MAJIBU: Biashara gani Ufanye

C.K

JF-Expert Member
Nov 5, 2010
394
162
Habarini wadau!

Nimekuwa nikisoma posts za watu wakiomba msaada juu ya biashara za kufanya kwa mitaji yao ambayo siwezi kusema ni mikubwa au midogo (mil.2 - 5). Kwanza ninawapa pongezi kwa mawazo na mtazamo huo wa kuzalisha hizo pesa kwani wengi wakizipata wanakimbilia kununua liabilities - vitu visivyozalisha kama simu za mkononi, vito vya thamani, gari za kutembelea, TV kuubwa n.k. badala ya kuwekeza kwanza. Watu kama hao ninawapa pole kwani umaskini hauwezi kuwatoka. Ok, kwa mtaji huo unaweza kufanya biashara mbalimbali kwa kadri ya soko na au upenzi wako mwenyewe-- duka, saluni, pikipiki/bodaboda, kufuga kuku, kilimo n.k.

Nimeambatanisha sehemu ya kitabu cha Ujasiriamali, MAFANIKIO YA KIFEDHA cha Robert K. inayoonyesha biashara gani unaweza kuanza nayo katika kuendea mafanikio ya kifedha (financial independency). Sura ya kwanza - UTANGULIZI na sehemu ya sura ya tano - Biashara za kufanya katika kitabu hicho chenye sura tano motomoto. Waliokisoma wanajua mambo yake. Ni zaidi ya kitabu. Kinafundisha, Chochea na Kuelekeza ufanye nini ili ufanikiwe kifedha. Kinapatikana bookshops na kwa wauza vitabu -- Ubungo, Mwenge, Posta, Kariakoo... na baadhi ya mikoa.

Hebu soma mwenyewe kiambatanisho hicho halafu utaniambia. SOMA ACHA UVIVU!

Kila la heri!

"kufanikiwa ni maamuzi.., kwa hiyo ukiamua utafanikiwa na kinyume chake ni sahihi"

 

Attachments

  • Biashara ya Kufanya - Mafanikio ya Kifedha.pdf
    379.1 KB · Views: 639
Ni kweli watu 2nanunua sana vitu badala ya kuwekeza jambo ni vizuri kununua usichonacho ili ukianza kuwekeza na kwa bahati mbaya ikala kwako usijutie saaaaana.

C.K senks kwa kitabu hebu ngoja nifungue na kukisoma kisha nitarudi.

shamito
 
Unaweza nunua usicho nacho na kikaungua au kupata ajali yoyote ile nakushauri bora uekeze watu wangekuwa na mawazo ya kwako wasingeekeza wangeogopa hasara
 
Unaweza nunua usicho nacho na kikaungua au kupata ajali yoyote ile nakushauri bora uekeze watu wangekuwa na mawazo ya kwako wasingeekeza wangeogopa hasara


Sijakuelewa...
 
Ziko pia biashara zingine nyingi mno, ni kiasi cha mtu wa kutaka kufanya biashara kukaa chini na kutafakari kwa undani, jamii iliopo inaitaji nini, hasa iliokaribu na huyo mtu.
Nimependa uchanganuaji wako, unatia moyo kwa kweli, hasa kwa sie wabongo tunaodhani ni lazima tuwe na mtaji mkubwa mno kufanya biashara, au kutokua wavumilivu na kutaka hela za chap chap, ambazo nyingi ni za wizi na rushwa!
Kudos C.K.
 
Back
Top Bottom