Majibu ya Gavana Ndulu kuhusu Noti Mpya na ubora wake

NI hela ya nchi gani umeshawahi kuisugua ikatoa rangi? Hivi jamani tutumia common sense...! Inamaanisha kuchujuka ni security feature? Mbona dola ambayo imetumia technolojia hiyo haichujuki?

Hana naona kuna kitu kimefichwa...! We need to know more and ot investigate...! Majibu kama haya ya kirahisi rahisi naona sikubaliani nayo kabisa...!
 
MImi bado sijakubaliana na hii argument ya kuchuja rangi kabisa...! Mbona fedha za nchi nyingine hazichuji? Kwanini tuwe na hela chafu zinazochuja rangi? Kwanini tughramie kutengeneza kitu kibovu? Mbona nchi nyingine zenye walizotumia technolojia kama hiyo fedha zao hazichuji? Mimi naona kuna tatizo mahali kwa kweli...!

Haya majibu ya kirahisi rahisi hivi napata shida kukubaliana nayo kwasababu naamini huwa kunakua na uzembe au ubadhirifu ndani yake...!
 
Sijapata kusikia "upuuzi, utumbo, kinyesi cha ng'ombe" kama kusema kuwa noti kuchuja rangi ni sehemu ya usalama wa noti zenyewe. Hata mtoto mdogo huwezi kumdanganya. Itakuwa ni mara ya kwanza duniani kutumika njia hii ya usalama. Sisi watu wa kuchunwa tu.
yaani eti wanaotengeneza feki wanashindwaga sana kutengeneza feza zinazochuja!!!!
Hayo maelezo yametoka kwa profesa kweli?
Maprofesa wengine kweli mnakubali u-profesa uharibiwe hivyo?
 
Kweli tungependa kujua gharama za uchapishaji!!!!!

Nani aluambie???? We subiri mpaka uongozi ubadilike ndo uone wakina Kweka wengine sio sasa hivi.Watu wamesha tumia hela katika uchaguzi wanasubiri kukava mashimo kwa miradi kama hii
 
Kwa nini gavana ndulu anamjibia mchapishaji hizo hela, why not bring a guy kutoka kwa hao wachapishaji halafu iitishwe press conference? Noti hizo zimechapishwa Sweden hivyo basi huyo mchapishaji aeleze utofauti wa say Euro hata Swedish Kroner na noti zake. Very likely jibu litakuwa u pay peanuts u get monkeyz!
 
Kwa vichwa kama ch Beno basi noti za dola ni za ubora wa chini sana. Yaani uozo tangu utendaji mpaka kuutetea?!! Ndo kwa utendaji huu Gavana asitahili jumba lile? Ipo siku majibu yatatoka tu.
 
Hii ni kali ya mwaka!
Sasa ikiwa inatoka rangi mwishoni si itapauka??....na mwisho wa siku haitajulikana ni noti ya sh. ngapi!.....dah! Hii Tanganyika mbona kila siku kinaibuka kioja?
 
Back
Top Bottom