Majibu ya Dr. Slaa kwa maswali ya watanzania, Julai 2011

swali limeulizwa na Albedo
Dr. Slaa

Nimekuwa ni mfatiliaji wa karibu wa Kikao cha Bunge kinachoendelea na namna Kinavyoendeshwa kwa Spika hasa Naibu Spika kuwa kandamiza sana Wapinzani na ( Hata jana kwenye Mdahalo ameonesha kwamba ana Chuki na CHADEMA). Hali hii Dr ikiachwa bila kukemea itapelekea Wabunge wa Upinzani kujiona ni Inferior ambacho naamini ndiyo hasa lengo la CCM ikiwatumia Spika na Naibu Spika.

Tumeona namna Naibu Spika anapovumila Uvunjifu wa kanuni hasa pale inapowahusu CCM na kuwa mkali pale inapowahusu Wapinzani.

Dr. Slaa wanannchi wanakerwa sana na hii Tabia ya Naibu spika ila wanakerwa zaidi na Ukimywa wa CDM katika kulikemea hili ikibidi kutumia Nguvu ya Uma kushinikiza Hatua zichukuliwe dhidi ya Viongozi hawa.

Nakumbuka Mheshiwa Shelukindo aliruhusiwa asome barua inayomhusu Jairo lakini Tundu Lisi alikatazwa na kuambia aandike Ushahidi

Nataka Kufahamu kama kama CDM kinayaona haya? na nini Msimamo wake/

Asante sana
 
Kwa vile watu wanapotosha habari ya kwamba nyie mnapenda fujo, na mnataka kuleta vita..... mna mikakati gani ya kuweza kuweka ukweli wazi, au mna mikakati gani ya kufanya majimbo mliyoyachukua yawe mfano kwa maendeleo ili hata wale wapenda tshirt za bure na wanaodhani upinzani ni vita waweze kuwaunga mkono 2015....?
 
Saint Ivuga,

Igunga kimsingi ni ya wana Igunga. Wao ndio wanaofahamu mwana Igunga mwenye kuijua vizuri Igunga, na mwenye Uchungu nayo. Si amini katika kugombea kwa lengo la kupata Ubunge.

Naamini Mbunge kuwa mwakilishi wa watu wake. Mimi nimerwawakilisha wananchi wa Karatu kwa miaka kumi na tano. Sasa nina jukumu la kujenga chama, ambacho nacho kikiwa imara kitawanufaisha wana Igunga. Ni mgawanyo wa majukumu. Ndicho tunachoamini ndani ya Chadema, nani anaweza kufanya vizuri nini na wapi na kwa wakati gani.

Ninawashauri na kuwashawishi sana Wana Igunga wenye sifa popote walipo wajitokeze ili tuweze kuijenga Igunga.

Mkuu Dr. W. Slaa, pole kwa majukumu.
Nimelipenda sana jibu lako. Kweli umejaa hekima.
Igunga ni ya wana Igunga, Bravooooo!!!!!
 
Dr W Slaa,
napenda kufahamu kama Mtanzania ili nivutike na sera za CDM, (1) Eti ni kweli wabunge wa CDM bado wanaendelea kuchukuwa posho bungeni? (2)
Na lile Shangingi la mkuu wa kambi ya upinzani bado nalo bado CDM wanalitumia?
(3) Kwa nini CDM hamfanyi maandamano Dar es Salaam!


RITZ
 
Dr. Slaa,
Tunakushukuru kwa muda wako hapa jamvini. Kumetokea ushabiki wa ajabu bungeni kwa siku za karibuni ambapo Spika na Naibu Spika pamoja na wenyeviti kwa makusudi wanapindisha kanuni za bunge na kupindisha mambo. Hata hivyo waheshimiwa wabunge wa bunge letu tukufu toka CDM wamekuwa makini na wamekuwa wakipakaziwa kuwa hawana hekima...wananchi tunayaona hayo na tumeamua kuwaadhibu na ushabiki wao wa kisiasa kwenye mambo ya msingi pale uchaguzi utakapoitishwa. Tunaomba mweekeo wa uchaguzi mdogo wa Igunga.
 
dr. Naomba nikuulize kidogo tu.
1. Kwanini mh. Shibuda huwa mnamtenga sana juu ya masuala ya chama?
2. Na kama hafuati misingi na sera za chama kwanini jina lake mlilipitisha kugombea ubunge maswa magharibi wakati mnajua matatizo yake ya huko alikokuwa na mpaka sasa hajabadilika na sidhani kama atafanya hivyo nini msimamo wa chama au tamko kuhusu wanachama na wapenzi wa cdm wenye tabia kama hiyo?
 
