Majibu haya ya serikali ni ya Kihuni!!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,461
39,928
Tuhuma za ufisadi dhidi ya viongozi:

Serikali yasema ni uzushi mtupu

(Kutoka gazeti la Uhuru)
NA MWANDISHI WETU


BAADA ya serikali kufuatilia kwa kina tuhuma za ufisadi dhidi ya viongozi wa serikali zilizotolewa na Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa, imebaini ni za uzushi na upotoshaji wa makusudi wa ukweli.

Tamko la serikali lililotolewa jana jijini Dar es Salaam lilieleza tuhuma za Dk. Slaa zinalenga kujengea umaarufu vyama vya siasa vya upinzani kwa kudhoofisha umoja wa kitaifa.

“Kwa ujumla, tuhuma za Dk. Slaa dhidi ya viongozi wa umma hazina ukweli wowote, bali zina lengo la kuchochea chuki dhidi ya serikali na kutaka kudhoofisha umoja na mshikamano wa taifa letu,” ilieleza sehemu ya tamko hilo.

Septemba 15, mwaka huu, Dk. Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, akiwa na viongozi wa muungano wa vyama vya siasa vya upinzani, alitoa tamko hadharani linalowataja watuhumiwa wa ufisadi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Temeke, Dar es Salaam.

Miongoni mwa tuhuma zilizotolewa na Dk. Slaa ni ubadhirifu wa mali za umma dhidi ya taasisi mbalimbali kama Benki Kuu ya Tanzania (BoT), NBC, NMB, mikataba ya ubinafsishaji na ununuzi wa mali za umma.

Serikali imefafanua kuwa, waliotajwa kuingiza fedha za kigeni nchini na baadaye kulipwa na BoT, walikuwa wameagiza bidhaa kutoka nje ya nchi miaka ya 1980, ambapo BoT ilipokea malipo yao kutoka NBC.

Tamko hilo lilisema BoT ilishindwa kuwalipa kwa wakati, baada ya kupokea fedha hizo NBC kwa sababu haikuwa na fedha za kutosha za kigeni.

Tuhuma kwamba kulikuwa na shinikizo kwa kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation ya Washington, Marekani, kupewa kazi ya kukagua hesabu za kampuni za uchimbaji dhahabu, serikali ilisema si kweli.

Ilieleza kuwa kampuni hiyo ilipatikana kwa kuzingatia sheria na kanuni za ununuzi wa umma na hakukuwa na shinikizo lolote.

Juu ya rushwa katika mkataba kati ya serikali na Alex Stewart, serikali ilisema suala hilo liko mahakamani, hivyo haina uwezo wa kulizungumzia.

Kuhusu tuhuma za uuzaji wa rasilimali za taifa, ununuzi wa ndege ya Rais, ubinafsishaji wa NBC na NMB, serikali ilisema hazina msingi wala ushahidi wowote, bali zinajaribu kujenga mazingira ya kujipatia umaarufu usiostahili.

Serikali imetafsiri tuhuma hizo kuwa jaribio la kuwavunja moyo wananchi, kuhusu manufaa ya utekelezaji wa programu iliyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 na kama ilivyotafsiriwa katika bajeti ya mwaka 2007/2008.

“Serikali inawahakikishia wananchi kuwa inapinga vitendo vya rushwa nchini kwa nguvu zake zote na msimamo wake ni thabiti kuhusiana na suala hili,” ilieleza sehemu ya tamko hilo
.
 
yangu macho..,duh..kama ungekuw amtihani nimempa mwanafunzi wangu ningempa negative marks..,

answers were extremely off-target..,
 
hahahahahahaha .... serikali yetu bwana.... ina majibu mepesi kwa hoja nzito.
 
msimamo wa wananchi uko pale pale, Bado serikali haijatoa majibu ya kuridhisha hivyo watuhumiwa wote ni mafisadi until further notice big up Dr Slaa naona umewakaba koo kweli kweli hawafulukuti hao wamezoea.
 
Hivi ni serikali ya kijijini gani iliyotoa "tamko hilo".. naona labda hii miwani yangu inaniletea matatizo
 
wameagizwa wasafishe nyumba kabla mpangaji hajarudi,
tutaona matamko mengi kuhusu list of shame,ila watanzania sio vipofu na viziwi wa kuwabadilisha IMANI YAO WALIYOKWISHA IJENGA,wamuulize MASAWE!
natamani watu kesho wasiende pale mnazi mmoja na waende MLIMANI kumsikiliza zito,
mzee mwanakijiji utabiri wako umetimia.!wananchi wameamua kuwaziria viongozi sasa!
na uhakika hata hawaombei ndo maana wanapapta na ajali..
simpendi FISADI
 
Dr. Slaa alisoma tu ripoti ya CAG. Sasa kama Mthibiti Mkuu wa Mahesabu ya Serikali anasema umetokea uporaji wa mali ya umma, iweje serikali hiyo hiyo iseme ni uzushi?

