Majibu rasmi ya BoT juu ya nyumba ya Ndulu

Nashindwa kuweka post kwa sababu bado naona kuwa huu ni wizi tu na sijui ni nani alaumiwe; $1.2m ni nyingi sana kwa ujenzi wa nyumba hizo nilizoona sehemu mbalimbali. Tatizo la nchi yetu ni kuwa watu hangalia bei za nyumba huko Marekani na kuzitumia kupanga bei za hapa Tanzania!!
Je hili ni tatizo la client ama contractor?
 
Hapo juu nimekufahamu...

Nimekufahamu kuwa tatizo hapa ni Ndulu na sio gharama za ujenzi. Kama ndio hivyo basi sina swali lingine unless otherwise kama hukubaliani na gharama za ujenzi huo.

Sasa mzee mie sikufahamu unataka kutwambia nini mie nimejaribu kukupambanulia kuwa huo ndio usanii wenyewe umesema hauoni. Hembu chukulia mfano wewe unateuliwa kuwa rais wa kampuni, halafu wewe ndio mhasibu wa kampuni halafu wewe ndio msimamizi wa kampuni who will held who accountable for his/her action??? Ukijibu swali hili nadhani utaelewa kwanini watu wanalalamikia 1.4 Billion otherwise inawezekana tunakipigia gitaa but wewe mwenyewe umeziba masikio
 
Timu ya wataalamu waelekezi ikiongozwa na M/S SKY Architects Consultants iliajiriwa kutengeneza michoro na ramani za nyumba hizo. Michoro miwili ilichaguliwa, moja kwa kila nyumba ili wataalamu hao watengeneze ramani kamili ya ujenzi. Nyumba zote mbili zilipangwa ziwe za ghorofa moja, vyumba vitano vya kulala, wenyeji na wageni, sebule ya wageni, sebule ya familia, mahali pa kulia na vyoo na mabafu yanayoendana na idadi ya vyumba. Majengo ya nje ni pamoja na nyumba ya kuishi watumishi, gereji ya magari, bwawa dogo la kuogelea, ukuta na vyombo vya usalama na kibanda cha walinzi.

Pamoja na kuwapongeza kwa kuwa wawazi lakini bado. Hapa ndipo kwenye matatizo. Mhimili mkuu wa gharama za ujenzi ni architect na siyo mkandarasi. Huyu akishirikiana na mshitiri ndiyo wanaoamua nyumba au jengo litakuwa na gharama gani kwa kuweka vigezo vyao. Mahitaji haya yanahusu idadi ya vyumba, ukubwa wa vyumba na namna vyumba vitakavyomalizwa. Na hawa waheshimiwa wakishirikiana na wakadiriaji gharama na mabosi wangu, wahandisi ada yao sio ndogo. Ni vyema basi tungefahamishwa walichaguliwa vipi? Ni direct appointment au walishindanishwa? Majengo ya nje ya wakina nani maana inaelekea si makazi ya watumishi? Hayo majengo ni pamoja na nyumba ya wageni? Juu ya vyumba vitano vya kulala?

Halafu ukiangalia mambo yaliyowekwa humo ni vizuri kujiuliza ulazima wake. Vyumba vitano vya kulala vya nini? Kuna ulazima gani kila chumba kiwe na bafu lake? Sebule ya wageni na sebule ya wenyeji za nini? Au moja ilitakiwa iwe majlis kwa ajili ya wakina mama. Bwawa la kuogelea la nini? Viyoyozi vya kila chumba vya nini? Gereji ya magari mangapi? Kwenye picha inaonekana kuna gereji ya gari mbili iliyojumuishwa kwenye nyumba kubwa. Wanataka kutuambia kuwa kuna gereji nyingine?

Tukumbuke kuwa kama hawa wanapewa nyumba bure ( juu ya mshahara wa dola 15000 kwa mwezi) ni lazima gharama za kuhudumia hiyo nyumba zitabebwa na taasisi. Hivyo viyoyozi, maji ya bwawa la kuogolea, taa za kwenye vyumba vyote hivyo , vyote vinagharimu mapesa. Ukiangalia picha hakuna ishara kuwa palifanyika jitihada yeyote ya kupunguza gharama za kuendesha jengo. Hakuna solar panels kwa ajili ya maji ya moto ya bafuni na jikoni. Hakuna solar panels za kutengeneza umeme. hakuna dalili kuwa maji ya mvua yanakusanywa kwa hiyo maji yote, pamoja na ya kwenye bwawa na ya kunyweshea bustani ni kutoka Dawasa. Madirisha hayatoa matumaini ya ventilation ya kutosha kwa hiyo viyoyozi ni 24/7.

