Majibu ya IKULU dhidi ya Tanzania Daima kuhusu ndege ya Rais na safari ya Davos

Achana na makosa ya kimaandishi, but ukweli uko pale pale kama siyo milioni 300 ni shillingi ngapi?
Hizo figure zilizotajwa kunufaisha nchi wametumia kigezo gani kuzipata?
 
Kuna pande kadhaa; Kwanza kukosea herufi sio jambo geni lakini katika taarifa iliyopo ni wazi hilo lingeepukika. Mwandishi alipaswa ajue Qatar ni ndege ya nchi gani na kujiuliza Rais anaenda kufanya connection wapi. Sitarajii habari hii ingeletwa bila mhariri kuipitia, sijui ilikuwaje hadi gazeti likachapwa na udhaifu huo wa wazi.

Pili, kukosea majina ya miji ni jambo la kawaida. Niliwahi kusoma gazeti la kiingereza la marekani likiandika New York kama New Yark.
Hata sisi Wtanzania mji wa Musoma wengine wanaandika au kusema Msoma

Kilichomsukuma mkurugenzi wa mawasiliano ni habari ya 'uongo' na alitaka kuweka rekodi sawa. Spelling hazifanyi hadithi ikawa ya uongo hasa inapokuwa wazi kama ilivyo. Ukisoma habari nzima hakukuwa na sababu ya kujibu spelling kwasababu hazijatoa jibu.
Sitegemei taarifa ya Ikulu isahihishe spelling na si kufafanua au kukanusha. Too low! Hivi Mkurugenezi wa mawasiliano Ikulu hakumbuki Mama Kikwete kukabidhiwa hundi ya laki tatu ikiwa imeandikwa 300,00! Hiyo ilifanya hundi na shughuli nzima kuwa ya uongo.

Kurugenzi haijakanusha Rais kusafiri na ndege binafsi, wala matumizi ya milioni 300 kwa siku nne. Sisi tunabaki kuamini kuwa ni milioni 300 hadi hapo atakapokuja mtu wa Ikulu na kiasi kilichotumika. Kama milioni 300 ni uongo ,ukweli ni milioni ngapi?

Kurugenzi inakubali kuwa ndege ilikuwa katika matengenezo, inachokataa ni serikali kuwa na ukata. Labda atuthinitishie zimelipwa pesa za matengenezo ?na ni kiasi gani, vinginevyo tutaamini ya Tanzania daima.

Hivi kuwaambia Watanzania safari ya Rais wao ni uchonganishi? Kama ni uchonganishi, hivi unazidi ule wa Rais kusema haifahamu Richmond halafu Richmond imtambue kuwa anaijua.

Siwezi kuwatetea waandishi na kutaka kufanya makosa yao yaonekane madogo, walichokosea ni zaidi ya spelling, wamebadilisha nchi aliyokwenda rais kabisa. Kama hawa waandishi wanapata tabu kuandika "Qatar" "Davos" na "Switzerland" napata mashaka kama wataweza uchambuzi na kuandika figures vizuri.

Lakini pia inawezekana Tanzania ya leo ili upate jibu kutoka ikulu inabidi uwape some "low hanging fruits" za kuficha aibu yao, na watu wakaona wafanye makosa strategically makusudi ili "kumtoa nyoka pangoni" kama alivyosema mkuu mmoja hapo juu. I doubt that highly though. It is more likely that this is the usual garden variety mediocrity flaunted by our recent "shule za kata" graduates.

Lakini ukweli mkubwa utabakia hawahawa graduates wa shule za kata wasiojua tofauti kati ya Qatar na Qatal, Davos na Davous, Switzerland na Sweden, wametoa figure ambayo Ikulu imeshindwa kuikanusha, hata kwa kutumia b.s boilerplate ya "matumizi ya Ikulu ni suala la usalama wa taifa" or some other phoney baloney like that.

Kwa hiyo mpaka sasa, ingawa team shule ya kata inaboronga and all, imefanikiwa kumtoa nyoka pangoni na bado haijajibiwa kikamilifu, dyslexia on geographic placenames aside.
 
Kwa mujibu wa taarifa hiyo "sahihi" ya Ikulu, Kikwete anatarajia kuwasili Addis Ababa Jumamosi, Januari 28, 2021 - mmeiona hiyo?

Halafu pili, wakati Salva anasahihisha makosa ya uandishi ya gazeti, yeye anaandika kuwa waziri mkuu wa zamani wa Australia ni Kevin Ruud, wakati jamaa anaitwa Kevin Rudd.

Nchi inatisha kwa kweli.


not only that mkuu bwana salva rweyemamu amemtaja waziri mkuu wa zamani wa Australia kwa jina la Kevin Ruud while his real name is Kevin Rudd
 
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais pamoja na Salva Rweyemamu hawana hata aibu kutaka kukosoa watu Kiingereza.

Ona walivyoandika hapa 30 December 2011

Urgent Press Notice


Shortly, there are will be a very important statement from the State House. Please be on the alert for the satement and briefly delay sending your publications to bed.

Sent by Salva Rweyemamu – Director of Presidential Communications – State House – December 30, 2011.

Tulishamchoma hapa

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/207742-balozi-ombeni-sefue-amrithi-luhanjo.html

Halafu kuna ule uzi mwingine wa barua zake na Rostam, ni aibu tupu! Then JK kampeleka Ikulu!

If you live in a glass house, don't throw stones.
 
Yafuatayo ni majibu ambayo IKULU imeyatoa dhidi ya gazeti la Tanzania Daima kuhusu utata wa ndege ya Rais 5H-One ambayo iko katika matengenezo nchini Marekani. Nimeona niwaletee habari hii kwa urefu wake ili msoma na kutafakari.

TAARIFAKWA VYOMBO VYA HABARI
Gazeti laTanzania Daima la leo, Jumatano, Januari 25, 2012, kwenye ukurasa wake wakwanza limechapisha habari yenye kichwa cha habari, “Ndege ya JK utata:Iko nje kwa miezi miwili. Serikali yakwama kuilipia.”

Miongoni mwayaliyoandikwa kwenye habari hiyo ni pamoja na “Ukataunaiokabili Serikali umesababisha kukwama kuilipia ndege hiyo maalum yaRais…Ndege ya Rais mahususi kwa ajili ya safari za namna hiyo imezuiliwa njebaada ya Serikali kukwama kulipia gharama za matengenezo yake…Kutokuwepo kwandege hiyo, kumesababisha Rais Kikwete na ujumbe wake wa watu 14, ulioondokanchini jana kwenda Davous, nchini Sweden kuhudhuriamkutano wa dunia wa uchumi, kuondoka na ndege ya Shirika la Ndege la Qatal”.

LimeendeleaGazeti hili la Tanzania Daima kudai kuwa kwa sababu ya kutokuwepo kwa ndegehiyo ya Rais gharama za safari hiyo ya Rais zimeongezeka na ziara hiyo ya Raisya siku nne kuhudhuria mkutano huo itagharimu kiasi cha shilingi milioni 300.Aidha,Gazeti hili linadai kuwa mkutano huo hauna tija kwa taifa, kwamba Rais Kikweteamehudhuria mikutano hiyo mara nyingi lakini hakuna faida iliyopatikana kwataifa.

Kwa hakika,maandishi na kauli hizi za ovyo na zisizokuwa za kweli za Gazeti la TanzaniaDaima zinalenga kuupotosha umma wa Tanzania bila sababu za msingi na hivyokuusababishia umma chuki isiyokuwa na msingi kwa Rais. Katika kuuelezea ummaukweli wa safari hiyo ya Mheshimiwa Rais Kikwete tunapenda kutoka ufafanuziufuatao:

Kwanza, kama tulivyoeleza, kwa usahihi, katika taarifa yetu kwa vyombo vya habari janajioni, Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekwenda katika mji/kijiji chaDavos, nchini Uswisi kuhudhuria Mkutano wa World Economic Forum (WEF) unaoanzaleo. Rais Kikwete hakuwenda katika mji wa
Davous, nchini Sweden kamalinavyosema Gazeti hili. Aidha, Rais Kikwete na ujumbe wake umesafiri kwa ndegeya Shirika la Ndege la Qatar na siyo Qatal kama linavyoripoti Tanzania Daima.

Pili,Serikali haijakwama, kwa sababu zozote zile, kulipia matengenezo ya kawaida (routinemaintenance) ya Ndege ya Rais. Hili limefafanuliwa vizuri na ipasavyo naMtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali, Rubani Kennan Paul Mhaiki jana.Isipokuwa nivyema kuongeza kuwa matengenezo ya ndege hiyo yalimalizika juzi tu, Jumatatu,Januari 23, mwaka huu, wakati ndege hiyo ilipofanyiwa safari ya majaribio (testflight) kule Savannah, Georgia, Marekani na wala siyo miezi miwili iliyopitakama linavyodai Tanzania Daima. Hivyo, madai kuwa ndege hiyo imezuiliwa nje kwamiezi miwili sasa kwa sababu ya Serikali kushindwa kulipia gharama zamatengenezo ni porojo tu zisizokuwa na msingi.

