Majembe auction mart inapata nguvu wapi?

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
Nadhani kwa wakazi wa Bongo tunajua kuwa Majembe walipewa tenda ya kukamata mabasi yanayo katisha ruti au kutofuata masharti ya biashara hiyo lakini namna walivyopewa mimi binafsi sifahamu. Sasa hivi karibuni wameanza kukamata na magari madogo hasa saluni kwa madai ya kuwa ni taxi bubu.

Jana jioni yamenitokea mimi ambapo nilimpeleka rafiki yangu sehemu fulani nilipofika nikamwacha kwa minajili ya kumrudia baadaye. Nikiwa nataka kutoka, kijana mmoja mwenye radio call (kama polisi vile) akaniomba lifti nafika hapo... Nikakubali, punde akasema wewe unafanya biashara bila kibali "kwanini unafanya gari hii kuwa taxi bubu?"!

Mimi nilibaki kushangaa na kupigwa bumbuwazi?! Sikuelewa hiyo biashara nimeifanya lini na nani? Rafiki yangu nilipomshusha, hatukupeana kitu chochote (ambacho kingemshawishi kuwa labda amenilipa chochote:. kama kawaida ya Dar, watu waliisha kusanyika!! nini? nini?...nini?. Tulizozana sana. Nikimweleza kuwa yule siyo mteja, ni rafiki yangu. Hakuelewa. Mwenzangu akaita breakdown haraka gari ikachukuliwa mwenge.

Nilikaa hapo mpaka usiku ambapo nililazimika kulipa 20,000. Ndipo gari ikatoka. Inawezekana kuna na wengine hali hii imeishawahi kuwatokea.

Swali gumu kwangu ni Hawa Majembe ni mali ya nani? Nguvu ya kuwanyanyasa wananchi wanaipoata wapi? Nani ana data zaidi atujuze??

Karibuni
 
Back
Top Bottom