Hapa tumeliwa na kwa bahati mbaya ndiyo mind set ya viongozi wetu. Inawezekana nia ilikuwa nzuri lakini utekelezaji ulikuwa mbovu. Viwango tunavyojiwekea si vya nchi hii. Marekani bosi wao wa benki kuu anakaa kwenye nyumba yake mwenyewe na anaendesha Ford Focus analoshirikiana na mke wake! Hizi stahili zinabidi ziangaliwe upya. Hazitufai.

Kama Tabora jazz walivyosema, " nachoka kabisa".

Amandla.........

Sasa mzee mie sikufahamu unataka kutwambia nini mie nimejaribu kukupambanulia kuwa huo ndio usanii wenyewe umesema hauoni. Hembu chukulia mfano wewe unateuliwa kuwa rais wa kampuni, halafu wewe ndio mhasibu wa kampuni halafu wewe ndio msimamizi wa kampuni who will held who accountable for his/her action??? Ukijibu swali hili nadhani utaelewa kwanini watu wanalalamikia 1.4 Billion otherwise inawezekana tunakipigia gitaa but wewe mwenyewe umeziba masikio
Sawa sawa kamanda, pamoja na mfano wako mzuri ambao unaonyesha jinsi gani usanii unaweza kufanyika. Nilichokifahamu ni ushiriki wa Nduli tokea mwanzo wa project hiyo. Hata hivyo hii haina maana kuwa gharama hizo sio sahihi.

Taarifa hiyo imeweka bayana jinsi project hiyo ilivyoondesha tokea hatua za awali hadi kupatikana kwa mjenzi. Iwapo gharama za ujenzi huo zitakuwa zimepangwa na BOT wenyewe na sio Wazabuni, basi hapo kuna ulazima wa kulalamikia hizo bilioni. Iwapo gharama za ujenzi zilipangwa na Wazabuni na kukubalika na client sioni kama kuna tatizo hapo.
 
Ningependa kuuliza kaswali kama kuna wajenzi humu ukumbini. Hivi leo nikitaka kujenga nyumba ya kisasa pale Tanzania, yenye vyumba vitano, sebule mbili, jiko ya kisasa, ikiwa na air conditioning na matenki ya maji safi itanigharimu kiasi gani? Achilia mbali bwawa la kuogelea kwa sababu tupo karibu na pwani nitaogelea pale Coco Beach. Tuseme viwanja Oyster Bay na Masaki havipatikani, basi kule Boko.

Hakuna mtu atakayeweza kukujibu. Inabidi ueleze vyumba vya ukubwa gani, vina nini ndani yake (self-container au la), unataka kutumia nini kujenga n.k. Jiko la kisasa maana yake nini? Unataka liwe na nini ndani yake? Ndiyo maana mara nyingi wataalamu wanapenda kujua eneo zima la jengo kabla ya kutoa makisio ya awali. Na ni makisio tu.

Amandla........
 
Fundi M.. hivi kuwawekea vyumba vya wageni kwenye nyumba za watumishi ni kwanini? Hivi Dar-es-Salaam hakuna hoteli za kufikia wageni? au ni wageni gani hawa ambao Benki Kuu inawafikiria kufikia kwa Gavana wao..?

Ndio maana nasema "ngojeni" kwani wamefanya kosa lile lile lakini Nguba kujibu kwa kutoa takwimu!
 
Sawa sawa kamanda, pamoja na mfano wako mzuri ambao unaonyesha jinsi gani usanii unaweza kufanyika. Nilichokifahamu ni ushiriki wa Nduli tokea mwanzo wa project hiyo. Hata hivyo hii haina maana kuwa gharama hizo sio sahihi.

Taarifa hiyo imeweka bayana jinsi project hiyo ilivyoondesha tokea hatua za awali hadi kupatikana kwa mjenzi. Iwapo gharama za ujenzi huo zitakuwa zimepangwa na BOT wenyewe na sio Wazabuni, basi hapo kuna ulazima wa kulalamikia hizo bilioni. Iwapo gharama za ujenzi zilipangwa na Wazabuni na kukubalika na client sioni kama kuna tatizo hapo.

Mkuu, wazabuni hata siku moja hawapangi gharama. Gharama zinapangwa na mshitiri pamoja na washauri wake. Washauri wanatakiwa kujua gharama za ujenzi kabla ya kuwaita wazabuni. Wazabuni wanachofanya ni kutoa bei yao kutokana na matakwa na masharti waliyopewa. Mshitiri kwa hali yeyote ile hawezi kukwepa lawama. Yeye ndiye aliyekuwa na uwezo wa kukataa makisio ya washauri wake kabla ya kuwakaribisha wazabuni. Atakubali bei ya mzabuni pale tu inapolingana na matarajio yake ya awali. Wazabuni hawana cheque tupu!