Dk.slaa unajiandaa vipi ktk kukabiliana na vitendo vya viongozi wa chama tawala bungeni kuwakandamiza wabunge wa chadema
 
Dr. Slaa tupe maoni yako kuhusiana na tamkola Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akiwa bungeni JUU ya NIA ya Serikali ya CCM kubadili sheria ya Maandamano. Naona wanataka kupiga marufuku maandamano. Kama tujuavyo CCM inaona raha watanzania wasipopata uhalisia wa mambo.
 
Dr. Slaa,

Shikamooni mzee wangu!

Swali: Chama chako kinaonekana kama kina mrengo wa military operations machoni mwa watu? Je, unalizungumzia je hili? Na je kuna strategy yoyote ya kikurudisha kuwa chama cha kupambana kwa nguvu za hoja na wala sio hoja za nguvu... mfano maandamano ni moja ya hoja za nguvu.

Kwa Mtumishi wa Mungu!
 
Asante sana Dr Slaa, majibu yako mazuri, swali langu la pili ni hili
1.Je ni kweli chama hakitaki kugharamia kesi za wagombea walioshindwa kwenye uchaguzi kwenye matokeo yenye utata?.
 
Wakuu,

Mkiangalia kwa makini anayeharibu threads sio Faiza Foxy. Wanaoharibu threads ni wachangiaji wengine pale wanapoacha thread na kuanza kuanza kujibizana na Faiza Foxy. Kama unaona ameandika pumba, then kwa nini unajibu pumba zake? As a great thinker, kwa nini usi ignore tuu pumba zake na kuendelea na thread? Na kama Faiza Foxy yuko hapa kuharibu thread, then she knows how to do it. Anaweza akaandika ovyo tuu ku divert attention. Na wachangiaji bila hata kufikiria wanaingia mkenge. Faiza Foxy hawezi kumkandia Dr Slaa kwa kuandika "Nimeona ombi na nimeielewa" halafu yeye mwenyewe aandike "wanakusanya kodi zanu".

Kwa Dr Slaa,

Mwisho naomba kumwuliza Dr Slaa juu ya msimamo wa Chadema kuhusiana na Suala la mgawanyo wa madaraka kati ya serikali na bunge. Kama alivyosema Mzee Warioba hivi karibuni, kuna mgongano ambapo wakati mwingine bunge limeonekana kufanya kazi za serikali. Wabunge wameanza kufanya hata kazi za kidiplomasia. Kwa mfano kuna wabunge walienda London ku negotiate change ya radar wakati waziri mhusika na balozi yupo. Pia wapo wabunge walioenda Malaysia kutembelea ile kampuni iliyopewa mkataba wa kutengeneza vitambulisho. Haya yote yalifanywa wakati vikao vya bajeti vinaendelea Dodoma.

Ukiangalia ile video ya kamati ya bunge la Uingereza likiwahoji maafisa wa BAE System kuhusiana na suala la change ya radar umwona mbunge wetu mmoja nae alikuwepo kwenye room. Alikuwa anafanya nini pale wakati alitakiwa kuwa bungeni Dodoma ku-scrutinise bajeti za wizara mbalimbali? Chadema haioni kama kuna tatizo hapa la wabunge wetu kufanya shughuli za kidiplomasia, n.k? Mzee Warioba ameghusia pia suala la Kamati za Bunge kutoa maelekezo kwa taasisi za serikali. Najua Tanzania tuna tatizo kubwa kwenye Separation of Powers kati ya bunge na serikali, lakini hili la wabunge kufikia kuwa wanadiplomasia, Chadema hamuoni kama tunavuka mipaka?

Asante.
 
Dr. Slaa, mimi nimefurahi kwa majibu yako yenye busara kubwa. Ila naona kutokana na kazi kubwa unayoifanya sasa inatakiwa upewe ulinzi binafsi na nyumbani lakini sio ulinzi wa polisi maana mimi binafsi siwaamini nafikiri JWTZ ndio inafaa zaidi. Nakutakia kazi njema.
 
Kwa vile watu wanapotosha habari ya kwamba nyie mnapenda fujo, na mnataka kuleta vita..... mna mikakati gani ya kuweza kuweka ukweli wazi, au mna mikakati gani ya kufanya majimbo mliyoyachukua yawe mfano kwa maendeleo ili hata wale wapenda tshirt za bure na wanaodhani upinzani ni vita waweze kuwaunga mkono 2015....?
Sio watu sema CCM wanapotosha, lakini naona watanzania wamewazoea kuwa CCM kazi yao ni kupotosha, wizi, ukandamizaji, udaku, kejeli, matusi, majungu, ulafi kila aina ya uchafu.
 