Tatu, nivigumu kujua Gazeti la Tanzania Daima limepata wapi habari kuwa safari hiyo yasiku nne inagharimu kiasi cha sh. milioni 300. Ukweli ni safari ya MheshimiwaRais Kikwete na ujumbe wake ni ya siku nane, kama tulivyoeleza jana, ambakoatahudhuria mikutano ya WEF na ule wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Afrika (AU)mjini Addis Ababa, Ethiopia atakapowasili Jumamosi, Januari 28, 2021.

Hivyo, sikweli kwa Gazeti hili kudai kuwa nauli tu na matumizi ya safari ya MheshimiwaRais ni shilingi milioni 300 kwa siku nne tu.
Nne, TanzaniaDaima linadai kuwa safari za Mheshimiwa Rais mjini Davos hazina tija na walafaida yoyote. Huu pia ni uongo mwingine wa dhahiri wa Gazeti hili.

Tunapendakukumbusha faida chache tu zilizotokana moja kwa moja na Mheshimiwa RaisKikwete kushiriki mikutano ya WEF kama ifuatavyo:
(a)Moja, ni kubuniwa na kupitishwa kwa Mpango Kabambe wa Uendelezaji Kilimokatika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania wa Southern Agricultural Growth Corridorof Tanzania (SAGCOT) uliozinduliwa wakati wa WEF mwaka jana.

Mpango huuutakaotekelezwa kwa pamoja na sekta binafsi na sekta za umma kwa kushirikishaSerikali ya Tanzania, Mashirika ya Kimataifa, Makampuni ya Kimataifa unalengakuleta faida zifuatazo:
(i) Uwekezaji wa kiasi cha dola za Marekanibilioni 3.4 katika kilimo cha Tanzania na kuongeza uzalishaji wa kilimo hichomara tatu katika miaka 20 ijayo.
(ii)Kuchochea uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na biashara kwenye eneoya hekta 350,000.
(iii)Kutengeneza kiasi cha ajira 420,000 za kudumu.
(iv)Kuwatoa kwa namna ya kudumu kiasi cha watu milioni mbili katikaumasikini.
(v)Kuleta usalama wa kudumu wa chakula kwa kuhakikisha kinapatikana chakulacha kutosha kwa Tanzania na nchi za jirani.
(vi)Kuboresha miundombinu ya umwagiliaji, barabara, reli, nishati na bandarikatika eneo lote la Mradi wa SAGCOT.(vii) Kuwahakikishia wakulima masoko ya mazao yao,kuwawezesha kupata dhana za kisasa, na kuwaanzishia mifumo ya kisasa yaumwagiliaji.
(viii)Kuingizia wakulima mapato ya kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.2 kilamwaka. (Kiasi cha dola za Marekani milioni 50 zinaendeleakuingizwa katika mfuko wa uanzishwaji wa Mpango wa SAGCOT utakaotelekezwa kwakuanzia katika maeneo ya Sumbawanga (Rukwa), Ihemi na Ludewa (Iringa),Kilombero (Morogoro), Mbarali (Mbeya), na Rufiji (Pwani)(b)

Pili, ni uwekezaji kabambe wa kiasi cha dolaza Marekani milioni 20 katika mfumo wa upakuaji wa mbolea kwenye Bandari ya Dares Salaam unaofanywa na Kampuni ya Yara International, moja ya makampunimakubwa zaida ya uzalishaji wa Kampuni ya Yara International, moja yamakampuni makubwa zaida ya uzalishaji wa mbolea duniani.
Yara International ni mmoja wa washirika wakubwakatika SAGCOT na uwekezaji wake unalenga kuhakikisha kuwa Tanzania na hatamajirani wanapata mbolea ya kutosha kwa ajili ya kuimarisha kilimo.

(c)Tatu, mikutano ya WEF ni shughuli moja inayomwezesha Kiongozi wa Nchikukutana na kufanya mazungumzo na wakubwa wote duniani – wawe wa siasa, wabiashara, wa uchumi, wa uwekezaji, wa kijamii – katika jitihada zake zakuitangaza Tanzania kama kituo muhimu cha uwekezaji.

Katika sikutatu zijazo, kwa mfano, Mheshimiwa Kikwete miongoni mwa watu wengine atakutanana Bwana Bill Gates wa Bill&Bellinda Foundation, Naibu Waziri wa Uchumi,Nishati na Kilimo wa Marekani Bwana Robert Hormats, Rais wa Benki ya DuniaBwana Bob Zoellick, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Australia Bwana Kevin Ruud, Mkuuwa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani Bwana Raj Shah, MtendajiMkuu wa Benki ya ABSA Bi. Maria Ramos, na Waziri Mkuu wa Thailand Bi. YingluckShinawatra.

Tunapendakumalizia kwa kusisitiza, kwa mara nyingine tena, kuwa ni vyema Gazeti laTanzania Daima lijiridhishe na usahihi na habari zake kabla ya kuzichapishakama inavyoelekeza misingi mikuu ya uandishi wa habari na weledi wa kazi hiyo.Uandishi wa habari za uongo unaleta hofu na kuanzisha uzushi usiokuwa na sababuzozote miongoni mwa wananchi na hiyo siyo kazi ya uandishi wa habari.

Imetolewa na:Kurugenzi ya Mawasilianoya Rais,
Ikulu, DAR ES SALAAM.
25 Januari, 2012

sijaona majibu ya matumizi ya sh 300milioni kumbe ni kweli.
Harafu hiyo ruzuku ya mbolea inachekesha mbolea ya kupandia inafika wakati watu wako kwenye parizi sasa nikilimo gani hicho
ushauri baada ya kupeleka bakuri hizo garama tungekuwa tunanunua mbolea wenyewe
 
La mwisho: mwenye kuweza kuitafuta humu JF post moja ya Mzee Mwanakijiji aliyoandika na kutoa barua moja ndefu ya Salva kwenda kwa Rostam kumuomba amuombee kazi kwa JK. Salva aliandika barua hiyo kwa Kiingereza kibovu wakati akiwa anasota bila kazi, isipokuwa ile aliyopewa na RA kupigia debe mitambo ya Richmond. Mwenye kuweza kuipata barua hiyo aiweke hapa tumsute aache kukosoa lugha zinazoandikwa na wengine.

Unaongelea hili bandiko
 
Njia bora kwa Tanzania Daima ni kurudia hiyo habari kama ilivyo except jina mji, nchi alokwenda na ndege alopanda JK.

How about that.???
Tatizo sio kurudia, tatizo ni kuwa "THEY ARE CARELESS" Hawafai kuwa waandishi wa habari huku wakifikiria kila Mtanzania ni mbumbumbu. Yaani kampuni Nzima hakuna aliye juwa kuwa Davos ipo Swiss? That is pathetic.
 
Siwezi kuwatetea waandishi na kutaka kufanya makosa yao yaonekane madogo, walichokosea ni zaidi ya spelling, wamebadilisha nchi aliyokwenda rais kabisa. Kama hawa waandishi wanapata tabu kuandika "Qatar" "Davos" na "Switzerland" napata mashaka kama wataweza uchambuzi na kuandika figures vizuri.

Lakini pia inawezekana Tanzania ya leo ili upate jibu kutoka ikulu inabidi uwape some "low hanging fruits" za kuficha aibu yao, na watu wakaona wafanye makosa strategically makusudi ili "kumtoa nyoka pangoni" kama alivyosema mkuu mmoja hapo juu. I doubt that highly though. It is more likely that this is the usual garden variety mediocrity flaunted by our recent "shule za kata" graduates.

Lakini ukweli mkubwa utabakia hawahawa graduates wa shule za kata wasiojua tofauti kati ya Qatar na Qatal, Davos na Davous, Switzerland na Sweden, wametoa figure ambayo Ikulu imeshindwa kuikanusha, hata kwa kutumia b.s boilerplate ya "matumizi ya Ikulu ni suala la usalama wa taifa" or some other phoney baloney like that.

Kwa hiyo mpaka sasa, ingawa team shule ya kata inaboronga and all, imefanikiwa kumtoa nyoka pangoni na bado haijajibiwa kikamilifu, dyslexia on geographic placenames aside.
Mkuu Kiranga, nakubaliana kabisa na wewe na ndiyo maana nasema kitu kama Qatar airline kwa mwandishi makini na mhariri ni mambo ya wazi.
Ninapokiona ni hoja ndogo ni pale kurugenzi mawasiliano inaposema kuwa taarifa ya Tanzania daima imelenga kumchonganisha rais na wananchi. Hapo nilitarajia majibu ya maana kuhusiana na taarifa. Inapotokea wanaacha kutueleza uchonganishi na wanakijikita katika herufi nabaki nikijiuliza hoja imejibiwa wapi na je herufi ndilo tatizo lililowasukuma kujibu hoja!!
Hata hivyo lawama bado zipo kwa mhariri kwasababu aliyeleta habari anaweza kuwa kanjanja.

Hata pale walipojaribu kutetea hoja ya ziara bado ni kitu kisichoingia akilini. Hawawezi kututajia mabilioni yanayotegemewa kupatikana wakati huo huo tukijua hawawezi hata kusafirisha umeme wa maji.

Hebu tujiulize, hivi ni kweli SAGCOT itatukomboa kama wanavyotuaminisha?
Nasema hivi kwasababu kulikuwa na Lower Moshi irrigation scheme, walipoondoka Wajapan imekufa.
Kulikuwa na mradi wa kutokomeza malaria Dar walipoondoka Wajapan umekufa.
Kulikuwa na mradi wa Mbarari walipoondoka ma-TX umekufa na sasa ni kilimo cha mibono.
Wameshindwa kuweka mabehewa juu ya reli na sasa tunatumia magari ya jeshi.
Wameshindwa kuendesha TRL, ATC lakini wana matumaini mkaubwa na SAGCOT.

Ukiangalia hoja za kuwachonganisha wananchi na utetezi wake, naona herufi bado ni suala dogo kujibiwa na Ikulu.
Hoja za milioni 300 ndiyo inatakiwa ijibiwe, na matokeo na umuhimu wa ziara na si hadithi za kufikirika kama kurugenzi inavyozileta.

Pamoja na yote japo Tanzania daima imewatoa mafichoni
 
....Mwacheni atabasamu huko , Cameroon na Bill gates wako huko pengine anaweza kurudi na hela tununulie dagaa ! ....[/SIZE]

Unataka kusema nini hapo kwenye Red? Si, unajua masharti ya huyo jamaa katika kutoa misaada? Unataka kusema JK kaenda kuyatimiza ili tupewe misaada?
 
Tumeshaambiwa na kurugenzi ya Ikulu kuwa wakulima watakuwa wanalipwa dola laki moja za Kimarekani kila mwaka kutokana na juhudi za vikao vya Davos. Kwa hiyo Watanzania tukae mkao wa kula.
 
Naona kaamua kuwakimbia madaktari! ha ha ha haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
SAGCOT itakuwaje ikiwa mjukuu wa Richmondi? Ni ile kampuni ya mpanda?

Kheee, unauliza hilo tena! Wewe hujui kwamba siku ukanda wa magharibi mwa Tanzania watakapopata mtu akawa waziri mkuu nao wataanzisha WAGCOT yaani Western Agricultural Growth Corridor of Tanzania! Manake Tanzania ndicho tulichabakiza & ndipo tulipofikia hv sasa! Haya hongera Mh. Mizenga Kayondo Patt.
 
Yangu mimacho tu maana sina la kuongea zaidi ya wachangiaji. Labda niseme kuwa tuombe mungu miaka iende haraka jk aondoke magogoni, na rais atakaekuja aondoe kizuizi kwa marais wastaafu kuchunguzwa tuhuma zao!
 
Hivi kazi ya waziri wa mambo ya nje ninini, kama JK anaenda mwenyewe kwenye mikutano inayomuhusu waziri wake?
 
habari yenyewe ni hii hapa chini

Ndege ya Rais yazuiliwa • IKO NJE KWENYE
MATENGENEZO, SERIKALI
YAKWAMA KUILIPIA

na Mwandishi wetu

UKATA unaoikabili serikali,
umesababisha kukwama
kuilipia ndege maalumu ya
Rais, inayofanyiwa
matengenezo nje ya nchi,
Tanzania Daima Jumatano limebaini.

Kutokuwepo kwa ndege hiyo,
kumesababisha Rais Jakaya
Kikwete na ujumbe wake wa
zaidi ya watu 14, ulioondoka
nchini jana kwenda Davous,
nchini Sweden, kuhudhuria mkutano wa dunia wa
mambo ya uchumi, kuondoka
na ndege ya Shirika la Ndege la
Qatal.

Habari ambazo gazeti hili
imezipata, zilisema kuwa
ndege ya Rais mahususi kwa
ajili ya safari za aina hiyo
imezuliwa nje ya nchi baada
ya serikali kukwama kulipia gharama za matengenezo
yake. Kutokuwepo kwa ndege hiyo
iliyonunuliwa kwa sh bilioni
40 na kuibua mzozo mkubwa
wakati serikali ya awamu ya
tatu chini ya Rais mstaafu,
Benjamin Mkapa, kunaelezwa kuwa kumeongeza gharama
kubwa kwa ziara za Rais
Kikwete ambaye amekuwa
akitumia ndege za kawaida
kwenye safari zake nje ya
nchi.

Habari kutoka ndani ya
msafara wa Rais, zilisema
kuwa zaidi ya sh milioni 300
zimetengwa kwa ajili ya
kugharimia ziara hiyo ya siku
nne nchini Sweeden. Habari ambazo Tanzania
Daima Jumatano imezipata,
zilisema kuwa kiasi hicho cha
fedha kinatumika ndani ya
siku nne kuanzia Januari 25
hadi 29 ambapo Rais na ujumbe wake watakuwa
wanahudhuria mkutano huo
ambao wataalamu wa
uchumi, wameuelezea
kwamba hauna tija kwa taifa.

Inaelezwa kuwa Rais Kikwete
ameshahudhuria mikutano
hiyo mara nyingi, lakini
hakuna faida inayopatikana
kitaifa baada ya serikali
kushiriki katika mikutano hiyo inayoratibiwa na Wizara ya
Fedha na Uchumi. “Jana

Rais Kikwete
ameondoka, yeye na msafara
wake watatumia zaidi ya sh
milioni 300 kwa siku nne tu,
atakazohudhuria mkutano wa
uchumi, Davos nchini Sweeden. Angekuwa na ndege
yake, gharama zingepungua,”
kilisema chanzo chetu cha
habari.

Vyanzo vyetu vya habari
vilisema kuwa kwa takriban
miezi miwili sasa, ndege hiyo
iko nje ya nchi ikifanyiwa
matengenezo kutokana na
kuwa na hitilafu. Hata hivyo Mkurugenzi
Mtendaji wa Wakala wa
Ndege za Serikali, Keenan
Mhaiki, alikiri kuwa ndege
hiyo iko nje kwa
matengenezo, lakini alisema ni matengenezo ya kawaida
yaliyomo ndani ya ratiba ya
ndege hiyo ya kisasa. “Ndege ya Rais iko kwenye
matengenezo. Sio kwamba ni
mbovu, hapana ni
matengenezo ya kawaida
ambayo yanachukua zaidi ya
mwezi mmoja,” alisema Mhaiki.

Alipoulizwa kwamba ndege
hiyo iko nje kwa muda mrefu
baada ya serikali kukwama
kulipa deni la matengezo yake,
Mhaiki alikana na kuongeza
kuwa hana taarifa za serikali kushindwa kulipia deni la
matengenezo. “Kwanza nikwambie tu kuwa
ndege hiyo sio mbovu, lakini
pia sisi hatuhusiki na malipo
ya matengenezo yake, kwa
kawaida ikishakuwa tayari
tunapewa taarifa nasi tunaandaa utaratibu wa
kuifuata,” alisema.

Alipoulizwa kuhusiana na
serikali kukwama kuikomboa
ndege ya Rais, Waziri wa
Uchukuzi, Omary Nundu,
alijibu kwa kifupi kwamba
hawezi kuulizwa swali hili kwenye simu. Alipotakiwa kufuatwa ofisini
ili kutoa ufafanuzi, Waziri
Nundu alikuja juu na kusema
yuko jimboni, hivyo waulizwe
wasaidizi wake walioko Dar
es Salaam. “Mimi niko jimboni, pale
ofisini kuna watendaji wa
wizara. Mimi siyo wizara,
nenda pale utapata majibu
yote,” alisema Waziri Ndundu.
 
issue ya TZ Daima ni matumizi ya ndege ya kibiashara ili hali ndege ya Rais ipo - ni mbovu ipo Marekani kwa mategenezo ( ikulu haijasema kama imesha lipia matengenezo )

pamoja na gharama ya sh 300mil kuelezwa kuwa ni gharama ya siku 4 lakini ikulu inashindwa kueleza gharama za siku 8 itakuwa siku ngapi

makosa ya kiuandishi ni ya kawaida sana ingelikuwa tatizo kama Tz Daima wangesema Rais amesafiri ilihali yupo

Sina imani kabisa na huu mradi ambao faida zake tuzitegemee baada ya miaka 20 ijayo

sijaona cha maana kwenye kanusho hili toka ikulu
 
Back
Top Bottom