Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Duh Pwida.. yaani ningepata hiyo link few days ago...ingesaidia kweli. Well.. I hope next time. Ila nashukuru I could use some information sometimes later.
Nikisoma makala ya mzee Mwanakijiji na jibu kutoka ofisi ya waziri mkuu, nashawishika kuamini jibu kutoka ofisi ya waziri mkuu. Kwa sababu moja ya msingi: Imeambatana na takwimu na element za utafiti. Takwimu na utafiti ni weakness kubwa ya postings za JF.
Vilevile hii hali ya kusingizia vitisho serikali inapotoa jibu la makala zetu inamomonyoa utashi wetu JF.
Nikisoma makala ya mzee Mwanakijiji na jibu kutoka ofisi ya waziri mkuu, nashawishika kuamini jibu kutoka ofisi ya waziri mkuu. Kwa sababu moja ya msingi: Imeambatana na takwimu na element za utafiti. Takwimu na utafiti ni weakness kubwa ya postings za JF.
Vilevile hii hali ya kusingizia vitisho serikali inapotoa jibu la makala zetu inamomonyoa utashi wetu JF.
Mgonjwa wa Ukimwi;
"NO INVESTIGATION NO RIGHT TO SPEAK" Ben Mkapa, Nkurumah Hall, 1990's'
Mnatoa hoja mkijibiwa mwaanza kusema mnatishiwa maisha tuoeni hoja na ninyi zenye takwimu kama zilivyotolewa na Ofisi ya Waziri mkuu, au tuamini ilikuwa udaku kama ilivyokawaida ya JF?!!!
Ukitaka kuchafua tu serikali bila kuwa na hoja unatakiwa kujiunga na vyama vya siasa na katika hilo huna haja ya kujificha... unajitokeza kama Mtikila, Mrema and the like...
Naona niongezee kuwa kama waziri mkuu alitaka kuonyesha jinsi gani serikali yake imepambana na maadui wa maendeleo angeonyesha jinsi walivyopambana na Umaskini, Ujinga, Magonjwa na Dhuluma. Inashangaza kuona kuwa serikali haitaki kuongea chochote kuhusu huyu adui wa maendeleo ajulikanaye kama Dhuluma. Dhuluma ina sura nyingi sana na mojawpao ni rushwa kama vile mikataba ya hovyo ya Richmond na upendeleo (nepotism) kama vile utoaji vyeo kwa wanamtandao bila kujali uwezo wao.
Katika yote yakiyoongelewa katika mada hii kilichonisikitisha wala sio majibu ya Waziri Mkuu..ninasikitishwa na wana jambo ambao wameamua kushambulia hoja iliyopelekea majibu hayo..
Huu ni uthibitisho tosha kuwa hao viongozi wetu wamefanikiwa kiasi kikubwa ku-shape akili za watanzania vile watakavyo..yaani kuwafanya waone kuwa kila kinachosemwa na serikali ni sahihi..hata wasomi wenye uwezo wa kuchambua mambo waridhike na statement za kiongozi bila kuuliza... Kwa maneno mengine seriakli ya CCM imefanikiwa kwa kiasi fulani kutuwekea uvivu wakufikiri..Kitendo cha kumkejeli Mwanakijiji..ati anaandika bila takwimu, au anaogopa nini wakati uandishi kautaka mwenyewe..kwangu naona kama its a plus to the CCM govt..wametuharibu akili kweli...wakiongea tu tunaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe..baadae tutasema CCM wachawi.. Yes, ni wachawi to the extent kwamba wametujengea culture ya silence, hivyo kwamba anayethubutu kuongea basi tunamuona msaliti, tunawaaacha wasaliti tunauana wenyewe..What a sorry state of affairs
Tuseme hoja ya Mwanakijiji haina maana for lack of research/statistics; swali litakuwa, Why did they bother to respond, tena so vehemently?
Mwenye statistics azilete hapa JF zimsaidie Mwanakiji kujenga hoja; afterall its not a film show, kwamba sisi tukae tuangalie mtu mmoja akipigana na serikali hapo kwenye stage halafu tushangilie mshindi..kama mtu ana data/takwimu anazoona zinapingana au zinakubaliana na hoja aziweke hapa zisaidie kuboresha hoja, mambo ya kutishana, kudharauliana , kukujeliana hayafanani na msimamo wa JF
Ni mawazo yangu tu...
Aloo, unajua bado tunasubiri ngwe ya pili ya ile mada ya malalamiko uliyoanzisha juu ya ahadi hewa za Kikwete wakati wa uchaguzi??
Chondechonde tena safari ijayo tunataka na wewe utuwekee takwimu na vikolombwezo vinginevyo vya kutetea hoja zako, na siyo nadharia kavu na riwaya dizaini ya John Rutasingwa.