Tunashukuru sana Dr. Slaa maana umejibu majibu yaliyojitosheleza wenye jukumu la kujibu ni chama tawala wal sio wewe
 
Thanks Dr. Slaa; ukichukua Dola husinisahau, hasa katika kazi maalum ya kuichimbia kaburi na kuizika CCM imfuate Yahya Hussein huko aliko, Mungu ni Mwema na Mwingi wa Rehema akujazie rehema zake tele, akupe afya njema na Maisha marefu ili uendele kuitumikia nchni yako maana wenye moyo huo wanahesabika na wanye ujasiri huo hakika nakuona upo mstari mbele kabisa.

Nchni tutaichukua tu! maana kazi ya shetani ilikwisha kushindwa siku nyingi na huyo waliyemtegemea kuuwa wagombea wanaoipinga CCM, Mungu alikwisha kumwita ili apate adhabu yake ya kujifanya Mungu mtu hapo Magomeni tunaishi kwa neema ya mungu sasa.
 
Kasheshe said:
Dr. Slaa,

Shikamooni mzee wangu!

Swali: Chama chako kinaonekana kama kina mrengo wa military operations machoni mwa watu? Je, unalizungumzia je hili? Na je kuna strategy yoyote ya kikurudisha kuwa chama cha kupambana kwa nguvu za hoja na wala sio hoja za nguvu... mfano maandamano ni moja ya hoja za nguvu.

Kwa Mtumishi wa Mungu!

Kasheshe,

..hizo ni propaganda za CCM tu.

...lakini mbona Nape,Sitta,Mwakyembe,na Kilango, wameandamana kule Mbeya na kwingineko?

..mbona wao hawaulizwi kama wanafanya military operations?

..hivi mmeona wapi operation za kijeshi zikafanyika mchana peupe?

NB:

..nawashauri CDM watembee na vitambaa vyeupe kwenye maandamano yao ili kuondoa dhana yoyote ile ya uvunjifu wa amani.

 
Dr Slaa,
Shalom!

Ninapenda kujua CHADEMA ina mpango gani wa kuendeleza Kurugenzi/Idara ya Habari na mawasiliano? Ni lini watendaji katika Kurugenzi/Idara hiyo wataanza kutekeleza majukumu yao ya upashaji habari na kujibu upotoshaji unaofanywa kwa makusudi na CCM, Vyama vingine na Vyombo vya Serikali kuhusu CHADEMA?
 
2) Ni kweli mazungumzo husika yalijulikana kwa ngazi ya Taifa. Mara ya kwanza Makao Makuu yalifahamu document ya mwafaka ya 15/4/2011, kwa kuona document tarehe 29/4/2011 katika Mkutano baina ya viongozi wa Madiwani akiwemo Mwenyekiti wao Mhe. Mallah na Mnadhimu Mkuu wa Kamati ya Madiwani Mhe. John Bayo. Kikao kilifanyika New Safari Hotel, Arusha chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu.
3) Kwa kutambua kuwa CCM wapo tayari kwa mazungumzo, Mhe. Katibu Mkuu atayapeleka mapendekezo ya muafaka huu kwa wanasheria wa chama ili kuyafanyia marekebisho na mapendekezo hayo yatakuwa ni sehemu ya mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa Chama Mhe. Freeman Mbowe (MB, KUB na Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda.

Kwa bahati mbaya, tarehe 20/6/2011 Madiwani waliridhia mwafaka wao kama ulivyokuwa kwenye Hati yao ya tarehe 15/4/2011, na kuendelea na uchaguzi, bila kujali mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya Mhe. Mbowe na Waziri Mkuu.
Kwanini mliamua kukaa chini na CCM kuongelea suala hili la madiwani?,badala ya kutumia nguvu ya umma kama kamati kuu ilivyoamua kwenye kikao chake cha march?
 
Dr. Slaa,

Mimi nina ushauri kwa CHADEMA; anzisheni Redio na TV yenu ili muweze ku-counter attack propaganda za CCM zinazorushwa na vyombo mbali mbali vya habari. Zaidi ya yote, vyombo hivyo vitawawezesha kuwafikia wananchi wengi kwa muda mfupi.
 
