Majibu ya Dr. Slaa kwa maswali ya watanzania, Julai 2011

Dr Willibrod Slaa

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
675
1,523
Zumbemkuu,

Wana JF awali nawasalimu. Ni muda kidogo sijapost kwenye jamvi japo nimekuwa nikichungulia ama kama member ama kama guest. Nimeona ombi na nimeielewa.

Pamoja na kuwa sina tatizo kutoa mchango wangu kama mkereketwa wa maendeleo ya Taifa letu, na kuchukizwa sana giza totoro linaloikimba nchi yetu, ni maoni yangu kuwa hoja nyingi zilizoko zinahitaji majibu ya Serikali na Chama Tawala. Kwa vile wako wa Chama tawala humu, ninashauri maswali hayo waelekezewe hao tuliowapa dhamana na wanakusanya kodi zetu.

Niko tayari kuchangia pale yatakapohitajika maoni yangu kuhusu jambo lolote lile kama maoni hayo yanaweza kusaidia tusonge mbele. Swala la Madiwani wa Arusha nimekuwa nikilitolea ufafanuzi wa mara kwa mara kwenye vyombo vya habari. Kama kuna mtu anahitaji ufafanuzi wowote, nitakuwa tayari kuutoak, alimradi ni ndani ya uwezo na mamlaka yangu kwa mujibu wa Katiba ya Chadema.

Nawashukuru sana na ninawatakia mjadala mwema, nikitegemea wahusika wa chama tawala watajitokeza wazi pia. Taifa ni letu sote na litajengwa na wale tu wenye nia njema na Taifa hili.
tunaomba Dr.Slaa uje tena JF ajibu maswali ya moja kwa moja,yapo mengi ya kukuuliza hasa kipindi hiki mfano:-
  • giza totoro na majibu mepesi ya rais na mawaziri,
  • bahasha la jairo.
  • kujivua gamba kwa RA.
  • sakata la madiwani wa arusha.
  • umaskini unaozidi kukua na gharama za maisha.
 
Naona Dr.Slaa kachomoa kujibu maswali yetu kiutu uzima.Anataka chama legelege kilichozaa serikali legelege kijibu maswali yetu.
 
Naona Dr.Slaa kachomoa kujibu maswali yetu kiutu uzima.Anataka chama legelege kilichozaa serikali legelege kijibu maswali yetu.
Hakuchomoa isipokuwa itakuwa ujinga kwake kujibu maswali ambayo yanawahusu CCM. Yeye sasa hivi ni sawa na sisi, bila shaka naye angependa sana kusikia majibu ya CCM kuhusiana na adha hii ya kiza...

Hata hivyo nasikia Symbion wameanza kuzalisha na kunalipia capacity charges, mitambo ambayo kwa uharamu wake tuliikataa toka Richmond na tungeweza kuinunua Tanesco wakaitumia bila hizi charges. Kifupi nchi yetu imepoteza mwelekeo kabisa. Ni jalala na vyombo chakavu, mitumba hadi serikali kuu maanake nasikia hadi Hospitali zenu zinatumia vifaa chakavu kama sio feki..
 
Sasa wewe si unataka umeme, hata ukiwashwa kwa kutumia mavi ya ng'ombe si umeme? Wabongo bana.
 
Pamoja na kuwa sina tatizo kutoa mchango wangu kama mkereketwa wa maendeleo ya Taifa letu, na kuchukizwa sana giza totoro linaloikimba nchi yetu, ni maoni yangu kuwa hoja nyingi zilizoko zinahitaji majibu ya Serikali na Chama Tawala.

Kwa vile wako wa Chama tawala humu, ninashauri maswali hayo waelekezewe hao tuliowapa dhamana na wanakusanya kodi zetu
. Niko tayari kuchangia pale yatakapohitajika maoni yangu kuhusu jambo lolote lile kama maoni hayo yanaweza kusaidia tusonge mbele.

Dr. tunashukuru kwa kujibu, ila hapo kwenye red kamwe hawatakuja kujibu, tunashuhudia kinachoendelea bungeni, hoja za msingi zinazimwa na mawakala wa serikali ya CCM (spika na timu yake).

Jana pia kwenye mdahalo wa naibu spika mh. Ndugai na mh. Tundu Lissu tumeona wenyewe kwa macho yetu jinsi hao viongozi wa bunge wanapokuwa mawakala wa serikali, hatutarajii waje wajibu.
 
Ahsante Dr Slaa, nina maswali machache yanayohusu suala la Arusha. Awali ya yote naomba nijenge hoja ili maswali yangu madogo na rahisi yaeleweke.

Sakata la Arusha lilikuwa katika msingi wa kupinga taratibu za uchaguzi wa meya zilizokiukwa kwa mujibu wa madai ya Chadema. Tuliona viongozi wakipigwa kwa mabomu, watu kupoteza maisha na wengine kubaki na vilema. Ni wazi suala hili lilichakua sura ya kitaifa kama si kimataifa kama lilivyoripotiwa na vyombo mbali mbali duniani. Ghafla tukasikia makubaliano ya madiwani Arusha(na muafaka ni jambo zuri siku zote). Ilichukua zaidi ya wiki mbili uongozi wa taifa kutolea ufafanuzi licha ya tambo na kejeli zilizokuwa zinatolewa na washirika wa muafaka.

Maswali
1.Je lengo la maandamano ya Arusha na kwingineko limefikiwa?
2.Je, uongozi taifa wenye dhamana tangu mwanzo ulifahamu kuwepo majadiliano baina ya madiwani?
3.Iweje suala zito kama hili liachiwe madiwani ikizingatiwa gharama kubwa iliyolipwa na wanachama
4.Kama uongozi ulifahamu,kwanini wanachama na wapenzi hawakutaarifiwa hadi habari zilipoletwa na kiongozi wa CCM
5.Je,uongozi mzima wa Chadema katika ngazi ya wilaya na mkoa ulihusika katika majadiliano.
6.Kamati ya mabere iliundwa kuchunguza kitu gani uongozi wa taifa uliokuwa haukijui na matokeo ya uchunguzi huo yameleta tija ipi Chadema
7.Kama madiwani wanagomea maamuzi ya uongozi wa taifa, Chadema inajengwa kwa misingi(principles) au haiba(personalities)
8.Nini unadhani itakuwa uungwaji mkono katika base ya chama siku za usoni kutokana na jinsi suala hili lilivyoshughulikiwa(handled in general)
9.Unawaambia nini wanachama na wapenzi wa Chadema kuhusu hatima ya sakata hili baada ya uchunguzi na malumbano yanayoendelea
10.Je mapungufu(kama yapo) ya suala hili yametokana na nini

Ahsante

Nguruvi
 
TUNAKUSHUKURU SANA DR. SLAA KWA KUITIKIA WITO WETU.

Mchango wako katika chama chako na kwa Maendeleo ya Taifa hili tunauthamini haswa! Mjadala naimani utapatiwa majibu!
 
Dr Slaa, nashukuru kwa kuwepo kwako leo, naomba kujua msimamo na mkakati wa CHADEMA, kuusu uporwaji mkubwa wa ardhi kwa kisingizio cha uwekezaji. Je swala hamuoni kama linahitaji kuvaliwa njuga kama mlivyofanya kwenye ufisadi.
 
Nguruvi3,

Ahsante kwa maswali yako. Naomba niyajibu kwa pamoja ifuatavyo:-

1) Msingi wa mgogoro wa Madiwani Arusha ni Uvunjifu wa Kanuni, Taratibu na Sheria zinazoongoza uchaguzi wa U meya katika Manispa ya Arusha. Kamati ya Marando imebaini kuwa "mchakato na utaratibu mzima wa uchaguzi wa Naibu Meya haikuzingatia Kanuni na Taratibu za Chama na Halmashauri" (Marando Kif.4.2). Hivyo, kama Chadema ilipinga ukiukwaji katika uchaguzi wa Meya, haiwezi kamwe kuidhinisha ukiukwaji ambao kwa bahati mbaya ni maradufu zaidi katika uchaguzi wa Naibu Meya.

2) Ni kweli mazungumzo husika yalijulikana kwa ngazi ya Taifa. Mara ya kwanza Makao Makuu yalifahamu document ya mwafaka ya 15/4/2011, kwa kuona document tarehe 29/4/2011 katika Mkutano baina ya viongozi wa Madiwani akiwemo Mwenyekiti wao Mhe. Mallah na Mnadhimu Mkuu wa Kamati ya Madiwani Mhe. John Bayo. Kikao kilifanyika New Safari Hotel, Arusha chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu. Miniti za Kikao hicho zinaonyesha mambo 5 ambayo Katibu Mkuu alibainisha kama msingi wa mazungumzo yeyote kama yatakuwepo. Nayo ni:-

i)Serikali ikiri kosa kuwa kanuni na mwongozo wa uchaguzi wa Meya Arusha mjini zilikiukwa.
ii)Uchaguzi wa Umeya urudiwe kwa vile haukufuata kanuni na Taratibu.
iii)Serikali itoe pole kwa wahangaa tukio la tarehe 5 Januari 2011
iv) Serikali ipitie madai ya msingi ya Chadema ikiwa ni ni kuwawajibisha Mkurugenzi wa Manispaa (kwa sababu ndiye alivunja kanuni) na OCD wa Arusha mjini
v) Kesi ya ya Viongozi wa chama na baadhi ya wananchi haina msingi hivyo ifutwe.

Kisha kikao kilijadili document ya 15/4 na kuona ina mapungufu makubwa. Iliazimiwa ifuatavyo:-
1) Miniti hii ina hila na ni ya unafiki na hivyo isitumike katika kufikia muafaka wa suala la Umeya hapa Arusha mjini.
2) Mwenyekiti wa Madiwani Estomih Mallah na Mnadhimu wa Madiwani Mhe. John Bayo wawajulishe madiwani na Mkuu wa Wilaya kuwa muafaka huu kwa mujibu wa chama una mapungufu ambayo chama hakitaweza kuyaafiki na hivyo usitumike kwa kufikia muafaka wowote.
3) Kwa kutambua kuwa CCM wapo tayari kwa mazungumzo, Mhe. Katibu Mkuu atayapeleka mapendekezo ya muafaka huu kwa wanasheria wa chama ili kuyafanyia marekebisho na mapendekezo hayo yatakuwa ni sehemu ya mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa Chama Mhe. Freeman Mbowe (MB, KUB na Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda.

Kwa bahati mbaya, tarehe 20/6/2011 Madiwani waliridhia mwafaka wao kama ulivyokuwa kwenye Hati yao ya tarehe 15/4/2011, na kuendelea na uchaguzi, bila kujali mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kati ya Mhe. Mbowe na Waziri Mkuu. Isitoshe utaratibu wa kisheria wa uchaguzi wa Naibu Meya nayo ilikiukwa (kwa mujibu wa Taarifa ya Marando kukiwa na kugushiwa kwa saini ya Katibu wa Wilaya wakati pia hakuna kikao chochote cha Kamati Tendaji kilichojadili na kuteua mgombea wa Chadema). Hiki ndicho kilichofikisha Kamati Kuu kuelekeza Madiwani waliochaguana kinyume na Kanuni wajiuzulu ndani ya siku 3.

Baada ya hapo Madiwani 6 wakiongozwa na Mallah walikata rufaa, kwa bahati mbaya kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama rufaa zao hazikukidhi mahitaji ya Kikatiba na Kanuni. Maswala yote hayo sasa yanarudi mikononi mwa Kamati Kuu ambayo hivi Karibuni itatolea ufumbuzi swala la Madiwani kwa mujibu wa Katiba ya Chadema.

Ahsante Dr Slaa, nina maswali machache yanayohusu suala la Arusha. Awali ya yote naomba nijenge hoja ili maswali yangu madogo na rahisi yaeleweke.

Sakata la Arusha lilikuwa katika msingi wa kupinga taratibu za uchaguzi wa meya zilizokiukwa kwa mujibu wa madai ya Chadema. Tuliona viongozi wakipigwa kwa mabomu, watu kupoteza maisha na wengine kubaki na vilema. Ni wazi suala hili lilichakua sura ya kitaifa kama si kimataifa kama lilivyoripotiwa na vyombo mbali mbali duniani. Ghafla tukasikia makubaliano ya madiwani Arusha(na muafaka ni jambo zuri siku zote). Ilichukua zaidi ya wiki mbili uongozi wa taifa kutolea ufafanuzi licha ya tambo na kejeli zilizokuwa zinatolewa na washirika wa muafaka.

Maswali
1.Je lengo la maandamano ya Arusha na kwingineko limefikiwa?
2.Je, uongozi taifa wenye dhamana tangu mwanzo ulifahamu kuwepo majadiliano baina ya madiwani?
3.Iweje suala zito kama hili liachiwe madiwani ikizingatiwa gharama kubwa iliyolipwa na wanachama
4.Kama uongozi ulifahamu,kwanini wanachama na wapenzi hawakutaarifiwa hadi habari zilipoletwa na kiongozi wa CCM
5.Je,uongozi mzima wa Chadema katika ngazi ya wilaya na mkoa ulihusika katika majadiliano.
6.Kamati ya mabere iliundwa kuchunguza kitu gani uongozi wa taifa uliokuwa haukijui na matokeo ya uchunguzi huo yameleta tija ipi Chadema
7.Kama madiwani wanagomea maamuzi ya uongozi wa taifa, Chadema inajengwa kwa misingi(principles) au haiba(personalities)
8.Nini unadhani itakuwa uungwaji mkono katika base ya chama siku za usoni kutokana na jinsi suala hili lilivyoshughulikiwa(handled in general)
9.Unawaambia nini wanachama na wapenzi wa Chadema kuhusu hatima ya sakata hili baada ya uchunguzi na malumbano yanayoendelea
10.Je mapungufu(kama yapo) ya suala hili yametokana na nini

Ahsante

Nguruvi
 
usisahau maswali yaliyoulizwa na wananchi legelege waliopigia kura serikali na viongozi legelege!
Naona Dr.Slaa kachomoa kujibu maswali yetu kiutu uzima.Anataka chama legelege kilichozaa serikali legelege kijibu maswali yetu.
 
Babu wa Loliondo,

Kwanza pole,

Naomba kwa kifupi: Uporaji wa Ardhi, Rasilimali za Taifa/ Mali Asili zetu, ufisadi zimebaki kuwa kuwa katika ajenda za Chadema. Katika Maandamano yetu maeneo mbalimbali yote hayo ni ajenda za kudumu lengo likiwa ni kuunganisha nguvu ya watanzania wenye uzalindo kutetea, kulinda na kutunza rasilimali zetu.

Wajibu wa Chadema, ambayo kwa leo haiko madarakani kazi yetu ni kuwaelimisha umma mpana wa Watanzania, na hatimaye wote kwa pamoja na kila mmoja kwa nafasi yake tutimize jukumu letu la kizalendo katika kutunza rasilimali za Taifa letu katika nyanja zake zote na siyo Ardhi peke yake.

Ni dhahiri Ardhi ndiye mama wa yote, Madini yako ndani ya Ardhi, Maji yako juu ya Ardhi, Misitu iko juu ya Ardhi na hata binadamu hujenga juu ya Ardhi.

Dr Slaa, nashukuru kwa kuwepo kwako leo, naomba kujua msimamo na mkakati wa CHADEMA,
kuusu uporwaji mkubwa wa ardhi kwa kisingizio cha uwekezaji.
Je swala hamuoni kama linahitaji kuvaliwa njuga kama mlivyofanya kwenye ufisadi.
 
1. Mna mkakati gani kuhusu Jimbo la Igunga?
2. Je, ni kweli kuwa utagombea hapo Igunga?
3. Sheria mpya ya maandamano mtaizuiaje?
 
Dr. Slaa

Nimekuwa ni mfatiliaji wa karibu wa Kikao cha Bunge kinachoendelea na namna Kinavyoendeshwa kwa Spika hasa Naibu Spika kuwa kandamiza sana Wapinzani na ( Hata jana kwenye Mdahalo ameonesha kwamba ana Chuki na CHADEMA). Hali hii Dr ikiachwa bila kukemea itapelekea Wabunge wa Upinzani kujiona ni Inferior ambacho naamini ndiyo hasa lengo la CCM ikiwatumia Spika na Naibu Spika.

Tumeona namna Naibu Spika anapovumila Uvunjifu wa kanuni hasa pale inapowahusu CCM na kuwa mkali pale inapowahusu Wapinzani.

Dr. Slaa wanannchi wanakerwa sana na hii Tabia ya Naibu spika ila wanakerwa zaidi na Ukimywa wa CDM katika kulikemea hili ikibidi kutumia Nguvu ya Uma kushinikiza Hatua zichukuliwe dhidi ya Viongozi hawa.

Nakumbuka Mheshiwa Shelukindo aliruhusiwa asome barua inayomhusu Jairo lakini Tundu Lisi alikatazwa na kuambia aandike Ushahidi

Nataka Kufahamu kama kama CDM kinayaona haya? na nini Msimamo wake/

Asante sana
 
Dr.W.Slaa utagombea ubunge kwenye huu uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga? kama hutagombea kwa nini?
ahsante.
Saint Ivuga
 
Saint Ivuga,

Igunga kimsingi ni ya wana Igunga. Wao ndio wanaofahamu mwana Igunga mwenye kuijua vizuri Igunga, na mwenye Uchungu nayo. Si amini katika kugombea kwa lengo la kupata Ubunge.

Naamini Mbunge kuwa mwakilishi wa watu wake. Mimi nimerwawakilisha wananchi wa Karatu kwa miaka kumi na tano. Sasa nina jukumu la kujenga chama, ambacho nacho kikiwa imara kitawanufaisha wana Igunga. Ni mgawanyo wa majukumu. Ndicho tunachoamini ndani ya Chadema, nani anaweza kufanya vizuri nini na wapi na kwa wakati gani.

Ninawashauri na kuwashawishi sana Wana Igunga wenye sifa popote walipo wajitokeze ili tuweze kuijenga Igunga.

Mh. Dr. Slaa tunakushukuru kwa kuwepo hapa jamvini leo, wewe ni kiongozi makini unawasikiliza watanzania wenzako wanapokuhitaji basi huna kinyongo kujumuika nao.

Kulikuwa na taarifa hapa jf na hata huko mitaani kwamba aliyekuwa mgombea ubunge wa cuf 2010 huko igunga yuko kwenye mazungumzo na chadema ili agombee nafasi hiyo kupitia chadema, je kuna ukweli wowote kuhusu jambo hilo?

Natanguliza shukrani.
 
DR slaa .ukiwa kama ndio katibu wa chama unafanya nini kuelimisha wabunge wawe na sauti ya pamoja katika maswala ya pamoja kule bungeni kwa kuwa naamini japokuwa kuna kanuni za bunge ambazo kwa kiasi kikubwa watawala wanazitumia kukandamiza michango ya maana kutoka kwa upinzani.

Je, kuna mkakati wowote unaowezwa kufanywa kwa sasa ili kuhakikisha bunge linakuwa na uwezo wa kukataa bajeti za wizara mojamoja bila kuadhiri bajeti kuu.

Je, kuna mpango wowote maalum ambao upo ambao kwa ajili ya kuwajengea uwezo na kuwapa data (analysis ) baadhi ya wabunge wetu ili waweze kuchangia kikamilifu badala ya kusinzia?

Mwisho: Ni vyema kukawa na mkakati ndani ya chama wa kutengeneza documentary au CD za kila tukio maalum ndani ya chadema kama maandamano ambalo litasaidia sana kuimarisha chama na kuwafikia wtu wengi?
 
Dr, u have said it all and I am so proud of u! Viva la chadema! Uroho wa madaraka sio ajenda mojawapo! Ni aibu kwa kiongozi kutangatanga kutafuta vyeo. Umesikika!
Saint Ivuga,

Igunga kimsingi ni ya wana Igunga. Wao ndio wanaofahamu mwana Igunga mwenye kuijua vizuri Igunga, na mwenye Uchungu nayo. Si amini katika kugombea kwa lengo la kupata Ubunge.

Naamini Mbunge kuwa mwakilishi wa watu wake. Mimi nimerwawakilisha wananchi wa Karatu kwa miaka kumi na tano. Sasa nina jukumu la kujenga chama, ambacho nacho kikiwa imara kitawanufaisha wana Igunga. Ni mgawanyo wa majukumu. Ndicho tunachoamini ndani ya Chadema, nani anaweza kufanya vizuri nini na wapi na kwa wakati gani.

Ninawashauri na kuwashawishi sana Wana Igunga wenye sifa popote walipo wajitokeze ili tuweze kuijenga Igunga.
 
Kama Katibu Mkuu wa magwanda, inabidi awe na busara zaidi yenu, capacity ya mtu hujulikana katika maswali kama hayo ambayo nyinyi mnayaona yanawatatiza, hivi, hawa viongozi wanawaongoza watu wa aina fulani tu katika tabaka za jamii?

Na kama hatoyajibu ntajuwa kuwa na yeye "capacity" yake si ya uongozi wa Taifa, msishabikie maswali sio yenu, as Katibu Mkuu anatakiwa awe makini na sio mwenye papara kama nyie. Kaeni kimya mumuwache Slaa ajibu au akatae, msimsemee tafadhali.
 
Back
Top Bottom