Kwenye misingi ya utawala bora, Auditor General akiripoti wizi wa mali ya uma umetokea, kinachobaki ni vyombo vya sheria kufuatilia na kuwashitaki wezi wahusika. Sio kusema ni uzushi!

Akina Chenge na Balali wanajua fika kwamba Dr. Slaa amenukuu tuu taarifa ya CAG, hakusema lake mwenyewe. Si kosa kunukuu taarifa za CAG. Kwani zinatolewa za kazi gani? Ni za kunukuu. Ndio maana hawadanganyi kwamba watamshitaki Slaa. Naomba Gary Mgonja aeleweshwe hivyo ili aache kudai kwamba atashtaki.

Anyway, wameshikwa pabaya sana hawa wenzetu, ni lazima watapetape. Sasa wamebanwa watoe tamshi, mlitaka waseme ndio ni kweli ni waporaji wakubwa wa mali ya uma? Inauma sana mtu kukuita mwizi na huku ameshika mkononi ushahidi kwenye ripoti ya CAG.
 
Haw serikali kupitia kwa waziriwa habari jana wametoa tamko lao japo feki kwani hawajajibu hoja hata kidogo, wao wameanza kusema mabo ya NMB NA NBC ambayo ukisoma kwenye maelezo ya mafisadi hayajatajwa ,naona wanatafuta jinsi ya kujinasua wanashindwas.

Eti wanasema kuwa wakurugenzi wa Tangold wameteulkiwa na serikali kutokana na vyeo vyao, mbona cjhenge sio mwanasheria mkuu wa serikali mbona mwanyika hajapewa huo ukurugenzi?

Mbona makatibu wakuiu wenginge wamehamishwa mbona wana bakia na vyeo vyao?

Iweje kampuni ya serikali isajiliwe nchini Mauritius?

Mbona kabidhi wasii mkuu wa serikali hayupo?

MNajibu haya ni ya kihuni sana nayatafuta kwenye soft copy halafu nitayaweka hapa.
 
Yaani baada ya kufuatilia "kwa kina" tuhuma za ufisadi, serikali ndio imekuja na "tamko" hilo? Duh! Sijui kama wasingefuatilia "kwa kina" tamko lingekuwaje? Kaazi kwelikweli!
 
hahahahahahaha .... serikali yetu bwana.... ina majibu mepesi kwa hoja nzito.


ni kwasababu wanatudharau sisi wananchi wake. wanajua hatuna elimu wala uwezo wa kufanya analysisi ya mambo wanakutu zuga na janja ya vyama vya upinzani against CCM! safari hii wamenoa maana hata makada wameanza kugutuka kuwa tukilala wachache watatuingiza shimoni na kutafuna kilicho chetu sote kama watanzania. kwenye rasilimali! tanzania kwanza chama baadae! tusikubali kufunikwa na scape gotting za ushindani wa kichama! lazima wajibu hoja baada ya hoja. kwa jinsi zilivyo nyingi nadhani itabidi watoe gazeti zima
 
Tumewazoe Hao Toka Uhuru Mpaka Leo,hayo Ndo Majibu Ya Kuwajibu Watu Wenye Akili Zao Timamu.
Problem Ya Viongozi Wetu Usanii Umewajaa.izo Issue Ni Raisi Mwenyewe Ndo Anatakiwa Kuzijibu Sio Wanasakizia Wengine/mamluki Kuua Soo.
 
Maneno matupu hayavunji mfupa. The books pale BOT hazibalance kuna a big hole sasa watueleze hao waliowapa pesa sijui meremeta, Import support, ujenzi hewa n.k.

Pesa ya walalahoi sio ya kuchezea chezea kama upatu.
 
Serikali yamjibu Slaa:

Yawatetea watu wanaotuhumiwa

na Mwandishi Wetu

WIKI mbili tangu wapinzani watoe tuhuma nzito za rushwa dhidi ya viongozi waandamizi serikalini na wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), serikali imetoa tamko ikitoa majibu yake.

Serikali katika tamko lake hilo lililotolewa kwa upendeleo maalumu kwa vyombo kadhaa vya habari leo hii, inakanusha tuhuma takriban zote zilizotolewa na wapinzani, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa.

Katika tamko lake hilo, serikali, inaziita tuhuma zote za Slaa, kuhusu Benki Kuu (BoT), Kampuni ya Tangold na nyinginezo kuwa ni za kizushi na ambazo zimetolewa pasipo kufanyika kwa utafiti wa kutosha.

Kuhusu Benki Kuu, serikali katika taarifa yake hiyo inasema; “Baada ya kufuatilia kwa kina kuhusu tuhuma hizi, serikali inatoa tamko kuwa ni za uzushi na upotoshaji wa makusudi wa ukweli. Aidha, tuhuma kuhusu majina ya wanaodaiwa kuingiza fedha za kigeni nchini na baadaye kulipwa na Benki Kuu, ni vyema ieleweke kuwa wadai wanaozungumziwa hawakuingiza fedha za kigeni nchini, bali walilipa fedha za Kitanzania kwa iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kama malipo ya kuagiza bidhaa kutoka nje katika miaka ya 80.”

Aidha, katika hilo serikali inasema BoT ilishindwa kufanya malipo hayo wakati huo, baada ya kupokea fedha kutoka NBC kutokana na kutokuwa na fedha za kigeni enzi hizo.

Bila ya kutaja wakati, serikali inaeleza katika taarifa yake hiyo kuwa, baada ya tuhuma za uwezekano wa kuwepo kwa malipo yasiyo sahihi kupitia akaunti hii kujitokeza, ilimuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kuteua mkaguzi wa kimataifa (International Auditing Firm) kwa utaratibu wa wazi wa zabuni ili kufanya uchunguzi maalumu na kuwasilisha taarifa yake serikalini.

“Uchunguzi huo unaendelea na serikali inasubiri ukamilike ili kuamua hatua muafaka. Mhe. Dk. Slaa na wenzake wanafahamu vizuri hatua zilizochukuliwa na serikali katika suala hili, kwani serikali ilitoa taarifa kwenye vyombo vya habari na imetoa maelezo ya hatua za utekelezaji wake bungeni mara kadhaa,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Kuhusu madai mengine ya wapinzani kwamba, ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kuhusu hesabu za Benki Kuu kwa mwaka 2005/06 kuonyesha mapungufu makubwa, serikali katika tamko lake inasema imepitia taarifa ya ukaguzi wa hesabu hizo, lakini haikuona hoja za ukaguzi zinazodaiwa kutolewa na CAG.

Mbali ya hilo, serikali inasema, taarifa ya hesabu za Benki Kuu kwa mwaka 2005/2006, ziliwasilishwa katika Kamati ya Fedha na Uchumi ya Bunge mapema mwaka huu na kukubaliwa na kamati hiyo na kwamba (kamati hiyo) iliwasilisha taarifa yake bungeni na Bunge likairidhia.

Serikali inaeleza katika tamko lake hilo kwamba, kwa nyakati tofauti, Kamati ya Fedha ya Uchumi ya Bunge pamoja na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) zimepata nafasi ya kutembelea miradi ya ujenzi wa majengo ya Benki Kuu ya Dar es Salaam na Zanzibar ili kupatiwa maelezo ya kutosheleza, kuhusu utekelezaji na gharama za miradi hiyo, hali ambayo inaifanya hoja ya Slaa kuonekana kuwa ni ya kubuni na yenye nia mbaya.

“Nia mbaya ya Mheshimiwa Dk. Slaa na wenzake katika kutoa tuhuma hizi, inadhihirishwa na upotoshaji wa makusudi wa takwimu zilizo katika hesabu hizi, ili kupindisha ukweli. Kwa mfano, anaituhumu Benki Kuu kutumia shilingi 522,459,255,000 (Bilioni 522.5) kwa ujenzi wa “Twin Towers” mjini Dar es Salaam. Ukweli ni kwamba kiasi hicho ni thamani ya mali zote za kudumu za Benki Kuu hadi tarehe 30 Juni, 2006. Taarifa hizi ziko wazi katika nyaraka zilizowasilishwa bungeni na zinaweza kuthibitishwa na mtu yeyote kutokana na Taarifa ya Benki Kuu ya Mwaka 2005/06 iliyosambazwa kwa umma,” inasema taarifa hiyo ya serikali.

Aidha, serikali katika tamko lake hilo, imewatetea watumishi wake wanaotajwa kuwa miongoni mwa mafisadi katika orodha ya Dk. Slaa, ikisema kuwa kwao wakurugenzi katika Kampuni ya Tangold Limited, kunatokana na uamuzi wa serikali na kuwa kampuni hiyo inamilikiwa kwa asilimia 100 na serikali.

“Wakurugenzi wa Tangold wameteuliwa na Serikali ya Tanzania, wote ni watumishi wa umma ambao ni pamoja na wale ambao Mheshimiwa Slaa anawatuhumu katika tamko lake.

“Watumishi hao wameteuliwa kuwa wakurugenzi wa Tangold kutokana na nafasi zao katika utumishi wa umma. Kuwa mkurugenzi katika chombo cha umma hakusababishi mgongano wa kimaslahi, kwani ni sehemu ya utumishi wa umma,” inasomeka sehemu moja ya tamko hilo la serikali.

Mbali ya hilo, tamko hilo la serikali linasema wakurugenzi hao wa Tangold hawana hisa katika kampuni hiyo, kwa sababu hisa zake zote zinamilikiwa na Mfuko wa Udhamini wa Maendeleo (Tanzania Development Trust) kwa niaba ya Watanzania wote.

“Kwa maana hiyo, wakurugenzi wa Bodi ya Kampuni ya Tangold hawana maslahi yoyote binafsi zaidi ya kusimamia maslahi ya Watanzania,” inasema taarifa hiyo.

Serikali katika tamko lake hilo, imekanusha madai mengine ya wapinzani, kwamba kulikuwepo na shinikizo kwa Kampuni ya Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation ya Washington, Marekani, kupewa kazi ya kukagua hesabu za kampuni za uchimbaji dhahabu.

Serikali katika tamko lake inasema, kampuni hiyo ilipatikana kwa kuzingatia sheria na kanuni za ununuzi wa umma na hakukuwa na shinikizo lolote.

Hata hivyo, kuhusu tuhuma zilizoelekezwa katika sekta ya madini, serikali katika tamko lake hilo imesema kutokana na unyeti wa suala lenyewe, inakusudia kulitoa tamko rasmi kuhusu jambo hilo katika taarifa nyingine maalumu kwa lengo la kuwaeleza wananchi ukweli kuhusu sekta hii.

“Sekta ya madini ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi yetu. Kutokana na unyeti wa sekta hii na tuhuma nzito zilizotolewa dhidi ya serikali juu ya sekta hii, serikali inaona ni vyema kutoa maelezo ya ufafanuzi zaidi. Hivyo, serikali itatoa taarifa maalumu na ya kina kuelezea wananchi juu ya sekta hili,” linasema tamko hilo.

Akizungumzia hoja za serikali katika tamko lake hilo, Dk. Slaa aliyejibu kwa maandishi kipengele kwa kipengele, anasema majibu takriban yote ya serikali yana mapungufu makubwa na akasema bado alikuwa akisubiri hatua za kisheria ili akatoe ushahidi alionao kuhusu madai yake mahakamani.

Katika sehemu moja ya majibu yake, Dk. Slaa anaeleza kusikitishwa na tamko la serikali linalozungumzia uchaguzi wa mwaka 2005 na kushindwa kwa upinzani, kuwa ndiyo sababu kuu ya wapinzani kujaribu kuwahadaa wananchi ili wawachague wao siku zijazo.

“Hoja hii ni ya watu walioshiwa, na wamebaki na fikra mgando. Nani kati yetu kipindi chote hiki amezungumzia masuala ya uchaguzi? Ni kazi yetu ya kikatiba kuelezea Watanzania pale ambapo serikali imefanya makosa. Si kazi ya upinzani kuipigia makofi serikali. Kazi ya kambi ya upinzani duniani kote inajulikana. Na ndiyo maana tuko kikatiba,” anasema Slaa katika majibu yake.

Aidha, Dk. Slaa anaitaka serikali kujieleza kwa wananchi ili ieleweke, badala ya kutafuta mchawi, na akasisitiza kuwa leo hii wananchi wanalalamika kila kona ya nchi maisha bora hayajaonekana, na kwamba vyama vya upinzani vina wajibu wa kuhoji kwa niaba ya wananchi kutaka kujua kuhusu rasilimali za taifa.
 
mbona hawakusema kama Tangold imesajiliwa nchini? mbona hawakuelezea biashara za Mkapa na Yona kule Mchuchuma..mbona hawakuelezea malipo ya Mkono ambayo ni zaidi ya asilimia 3 ya kisheria... majibu nusu nusu ni majibu ya kihuni!!
 
Tusaidie kukomesha na ikiwezekana kutokomeza kabisa ufisadi katika nchi yetu.Mungu tusaidie.
 
Akizungumzia hoja za serikali katika tamko lake hilo, Dk. Slaa aliyejibu kwa maandishi kipengele kwa kipengele, anasema majibu takriban yote ya serikali yana mapungufu makubwa na akasema bado alikuwa akisubiri hatua za kisheria ili akatoe ushahidi alionao kuhusu madai yake mahakamani.

This is what I am talking about, in fact ninazimia sana na huu msimamo ambao ni bold, iliyobaki sasa siasa ziachwe tusubiri mahakamani!
 
hakuna atakayekwenda mahakamani, unless wakubaliane kuwa JK, Lowassa, Mkapa, watakuwa tayari kusimama kama mashahidi...
 
hakuna atakayekwenda mahakamani, unless wakubaliane kuwa JK, Lowassa, Mkapa, watakuwa tayari kusimama kama mashahidi...


Ukifungua kesi mashahidi huitwa na mahakama kwenye kesi kubwa, hungoji mashahidi wakubali kwenda mahakamani. Wataitwa na wakikataa mahakama ina njia zake za kufuatilia hilo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom