Majibu ya Dr. Slaa kwa maswali ya watanzania, Julai 2011

Dr. Slaa,

Mimi nina ushauri kwa CHADEMA; anzisheni Redio na TV yenu ili muweze ku-counter attack propaganda za CCM zinazorushwa na vyombo mbali mbali vya habari. Zaidi ya yote, vyombo hivyo vitawawezesha kuwafikia wananchi wengi kwa muda mfupi.

Mkuu Nadhani Sheria za nchi haziruhusu vyama vya Siasa kumiliki Radio au Television unless CDM wangeshafungua tayari
 
mimi naomba ushauri. napokea posho chini kidogo tu ya milioni moja na wananikata kodi. je wananionea.

baada ya kujua kutolipa kodi ni makosa. mzee wa phd umeanza kulipa kodi.

ni hayo tu kwa leo mbaba
 
Dr. Slaa,

Mimi nina ushauri kwa CHADEMA; anzisheni Redio na TV yenu ili muweze ku-counter attack propaganda za CCM zinazorushwa na vyombo mbali mbali vya habari. Zaidi ya yote, vyombo hivyo vitawawezesha kuwafikia wananchi wengi kwa muda mfupi.

Akihojiwa na Mwanakijiji mwezi wa tano mwaka huu Dr Slaa alikiri kuwa kitengo chao cha habari na mawasiliano kinahitaji kuboreshwa. Alisema kitengo hakina nyenzo na akaomba radhi.

Lakini alisema wanajipanga kuwa na watu wenye ujuzi zaidi katika matumizi ya nyombo vya habari kama kamera na mitandao ili kurahisisha habari kuwafika mapema walengwa. Alisema kuna kitu wanafanya na watakuwa wa kwanza kabisa kukifanya Afrika lakini hakupenda kukitaja.

Alisema wameona dosari ya mawasiliano na kuwa maandalizi yako very advanced kwa sasa. Alisema kuanzia tarehe 15 July 2011, tunaona mabadiliko makubwa sana ndani ya Chadema kuhusiana na habari na mawasiliano.

Lakini leo ni mwisho wa mwezi July 2011. Sikiliza hii video clip kuanzia dakika ya nane.

Last edited by a moderator:
Dr. Slaa,
nashukuru kwamba upo pamoja nasi JF.

Naomba niulize swali tofauti kidogo. Leo nikiwa sehemu nimepumzika nimeshuhudia sehemu ya mwisho ya shoo ya original komedi (TBC). Nilistushwa kuona wakiuelimisha umma wa watanzania kuwa wabunge wa CHADEMA ni wavuta bangi (indirectly). Hawakutaja moja kwa moja lakini ujumbe ulilenga moja kwa moja wabunge wa CHADEMA kwamba huvuta bangi ili wakafanye fujo bungeni. Kweli moyo wangu umenyong'onyea hasa nikijiuliza ni ujembe gani unapelekwa kwa wananchi.

Si wote wenye uwezo wa kupuuza mambo kama baadhi wanavyodhani. Je, huoni ni muhimu udhalilishaji ni upotoshaji huu unapaswa kukemewa waziwazi?
 
Maswali mengi, Dk tunakusubiri, wengine tuko reserve bado......!! Tunaomba majibu kwa maswali ya msingi
 
.....lugha zingine ni kali sana,na hazipaswi kuelekezwa kwa kiongozi wa kitaifa kama Dr Slaa. hata kama unatekeleza majukumu yako zingatia uadilifu.

ndo sbb viongozi wa CCM hawawezi kujitokeza na kujibu kama Dr anavyofanya,anatuheshimu wanaJF nasi tumheshimu ili tuendelee kupata majibu ya masuala ya kitaifa.

Hata kama majibu hayatakuwa ya kiutendaji yanafariji sana na kutufanya tujue tuna watu makini ambao soon or later wataongoza nchi hii kwa uadilifu
 
Dr. Slaa,
nashukuru kwamba upo pamoja nasi JF. Naomba niulize swali tofauti kidogo. Leo nikiwa sehemu nimepumzika nimeshuhudia sehemu ya mwisho ya shoo ya original komedi (TBC). Nilistushwa kuona wakiuelimisha umma wa watanzania kuwa wabunge wa CHADEMA ni wavuta bangi (indirectly). Hawakutaja moja kwa moja lakini ujumbe ulilenga moja kwa moja wabunge wa CHADEMA kwamba huvuta bangi ili wakafanye fujo bungeni. Kweli moyo wangu umenyong'onyea hasa nikijiuliza ni ujembe gani unapelekwa kwa wananchi. Si wote wenye uwezo wa kupuuza mambo kama baadhi wanavyodhani. Je, huoni ni muhimu udhalilishaji ni upotoshaji huu unapaswa kukemewa waziwazi?

Zekomedy wamekosa mvuto kabisa kwa sasa!! Wapo so cheap nowdays.
 
Mwenye macho na aone na mwenye masikio na asikie, napita tu ntarudi tena nami kumtwanga swali dr.
 
Asante Dr. Slaa kwa majibu yanayoakisi maswali yaliyoulizwa. Nakuunga mkono kwa kutogombea jimbo la Igunga. Endelea kujenga chama.
 
mimi naomba ushauri. napokea posho chini kidogo tu ya milioni moja na wananikata kodi. je wananionea.

baada ya kujua kutolipa kodi ni makosa. mzee wa phd umeanza kulipa kodi.

ni hayo tu kwa leo mbaba
Duh kweli hapa moderation imefanya kazi. Maana maneno ambayo hayakuwa na umuhimu zaidi ya kuudhi yalikuwa yanaleta kinyaa.
 
