua na inakuja kujua kupitia wabunge? Yeye kama mkuu wa Usalama wa Taifa alikuwa anajua au alikuwa hajui? Na kama alijua alichukua hatua gani kulizuia lisifanyike?

Anyamaze kimya ache mahoka.

Anachefua.
 
huyo cjui nzoka, kikwete na majambazi menginemengine humo serikalini, ni vapour mbele za MUNGU! Waache watambe duniani, maana mbinguni hakuna hata ajuaye kama wanaexist!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom