FortJeasus
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 603
- 397
Msisitizo katika redi hapo juu upo sahihi (correct) lakini hauko timilifu (incomplete).Kwenye the game of politics, hakuna permenent friend or enemies, kuna comon interests only!.
Kama ni kweli Sitta alijipanga kujoin Chadema na kuzungumza na uongozi wa Chadema in confidence, then this is uncalled for kwa Dr. Slaa to reveal this!. This is too low!''
Pasco.
Hauko timilifu kwa sababu hukuweza kuweka bayana hizo permanent interests zinalindwa na kuhifadhiwa kwa namna gani!
Tunaelewa kuwa katika siasa kuna kitu kinaitwa mikakati/mbinu za kisiasa(political strategies).Na kwa kutambua umuhimu wa mikakati, baadhi ya vyama huwa na wapanga mikakati wake(political strategists).
Kwa kawaida hawa huwa ni watu wenye ufahamu na ujuzi mpana katika maeneo ya siasa,saikolojia, uchumi ,elimu na mawasiliano.Ni wabobezi katika maeneo yao na wana akili zinazochemka..Hawa huweza kufanya kazi pasipo kujulikana kwa umma kwa kufanya kazi nyuma ya pazia(behind the scene).
Ni fani inayothaminiwa na inafanywa kisayansi na kimantiki na kwa kuzingatia ukweli pasipo kuweka uzandiki fitna,unafiki, majungu, uongo na upotoshaji uliopoozwa kwa kuitwa ''propaganda''..Mara tu weledi na umakini unapopuuzwa,mara moja, propaganda huchukua nafasi yake.
Sasa Spika Majeruhi amefanya propaganda zenye lengo la kupotosha.
Makamanda wameona ni vema kuweke ukweli hadharani ili wananchi wamwelewe mtoa ''hoja'' kwa kina.
Tunawezaa kuona kuwa lengo kuu(general objective) katika tamko hilo lilikuwa ni kuonyesha ya kuwa Majeruhi wetu hana uhalali wa kimaadili.Lengo mahususi(specific objective) lilikuwa kukanusha shutuma alizotoa hata kama zingekuwa zimetolewa na mtu mwenye uhalali wa kimaadili tofauti na yeye..Mara mtoa hoja anapokosa uhalali wa kimaadili asilalamike upande wa pili unapoachana na hoja zake na kuanza kumkabili mtoa hoja.Hii ni kawaida kabisa.
Katika siasa mbinu mbali mbali huweza kutumiwa..Hakuna mbinu ya aina moja..Mazingira ,kwa maana ya hoja na wakati tofauti, huhitaji mbinu tofauti.Naamini mbinu mwafaka imetumika.