Maji ya kuoga...!

Museven

JF-Expert Member
Aug 22, 2011
629
447
Naomba msaada wanaJF. Hivi mwanamke kumwekea maji mumewe bafuni ni wajibu au ni fadhìla tu? Nauliza hivi sababu mke wangu haniwekei maji mpaka nimgombeze au siku akipenda mwenyewe. Siku nyingi nalazimika kujibebea mwenyewe. Nimeshagombana naye mara kadhaa lakini habadiliki. Nifanyeje?
 
Sema naye kwa hisani ya watu wa marekani na sio kugombana.
 
...kaka, kwani wewe unamuwekea maji ya kukoga?

wajibu na fadhila ni suala la hiari...kila moja lina shurti na hukumu zake
zinazojitosheleza kwa kadri ya maisha mnavyoyachukulia.
 
Naomba msaada wanaJF. Hivi mwanamke kumwekea maji mumewe bafuni ni wajibu au ni fadhìla tu? Nauliza hivi sababu mke wangu haniwekei maji mpaka nimgombeze au siku akipenda mwenyewe. Siku nyingi nalazimika kujibebea mwenyewe. Nimeshagombana naye mara kadhaa lakini habadiliki. Nifanyeje?

Kumwekea mwenzako maji bafuni ni penzi/fadhila. ukishurutishwa ni utumwa.
 
Duh! Yaani mnatufanya wanawake kama ni watumwa wa ndoa! Hivi kuna kitu chochote ambacho mwanamke anapaswa kuenjoy kwenye ndoa?! Kufua hadi vyupi,kupika kutumikia penzi mara sijui gogo,mara chai,mama mkwe,ndugu, watoto! Mwanamke role yake ni ipi na mwanaume yake ipi?
 
Unapenda ubosi eeh! We kupeleka maji bafuni vinakushinda? Kabla hujaoa ulikuwa unapelekewa na nani?
Acheni kukera na kuchosha wake zenu. Kwanza hata unyumba ni hiari yake akupe au akunyime.
umeonaeeeeeeeeeeee wao hilo hawalijui
 
Naomba msaada wanaJF. Hivi mwanamke kumwekea maji mumewe bafuni ni wajibu au ni fadhìla tu? Nauliza hivi sababu mke wangu haniwekei maji mpaka nimgombeze au siku akipenda mwenyewe. Siku nyingi nalazimika kujibebea mwenyewe. Nimeshagombana naye mara kadhaa lakini habadiliki. Nifanyeje?
Haya mambo mengine ni kujiendekeza tu na kuendekeza mfumo dume katika familia. Mimi nachopenda kukuuliza ni kwamba kwa hizo siku ulizobeba mwenyewe maji UUME wako ulitoweka?
 
Jiwekee shower yako mwenyewe uondokane na kuomba omba.
 
Naomba msaada wanaJF. Hivi mwanamke kumwekea maji mumewe bafuni ni wajibu au ni fadhìla tu? Nauliza hivi sababu mke wangu haniwekei maji mpaka nimgombeze au siku akipenda mwenyewe. Siku nyingi nalazimika kujibebea mwenyewe. Nimeshagombana naye mara kadhaa lakini habadiliki. Nifanyeje?

kwa utaratibu wa mila zetu za kiswahili .... mwanamke kabla hajaolewa (MWARI) anapofundishwa jinsi ya kuitunza ndoa yake basi hilo ni moja ya jukumu lake kuonesha jinsi mapenzi yake yalivyo ya dhati kwako....

sasa huyo wako hakuwekei seems she doesnt take you serious as a hubby ama kuna jambo unamfanyia halipendi, ama ulimuoa kwa kutafutiwa na wazazi .... kwa mila na taratibu zetu za kiafrika jibu ni kwamba hakupendi huyo
 
wanaume bwana. Kwani iliandikwa wapi kuwa lazima uwekewe maji? Acha uvivu. Si ajabu mkeo maji anachota mtaa wa tano. Anahakikisha mapipa 2 ya ndoo 12 yanajaa maji, bado akuwekee bafuni!

Kwani ukijiwekea mwenyewe unapungua nini? Mwisho mtataka kubebwa mgongoni.

Kujibu swali lako hiyo ni hiari. Ila Ni vyema kujibebea mwenyewe haitakudhuru.
Ila zungumza na mkeo. Jua majukumu yake nyumbani kama mwenzio ana kazi nyingi+watoto mpunguzie majukumu kwa kufanya vikazi vidogo vidogo, apate muda wa kupumzika na kufurahia tendo la ndoa!
 
Haya mambo mengine ni kujiendekeza tu na kuendekeza mfumo dume katika familia. Mimi nachopenda kukuuliza ni kwamba kwa hizo siku ulizobeba mwenyewe maji UUME wako ulitoweka?

hahaha labda ulipotea hakuuona hadi alipotengewa maji kwa bafu
 
Naomba msaada wanaJF. Hivi mwanamke kumwekea maji mumewe bafuni ni wajibu au ni fadhìla tu? Nauliza hivi sababu mke wangu haniwekei maji mpaka nimgombeze au siku akipenda mwenyewe. Siku nyingi nalazimika kujibebea mwenyewe. Nimeshagombana naye mara kadhaa lakini habadiliki. Nifanyeje?

mpige chini fasta..
 
Huu ndo mtazamo wangu;Tatizo liko kwako!Yes wewe ndo mwenye tatizo,kwanza jiulize kwanini akupelekee?Unaweza kuhisi ni upendo nenda kaulize vizuri maana ya upendo,pia jiulize ndoa maana yake nini,halafu jiulize wakati unaoa ni sababu zipi zilikufanya ukaoa.KUMBUKA sijasema kama kukupelekea maji bafuni ni kosa au sio kosa!
 
Duh! Yaani mnatufanya wanawake kama ni watumwa wa ndoa! Hivi kuna kitu chochote ambacho mwanamke anapaswa kuenjoy kwenye ndoa?! Kufua hadi vyupi,kupika kutumikia penzi mara sijui gogo,mara chai,mama mkwe,ndugu, watoto! Mwanamke role yake ni ipi na mwanaume yake ipi?

kama kupata 'msaidizi' ni hivi kazi ipo! Wasaidizi poleni
 
wanaume bwana. Kwani iliandikwa wapi kuwa lazima uwekewe maji? Acha uvivu. Si ajabu mkeo maji anachota mtaa wa tano. Anahakikisha mapipa 2 ya ndoo 12 yanajaa maji, bado akuwekee bafuni!

Kwani ukijiwekea mwenyewe unapungua nini? Mwisho mtataka kubebwa mgongoni.

Kujibu swali lako hiyo ni hiari. Ila Ni vyema kujibebea mwenyewe haitakudhuru.
Ila zungumza na mkeo. Jua majukumu yake nyumbani kama mwenzio ana kazi nyingi+watoto mpunguzie majukumu kwa kufanya vikazi vidogo vidogo, apate muda wa kupumzika na kufurahia tendo la ndoa!

Umejibu bila kufikir..... mke yuko nyumbani mme ana mizunguko ya kupata hata hizo pesa za matumizi hom kwani yy hachoki majibu ya wanawake wengi ktk hili imenipa picha ya kwa nn ndoa zinawashinda hili ni moja ya jukumu la mwanamke wa kiafrika kwa mmewe
 
Back
Top Bottom