Majengo ya nic kuuzwa;kulipa madeni,ndege za atcl,treni za trl kufwata????masikini jk

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,778
UUZAJI wa Majengo ya Shirika la Bima (NIC), unatarajiwa kuliingizia shirika hilo Sh bilioni 40 ambazo zitatumika kuwalipa watu wote ambao wanalidai shirika hilo.

Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Yussuf Omar Mzee, aliliambia Bunge kuwa hadi sasa shirika hilo linadaiwa na wateja wake Sh bilioni 28.

“Tathmini iliyofanywa imebaini kuwa iwapo majengo hayo yatauzwa, zaidi ya Sh bilioni 40 zitapatikana, hivyo wateja wote wanaolidai shirika watalipwa madai yao,” alisema Naibu Waziri huyo.

Tathmini ya majengo hayo imefanywa na tayari imekamilika hivyo kilichobaki ni kuanza kuyauza.

Alisema kufanywa tathmini hiyo, kulichelewa kutokana na majengo hayo kuwa mengi ambayo yametapakaa katika sehemu mbalimbali nchini.

Majengo yanayouzwa kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo ni yale ambayo hayaambatana na biashara ya Bima, ili kupata fedha zitakazosaidia kulipia madeni hayo ambayo pia ni hatua za kulikwamua shirika hilo.

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Kondoa Kusini, Pascal Degera (CCM) aliyetaka kufahamu sababu za shirika hilo kutotekeleza majukumu yake kikatiba na hatua ambazo zinachukuliwa kuhakikisha kuwa wateja wa shirika hilo wanalipwa madai yao.

Katika majibu yake, Mzee alikiri kuwa NIC imechelewa ulipaji wa madai ya bima mbalimbali zilizoiva kwa baadhi ya wateja wake, kutokana na shirika kuwa katika hali mbaya ya kifedha.

Hali hiyo kwa mujibu wa Mzee, imetokana na kupungua kwa biashara ya shirika kutokana na ushindani wa soko na hivyo kushindwa kupata mapato ya kutosha ambayo yangemudu gharama za uendeshaji pamoja na kulipia madai ya bima.

Hata hivyo, kwa kutumia mapato yanayopatikana, shirika hilo limefanikiwa kulipa madai yenye thamani ya Sh bilioni 51.35 hadi kufikia Desemba 2008.

Pia aliongeza kuwa serikali imechukua hatua mbalimbali ambao zitasaidia kuhakikisha kuwa wateja wa shirika la Bima wanalipwa kwa haraka.

Alitaka hatua hizo kuwa ni kulifanyia marekebisho shirika la bima ili lijiendeshe kwa ufanisi, ikiwemo kupunguza watumishi kutoka 480 wa awali hadi kubaki 250.



KWA MTAJI HUU NAONA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO NDEGE ZA ATCL ,JENGO LAO PALE MJINI ZIKITAFUTIWA MTEJA

YALE MABEHEWA NA VICHWA VYA TRENI VYA TRL VIKIREKEBISHWA KWA AJILI YA UUZWAJI KULIPA MADENI.......JE KWA MTAJI HUU WA KUZA RASILIMALI ZILIZOTAFUTWA KWA SHIDA JAMANI NI SOLN YA KUTATUA MATATIZO YA SHIRIKA AMA ....??

MASKINI NCHI YETU
 
High time they did so..... hawa wapuuzi nawadai toka pesa kibao ambazo kwa vile sikukubali kuvunja principle yangu ya kutoa rushwa hawakuishughulikia. Mashirika
I can't see how a corporation which had a monopoly of insurance business for decades could go bankrupt if not for the mental bankruptcy of the vigogo's who were being awarded zawadi ya kulila shirika. Bora wafunge tu huu uozo, after they have paid my money!!
 
hahaha..................only in TZ.......... sasa wakimaliza majengo, wakipata madeni mengine watauza nini............. probable mak**** kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu........ mental shortsightedness!!!!!!!!...............
 
Sawa mnauza majengo halafu? Na huyo mliomuweka akileta hasara nyingine mtauza nini? Watanzania tunataka kuona mameneja wanaoletea mashirika ya umma hasara wanashughulikiwa kinidhamu na kisheria. Haiwezekani NIC wanadaiwa 44bl + halafu meneja yuko kwenye Su V8 ya shirika hilo hilohilo anarandaranda kwenye site za mansion zake mbezi beach na mikocheni.

Inabidi kubadili approach, yaani individual ambao hawakuwa responsible wafilisiwe kwanza ndipo hiyo mali ya umma iguswe. Kwa mtindo huo, atakaefuata atakuwa na nidhamu. Mbona kina Liumba wako mahakamani? au kwa vile hawana ma-Godfather. Let adopt Chinise style.
 
Back
Top Bottom