Nguruvi3,

Ahsante kwa maswali yako. Naomba niyajibu kwa pamoja ifuatavyo:-

1) Msingi wa mgogoro wa Madiwani Arusha ni Uvunjifu wa Kanuni, Taratibu na Sheria zinazoongoza uchaguzi wa U meya katika Manispa ya Arusha. Kamati ya Marando imebaini kuwa "mchakato na utaratibu mzima wa uchaguzi wa Naibu Meya haikuzingatia Kanuni na Taratibu za Chama na Halmashauri" (Marando Kif.4.2). Hivyo, kama Chadema ilipinga ukiukwaji katika uchaguzi wa Meya, haiwezi kamwe kuidhinisha ukiukwaji ambao kwa bahati mbaya ni maradufu zaidi katika uchaguzi wa Naibu Meya.

2) Ni kweli mazungumzo husika yalijulikana kwa ngazi ya Taifa. Mara ya kwanza Makao Makuu yalifahamu document ya mwafaka ya 15/4/2011, kwa kuona document tarehe 29/4/2011 katika Mkutano baina ya viongozi wa Madiwani akiwemo Mwenyekiti wao Mhe. Mallah na Mnadhimu Mkuu wa Kamati ya Madiwani Mhe. John Bayo. Kikao kilifanyika New Safari Hotel, Arusha chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu. Miniti za Kikao hicho zinaonyesha mambo 5 ambayo Katibu Mkuu alibainisha kama msingi wa mazungumzo yeyote kama yatakuwepo. Nayo ni:-

i)Serikali ikiri kosa kuwa kanuni na mwongozo wa uchaguzi wa Meya Arusha mjini zilikiukwa.
ii)Uchaguzi wa Umeya urudiwe kwa vile haukufuata kanuni na Taratibu.
iii)Serikali itoe pole kwa wahangaa tukio la tarehe 5 Januari 2011
iv) Serikali ipitie madai ya msingi ya Chadema ikiwa ni ni kuwawajibisha Mkurugenzi wa Manispaa (kwa sababu ndiye alivunja kanuni) na OCD wa Arusha mjini
v) Kesi ya ya Viongozi wa chama na baadhi ya wananchi haina msingi hivyo ifutwe.

Kisha kikao kilijadili document ya 15/4 na kuona ina mapungufu makubwa. Iliazimiwa ifuatavyo:-
1) Miniti hii ina hila na ni ya unafiki na hivyo isitumike katika kufikia muafaka wa suala la Umeya hapa Arusha mjini.
2) Mwenyekiti wa Madiwani Estomih Mallah na Mnadhimu wa Madiwani Mhe. John Bayo wawajulishe madiwani na Mkuu wa Wilaya kuwa muafaka huu kwa mujibu wa chama una mapungufu ambayo chama hakitaweza kuyaafiki na hivyo usitumike kwa kufikia muafaka wowote.
3) Kwa kutambua kuwa CCM wapo tayari kwa mazungumzo, Mhe. Katibu Mkuu atayapeleka mapendekezo ya muafaka huu kwa wanasheria wa chama ili kuyafanyia marekebisho na mapendekezo hayo yatakuwa ni sehemu ya mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa Chama Mhe. Freeman Mbowe (MB, KUB na Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda.

Kwa bahati mbaya, tarehe 20/6/2011 Madiwani waliridhia mwafaka wao kama ulivyokuwa kwenye Hati yao ya tarehe 15/4/2011, na kuendelea na uchaguzi, bila kujali mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya Mhe. Mbowe na Waziri Mkuu. Isitoshe utaratibu wa kisheria wa uchaguzi wa Naibu Meya nayo ilikiukwa (kwa mujibu wa Taarifa ya Marando kukiwa na kugushiwa kwa saini ya Katibu wa Wilaya wakati pia hakuna kikao chochote cha Kamati Tendaji kilichojadili na kuteua mgombea wa Chadema). Hiki ndicho kilichofikisha Kamati Kuu kuelekeza Madiwani waliochaguana kinyume na Kanuni wajiuzulu ndani ya siku 3.

Baada ya hapo Madiwani 6 wakiongozwa na Mallah walikata rufaa, kwa bahati mbaya kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama rufaa zao hazikukidhi mahitaji ya Kikatiba na Kanuni. Maswala yote hayo sasa yanarudi mikononi mwa Kamati Kuu ambayo hivi Karibuni itatolea ufumbuzi swala la Madiwani kwa mujibu wa Katiba ya Chadema.


Thanx Dr. Slaa kwa ufafanuzi.
 
Back
Top Bottom