Zumbemkuu,

Wana JF awali nawasalimu. Ni muda kidogo sijapost kwenye jamvi letu japo nimekuwa nikichungulia ama kama member ama kama guest. Nimeona ombi na nimeielewa.

Pamoja na kuwa sina tatizo kutoa mchango wangu kama mkereketwa wa maendeleo ya Taifa letu, na kuchukizwa sana giza totoro linaloikimba nchi yetu, ni maoni yangu kuwa hoja nyingi zilizoko zinahitaji majibu ya Serikali na Chama Tawala.

Kwa vile wako wa Chama tawala humu, ninashauri maswali hayo waelekezewe hao tuliowapa dhamana na wanakusanya kodi zetu. Niko tayari kuchangia pale yatakapohitajika maoni yangu kuhusu jambo lolote lile kama maoni hayo yanaweza kusaidia tusonge mbele. Swala la Madiwani wa Arusha nimekuwa nikilitolea ufafanuzi wa mara kwa mara kwenye vyombo vya habari.

Kama kuna mtu anahitaji ufafanuzi wowote, nitakuwa tayari kuutoak, alimradi ni ndani ya uwezo na mamlaka yangu kwa mujibu wa Katiba ya Chadema. Nawashukuru sana na ninawatakia mjadala mwema, nikitegemea wahusika wa chama tawala watajitokeza wazi pia.

Taifa ni letu sote na litajengwa na wale tu wenye nia njema na Taifa hili.

kisomi zaidi
 
Dr. Slaa,

Mimi nina ushauri kwa CHADEMA; anzisheni Redio na TV yenu ili muweze ku-counter attack propaganda za CCM zinazorushwa na vyombo mbali mbali vya habari. Zaidi ya yote, vyombo hivyo vitawawezesha kuwafikia wananchi wengi kwa muda mfupi.

Chama hakitakiwi kuanzisha Radio wala TV. Sio demokrasia na wala haijengi demokrasia ya kweli. Watanzania sio wajinga hizi propaganda zinaanzishiwa na vyombo vingine zinaeleweka. Bora chadema ipige propaganga bila kuwa na chombo cha habari . propaganda itakuwa na nguvu . Lakini wakisha miliki vyombo vya habari propaganda zao zitakosa nguvu.......

  • Chama cha siasa kinatakiwa kutumia uwezo wake na rasilimali kushawishi hivyo voymbo vya habari viandike habar zake vizuri. watumie mbinu zote wanazojua za halili na za ........ wanaweza kuwaweka "kwenye salary slip yao" wandishi wa makala eye magazati fulani . E bu fikiria kama mwandishi mmja wa daily news au uhuru au chanel Ten angekuwa kwenye salary slip ya CDM ........... teh teh teh
  • Wanachama na wakareketwa wa CDM ndio wanatakiwa kuanzisha vyombo vya habari wakibebe chama chao

CDM kuanzisha radio au gazeti au TV ni kujiongezea mzigo mkubwa tu wa kiundeshaji na hakuna tofauti kubwa na chanya itayopata
.

So msiwadangaye na kuwapotosha CDM waanzishe TV au radio yao waambieni wawe wabunifu wajue nji za kudeal na vyombo mbali mbali vilivyopo.
Nimetoa mfano
 
.....lugha zingine ni kali sana,na hazipaswi kuelekezwa kwa kiongozi wa kitaifa kama Dr Slaa. hata kama unatekeleza majukumu yako zingatia uadilifu.

ndo sbb viongozi wa CCM hawawezi kujitokeza na kujibu kama Dr anavyofanya,anatuheshimu wanaJF nasi tumheshimu ili tuendelee kupata majibu ya masuala ya kitaifa.

Hata kama majibu hayatakuwa ya kiutendaji yanafariji sana na kutufanya tujue tuna watu makini ambao soon or later wataongoza nchi hii kwa uadilifu
You said it all,shukran.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kuna mtu juzujuzi (FF) alitimiza miaka 30 ktk ndoa. Sijui kama ni kweli maana nina mashaka kwa jinsi ninavyomwona asivyojiheshimu anapokuwa kwenye mijadala mbali mbali hasa huu ambao Dk Slaa ameombwa na wanaJF. Nadhani ndio maana hata sikuweza kumpongeza maana najua sio mama anayejiheshimu. Na ni hivyo hivyo pia asivyoiheshimu ndoa yake.

Si majibu ya kumtukana mtu kama Dk Slaa kusema hajui Kiswahili. Swali: Kiswahili ni lugha ya kabila gani hapa Tanzania? Je, ni nani anayeijua kiswahili kilivyo? Sasa hili alilolileta huyu mama limetoka wapi?

Sasa naona Dk Slaa haendelei kutujibia maswali yetu sijui ni kwa sababu ya huyu au kitu kingine; sijui. Tafadhali Dk endnelea kutupa mwanga.

Asante.
 
.....lugha zingine ni kali sana,na hazipaswi kuelekezwa kwa kiongozi wa kitaifa kama Dr Slaa. hata kama unatekeleza majukumu yako zingatia uadilifu.

ndo sbb viongozi wa CCM hawawezi kujitokeza na kujibu kama Dr anavyofanya,anatuheshimu wanaJF nasi tumheshimu ili tuendelee kupata majibu ya masuala ya kitaifa.

Hata kama majibu hayatakuwa ya kiutendaji yanafariji sana na kutufanya tujue tuna watu makini ambao soon or later wataongoza nchi hii kwa uadilifu

Ahsante sana kwa maneno yako mazuri yaliyojaa hekima na busara tele.
 
Back
Top Bottom