Kwa muda mrefu nimekuwa najiuliza kwa nini majeshi yetu i.e Jwtz,polisi,magereza wanalazimisha kuajiri watu warefu peke yao?hii imekuwa kama ukiukwaji wa haki za binadamu,watu wafupi waliowengi ni wakakamavu na wanafanya mambo makubwa sana....ni Mungu aliumba wafupi na warefu wote wakiwa na ukamilifu kabisa wanaweza kufanya chochote na lolote popote kwa kutumia nyenzo au kwa asili. Ningeshauri majeshi yetu yaajiri kwa kuangalia uwezo(competence) kwa ujuzi,elimu,ukakamavu n.k. hiki kigezo cha kuzaliwa ambacho hawezi kubadilisha inapokuwa kikwazo inambania na kumkwaza mtu mfupi. nawafahamu wafupi kibao ambao wanahamu(interest) na ni wazalendo kwelikweli wameshindwa kujiunga na majeshi kwa kigezo hiki. Wote tunajua vimo wa wachina na mataifa mengi ya kiasia kama Korea lakini wana majeshi imara sana, tanzania ina watu wachache wanaozidi futi 6 na wengi ni chini ya hapo kwa nini kung'ang'ania kigezo hiki?
wanaJF naomba mawazo yenu
wanaJF naomba mawazo yenu