Amandla.......
 
Haya ni baadhi ya mambo yaliomo kwenye waraka wa Kanisa Katoliki Tanzania, bahati mbaya propaganda za akina Kingunge, 'askofu' Kakobe, Hiza Tambwe, Makamba na baadhi ya watu waliokubali kudanganywa kuwa eti ni kuchanganya mambo ya siasa na dini, zimefanikisha kutofikisha ujumbe vyema.

Waraka huo ulihoji kama kuna haja ya wananhi walipa kodi kujadiri na kuangalia mishahara, marupurupu ya viongozi kama yanaendana na hali ya uchumi wetu au ndiyo ufisadi wenyenyewe.

Nasikikitika sana hoja haikuangaliwa ila nani kasema ndiyo ikapewa umuhimu. Leo tunashangaa.

Nenda kaulize posho wanazolipana wizarani, kwenye mashirika, per diem za safari za ulaya/Aisa/Amerika. Kilio ni hicho hicho.
 
Na wabunge wako wapi kwenye hili? Kuna hata mmoja aliyelitolea tamko? kupeleka bungeni kujadiliwa? and is this outrage only on the internet? what about on the ground?
 
Fundi M.. hivi kuwawekea vyumba vya wageni kwenye nyumba za watumishi ni kwanini? Hivi Dar-es-Salaam hakuna hoteli za kufikia wageni? au ni wageni gani hawa ambao Benki Kuu inawafikiria kufikia kwa Gavana wao..?

Ndio maana nasema "ngojeni" kwani wamefanya kosa lile lile lakini Nguba kujibu kwa kutoa takwimu!

Sijui, Mkuu! Sina uhakika kama hivyo vyumba vya wageni vya ziada vipo. Ninachokusudia kusema ni kuwa taarifa yao haijitoshelezi. Kutokana na taarifa yao kuna majengo ya nje ya ziada kuliko yatayayohifadhi watumishi ndiyo maana nikakisia kuwa kuna nyumba ya wageni, kwa lugha yenu mlioenda shule, guest wing!

Amandla......
 
Watu wakishakula pesa usitarajie kuwa watashindwa kuhalalisha ulaji wao. Sasa naanza kuelewa kwanini twin towers zilitaka kuingia kwenye guiness book as the most expensive building in the world per sq mita. Kabla hatujasahau zinakuja hizi nyumba za kawaida ambapo hizo gharama hazijumuishi gharama za kiwanja. Zikifanyiwa tathmini nadhani zitafunja rekodi ingine ! SIJUI KWANINI HAWA JAMAA HAWATAKI KUFIKIRIA KUWA ZILE PESA NI KWETU WOTE NA WAO TUMEWAPA KAZI YA KUZILINDA TU!
 
Kwa mujibu wa mikataba yao.
Kuna tofauti yoyote na ile mikataba ya awali ya viongozi hao?

Tunaambiwa iliamuriwa kujengwa
Swala Je, kwa gharama gani?

Nyumba zilizokuwa huko zilikuwa ni magofu yaliyopigwa marufuku kuishi binadamu
Jamani hizi nyumba kweli zilikuwa magofu? Salaleee tena zilikuwa huko Osterbay?

Sasa standard ya nyumba hizo i.e. kuwa na vyumba vya wageni walinzi n.k. ndiyo specs zilizotolewa na uamuzi wa kujenga au mbwebwe za wanaokaa? Je wageni ni part and parcel ya BOT standards au viongozi wa mashirika yote ya serikali?

Sasa wataitwa CAG kuja kuhalalisha wizi. Watoe report ya waliokaa na kuamua nyumba mbili zijengwe kwa kiasi kilichotumika na waliokuwa kwenye hicho kikao.
 
Na wabunge wako wapi kwenye hili? Kuna hata mmoja aliyelitolea tamko? kupeleka bungeni kujadiliwa? and is this outrage only on the internet? what about on the ground?

Wakishapata zile millioni 40 za mashangingi wanasahau kazi waliyopewa na wapiga kura.
 
Fundi M.. hivi kuwawekea vyumba vya wageni kwenye nyumba za watumishi ni kwanini? Hivi Dar-es-Salaam hakuna hoteli za kufikia wageni? au ni wageni gani hawa ambao Benki Kuu inawafikiria kufikia kwa Gavana wao..?

Ndio maana nasema "ngojeni" kwani wamefanya kosa lile lile lakini Nguba kujibu kwa kutoa takwimu!
Mwanakijiji,
Nijuavyo mimi ni kwamba BOT inayo bajeti ya kuwasetiri wageni wake hotelini, kv New Africa Hotel. Sasa labda kuna tofauti kati ya wageni official na wageni wa kifamilia. Lakini nijuavyo hiyo bajeti ipo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom