Majawabu ya Kigwangalla: Tunawezaje Kuleta Usawa Kwenye Ubora wa Elimu Yetu?

Kitu kikubwa kinachoniudhi kuhusu huyu Dr. Kingwangala ni kuwa anajifanya kama yeye ni outsider, wakati yeye ni mbunge wa chama tawala. Ni chama chake ndicho kinachoandaa bajeti na kusimamia policy mbali mbali. Sasa kama kweli anataka kuwasaidia Wananchi aingie jikoni na kupambana na wenzake kwenye kamati mbali mbali. Na sio kuuliza maswali basic ambayo hata mtoto wa darasa la saba anaweza kuuliza...
Rufiji (kwa ndg yangu Hamisi Mrufiji, mimi ni Hamisi Mtabora), naomba nifafanue kitu kuhusu checks and balances za mihimili ya dola kwenye system ya Westminster. Mimi ni mbunge na kazi zangu kikatiba ni legislative, overseer and advisory role, na representation role. si zaidi ya hizo. Kuna ambao wametoka kwenye hizi role tatu na wameingia kwenye role za executive (ministers) na hawa wanasaidiwa na watendaji mbali mbali ambao aidha wameteuliwa na Rais ama wameajiriwa. muhimili wa tatu (judiciary) una-consume legislatures ambazo sisi tunazitunga, kwa kuzitafsiri na kuzitumia. Sasa unapata wapi dhana ya kuniona mimi ni miongoni mwa serikali, unless kama wewe mbunge haujui kazi yako! Mimi nashukuru Mungu naijua vizuri kazi yangu na wala sitetereki kwenye hilo.
 
Mkuu Kingwala hii ni idea niliwai kuwea weye juwa alatenoojia uhusiana na Elimu.. Nini tufanye
Mara nyingi tukiongelea vikwazo kwenye sekta ya ICT serikali imeonekana ni kikwazo katika mambo mengi.

Wakati nakubaliana kuna mambo serikali inatakiwa kuyaweka sawa bado kuna wataalam wengi kwa nafasi taasisi , majukumu au uwezo wa maamuzi waliyonayo wanaweza kyafanya na kuifanya ICT kuyoa mchango.

Nitatoela mfano taasisi au maaumizi mabali mabli ambayo hayahitaji gharama kubwa na yana mchango wa kuleta mabadilliko endelevu.

I Elimu

Hili Nimeliandika sana hapa. Kuna shule hazina maabara,kama maabara ziipo basi hazina vifaaa . kuna shule hazina waalimu wa sayansi . ICTina toa fursa za kufukia mapungufu haya
How?
Ni kiasi cha wizira au Idara, NGO au Mbunge au hata shule binafsi au hata mtu binafsi anayejihusiha na elimu kutafuta mwalimu mzuri wa somo fulani na watalmu wa kurekodi video, Kurekodi video akifunidisha au akifanya practical ya somo fulani. Then kutoa kuuza copi ya DVD kwa shule na wanafunzi. Shule zitahitajika kununa TV na DVD player kwa ajili hii. Naamini shule nyingi zinavyo hivi vifaa . One time cost inafanya kazi kwa miaka kadhaa. Wanafuzi na wazazi wanatkiwa kujua video sio lazima iwe ya kanumba . Waleweshwe unaweza kutazama video ya Laws of motion of balancing chemical equation.
Faida zake nini

  • Tatizo la maabara litakuwa limekiwisha na hakuna ulazima shule kuwa na maabarabadla yake wanaweza kuwa video room ya wanafuzi kuona kila practical inafanyikaje. kama shule haina mwalim au zile topic ngumu practical. One time cost. na hivyo ufanisi na matoek ya mwnaafunzi kuboreka.



  • kwa mwanafuzi itasaidia akiwa nyumbani anaweza kuona zaidi ya video ya anumba. anaweza kuona video ya lawas of motion.zaidi kuelew kama hakuelewa mwalimu darsani. mwnafuzi kuuliza maswali na kuongeza ubora wa elimu.

Wito
Tuwaombe wabunge tunaowajua na tuwashawishi watumie japo kias fulani cha pesa za mfuko wa jimbo kufanya kitu hiki. Mbunge atakeyajribu kufanya hivi ataona serikali inaiga siku si nyingi. Binafis najua hili linawezekana lakini sina uwezo wa kuorangise resources, na sina access ya kuwapa idea hii wale wenye uwezo wa kufanya maamuzi. So tusaidiane.

Nawaombeni muwaambie waheshimiwa vijana wenzetu kina myika, zitto,january makamba, etc. Na hata kina Mbowe , Dr slaa prof lipumba mawaziri na maktibu wa jk waje wasome uzi huu kama wataona yanafaa wayafanyie kazi .. kama watataka maelezo zaidi tutawafamisha na kueleza option zilizopo kwa upana zaidi


NB.
Nitaendela kutaja opportunities za iCT zinazoweza kufanyika kwenye sekta au tasisi mbali mbali. kutatua matatizo .​

Last edited by Mtazamaji; 8th April 2011 at 02:01.​

Ukioata muda aribu kusoma
https://www.jamiiforums.com/tech-ga...mia-ict-kutatua-matatizo-halisi-ya-jamii.html
 
Tuiendea kwenye eimu mja ya comment katika uzi huu

Serikali ngazi ya wilaya na Mkoa zinatakiwa kuazisha ofisi au vituo vya ICT zilizounganishwa na internet . kwa jina la kitaalamu Computing Center. Ofisi hizi na ofisa wa ofisi hii atawasaidia watumishi mbali mbali kupata curent na latest information kuhusu mambo mbali mbali. Zitawanufaisha walimu kudownload kuhusu mada mbali mbali ambazo shule zao zimekosa vitabu vya kiada juu ya jambo fulani. Vituo hivi vitawanufaisha wafanyakazi wa sekta za afya, wahandisi , maofisa kilimo.Wafanyabiashara na hata wanafuzni

Ninachomaanisha hapa Serrikali ngazi ya wialya na Mkoa zinatakuwa kuwa na kitu nachoweza kusema ni "Internet-cafe"

Tayari kuna mikoa ina maktaba ambazo hazina vitabu vinavyokwenda na wakati. Serikali kwa kutumia fursa ya ICT inaweza kubadlisha sehemu za maktaba hizi kuwa computing center inayowajibika kuwapatia na kuwatafutia watu taarifa fulani.

Fursa nyingine seikali kwa.kutumia gharama ndogokwa vitabu vya makataba inaweza kujiandikisha kwenye taasisi mbali mbali zenye maktaba ya vitabu/ video online. usumbufu wa vitabu kupotea u kubiwa maktaba utaondoka na vile vile kutazifanya maktaba zetu kwenda na wakati .kwa kuongea na taasisi kama ACM Online Books and Courses na nyingine kama hii kunaweza kufufua makataba zetu .

NB
Mawazo kama haya inabidi watu waliojairiwa ofisi za mikoa kama watalaama wa ICT wawape wakubwa. Tusiwalaumu wakubwa wakati sisi hatuwi creative. Usimlamu mkubwa wakati hujawai kushika kalamu na kuandika ushauri wowote akaukataa.

Binasfsi nashangaa kwa serikali mpaka leo haina nafasi/Vyeo vya maafisa ICT wa Mkoa na wilaya kama tuivyo na vyeo na jaukumu ya waganga wakuu, Afisa Kilimo, Mifugo . Huu mkonga hautaleeta faida kwenye huma kama Umuhimu TEKNOHAma unaongelewa kisiasa tu.

Hope Mkuu kingwala ukiona yapo yanayofaa unawez kupaza sauti. au tunaweza kuyafafanua kitaalama zaidi ikibidi.
 
Mh. Kigwangalla i don't see the logic from this paragraph, unaweza kutueleza ulikuwa unamaanisha nini hadi wakakupigia makofi. Kwani kupewa motisha walimu wanaofanya kazi katika mazingira magumu ndiyo kupunguza tofauti kati ya walionacho na wasionacho? I don't think so Mh. hapa mlikuwa mnapitisha muda tu ili posho iingie. Kwenye hii paragraph ulikuwa unawazungumzia zaidi walimu na si wananfunzi, sasa basi unataka kutuambia walimu walionacho na wasionacho wanapatikana kutokana na jiografia ya nchi...hapana mheshimiwa.
ukiangalia mchango wangu juu juu utasema nilikuwa nawaangalia walimu (kwa bahati mbaya sana umeenda mbele na kusema walimu walionacho na wasionacho, hicho sikukilenga hapa!) kumbe unasahau kwamba bila walimu kwenye sekondari literaly hakuna elimu hapo! Mimi nilimaanisha kwamba tutengeneze system ya kuyatathmini maeneo kutokana na sababu za kijiografia na tuyape alama maalum kwa vigezo hivyo ambavyo vitakuwa pre-determined, kisha walimu watapangwa na kuwa appropriated compensated kutokana na sababu hizi za kijiographia, kwamba wa mbali (remote) zaidi atapewa posho kubwa zaidi ukilinganisha na yule wa karibu zaidi na center. Hii itatufanya tuwa-retain walimu wazuri na wengi kwenye shule ambazo ziko kwenye maeneo yenye disadvantage kijiografia na hapo indirectly tutakuwa tumeinua ufaulu wa wanafunzi wa kwenye shule za remote areas(vijijini). assumption hapa ni kwamba, wanafunzi wanaosomea shule za vijijini na kadri unavyozidi kuingia ndani zaidi ndipo idadi ya walimu inapungua kwa sababu ya ukosekanaji wa huduma na umbali na ama ukosefu wa miundombinu, hivyo walimu wa kule wana high propensity ya kutoroka ama kuhama vituoa vya kazi na hata kuacha kazi serikalini kabisa. Maana kunakuwa hakuna sababu ya mwl kufanya kazi kijijini Sakasaka wakati angeweza kuhonga ama ku-lobby na akapangiwa Shinyanga mjini!

Mpango huu ukifanikiwa na tukawa na equal distribution ya walimu tutajikuta sasa tunatakiwa tuanzishe performance based paying system (pay4performance scheme) ili ku-reward wale watakaoenda an extra mile na kufanya vizuri kuliko wengine. hizi zote ni incentive schemes ambazo zingeleta tija na ufanisi wa hali ya juu kwenye systems zetu. Na systems hizi zinaweza kutumika kwenye Afya pia na huduma ungeona zinakuwa bora zaidi ya zilivyo sasa.
 
Mh Mbunge, nilipoona hii title na kuwa imatumwa na wewe, niliacha shughuli zangu na kuifungua haraka sana. Sababu ni kwamba mimi nina shauku sana ya kupata jukwaa litakalojadili hili suala 'kisayansi'. Pamoja na nia yako nzuri ya kuuleta huu mjadala, lakini preamble uliyotoa hata haihamasishi. Can you please carry a litle research and come up with a touching data enriched introduction?
...Tuko,

...Nadhani Mhe. ametu engage kwenye mada nzuri. Hebu tuijadili. Data haziwezi kutukwamisha tuijadili, ukizingatia kwamba wapo wenye data kuliko hata Mhe. humu na nyingine zimejaa mtandaoni.

...Narudi kwako Mhe. Kigwangala kwa mchango wa swali lenye kuzaa mjadala zaidi. Je, tuna standards zozote zinazoainisha aina za shule na vigezo vyake, hasa hizi za msingi?. Maana kwenye elimu ya juu, vigezo hivi hutumika kutambua kama shule husika zinafaa kutoa elimu au la.

...Je, kwanini tusiwe na minimal requirements katika kuhakiki na kukubali shule za msingi kuitwa hivyo. Kama vigezo hivi vipo, kwanini havitumiki.

...Maana habari ni nyingi mno kuhusu shule zenye mwalimu mmoja, dawati kumi, bila choo, n.k. Hizi nazo zinakidhi viwango vya shule? kama la, kwanini zinatambulika kama shule?
 
kati ya walio nacho na wasio nacho, na pia ili kuondoa uwezekano wa kuunda matabaka ya watumwa na watawala kwa kuruhusu uwepo wa kundi la watu wenye elimu bora na la wale wasio na elimu kabisa. Hii inatokana na uwepo wa shule za sekondari za kata zenye ubora huu wa elimu tunaoufahamu, ambazo wanasoma watoto wa pangu pakavu na uwepo wa private schools wanazosoma watoto wa wenyenacho. (Makofi)
...Kama hamna standards -kuanzia kwenye ujenzi, vifaa, walimu na vingine- zinazosimamiwa katika utoaji elimu -na hili tatizo liko zaidi katika elimu ya chini-, hata walimu wakipewa motisha wa namna gani, haitasaidia. Kwanza, huko vijijini ndio watakufa kwa ulevi na watawekeza zaidi kwenye kilimo na kusahau hata kufundisha, maana hamna vigezo vya kufuata na havikaguliwi.

...Mhe. tatizo liko kwenye mfumo mzima wa elimu. Haina mwenyewe!
 
HUU NI MMOJA WA MICHANGO YANGU KWENYE BAJETI YA ELIMU MWAKA JANA WAKATI BUNGE LIMEKAA KAMA KAMATI.




MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla!


MHE. DKT. HAMISI A. KIGWANGALLA: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ahsante kwa kunipa fursa hii.


Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mchango wangu wa maandishi niliongelea kwa kirefu
kuhusu jitihada za Serikali katika ku-foster equity kwenye utoaji wa elimu nchini ili kupunguza gap
kati ya walio nacho na wasio nacho, na pia ili kuondoa uwezekano wa kuunda matabaka ya watumwa
na watawala kwa kuruhusu uwepo wa kundi la watu wenye elimu bora na la wale wasio na elimu kabisa.
Hii inatokana na uwepo wa shule za sekondari za kata zenye ubora huu wa elimu tunaoufahamu, ambazo
wanasoma watoto wa pangu pakavu na uwepo wa private schools wanazosoma watoto wa wenyenacho. (Makofi)


Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nimependekeza na kutoa ushauri kwa Serikali ili kuweza kupunguza

tofauti iliyopo kati ya walio nacho na wasio nacho ni lazima walimu ambao wanafanya kazi katika mazingira
magumu wapewe motisha maalum ambazo zinaweza zikawa calculated kijiografia au kwa vigezo vingine ambavyo
vinatokana na tafiti mbalimbali. (Makofi)


Je, Serikali imejipanga vipi katika kutoa motisha kwa walimu wanaoishi katika
mazingira magumu ikiwa ni pamoja na nyumba, mikopo ya vyombo vya usafiri na posho
za hardship katika kazi zao. Ahsante.

Hoja duni kama hii hata mtoto wa darasa la 6 angeweza kutoa. Hamna any semblance of objectivity kama takwimu, case studies au utafiti unaokubalika zaidi ya maoni yako binafsi. Wewe kuweka humu pumba kama hii inaashiria jinsi unavyohusudu "misifa" na tabia yako ya kujifagilia (makofi). To put it bluntly, it looks like you have an ego problem, dude.
 
kaka
kama kweli serikali ingekuwa inatoa kipaumbele kwa walimu wanaofanya kazi ktk mazingira magumu,basi mimi nisingesoma engineering tena,
kwani nina diploma ya ualimu niliyopata ktk chuo cha ualimu dar es salaam(DTC) na niliajiliwa na kufanya kazi malinyi ulanga kipingo sekondari kama mwalimu wa fizikia na hisabati,ki ukweli mazingira yale kutoka

Ifakara-Lupiro-idete-kipenyo-mtimbra-malinyi

kufika huko tena kwa kipindi cha masika ni issue kubwa sana,mazingira ni magumu na inataka moyo sana,ila huwezi amini kidume nilipiga kazi miaka miwili na nusu na baada ya hapo nikaona ni bora ni umie kwa engineering lakini mwisho wa siku nitafaidi na ni kweli saizi naona faida ya kubadili fani

mazingira yale huwezi kufananisha na mtu anaefundisha DSM ama MOROGORO mjini.


Lakini pia nimefanya kazi chilonwa(kama mnakumuka i am taking this girl to the hospital,if polisi come tell them chonya of chilonwa me)

yale mazingira ni tabu kuanzia usafiri hadi maji,usiku kuna kimlima unasikia fisi wanalia,ukirudi kazini huna pa kwenda wala cha kufanya zaidi ya kusahihisha ama kulima ufuta kipindi cha masika.

namshukuru mungu siko huko tena na sitaki rudi tena,maana walimu wenzako wa mjini walikuwa na vitu vingi kimaisha ukifananisha na mimi
Sasa mchango wako hapa ndio upi hapa maana umeeleza profile yako tu ambayo sidhani kama inatusaidia sisi.
 
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nimependekeza na kutoa ushauri kwa Serikali ili kuweza kupunguza

tofauti iliyopo kati ya walio nacho na wasio nacho ni lazima walimu ambao wanafanya kazi katika mazingira
magumu wapewe motisha maalum ambazo zinaweza zikawa calculated kijiografia au kwa vigezo vingine ambavyo
vinatokana na tafiti mbalimbali. (Makofi)


Je, Serikali imejipanga vipi katika kutoa motisha kwa walimu wanaoishi katika
mazingira magumu ikiwa ni pamoja na nyumba, mikopo ya vyombo vya usafiri na posho
za hardship katika kazi zao. Ahsante.
Ulikuwa unauliza au unatoa ushauri?
Kwa mfano taifiti gani ziliongelea malipo kutokana na ugumu wa mazingira? Ungezitaja na kuelezea mifano ya maeneo yenye mazingira magumu.
Mikoa yote ambayo ipo mbele kielimu, ni wananchi wenyewe ndiyo waliojitolea kujenga shule na nyumba za walimu.
Kwa sasa hivi, magari utakuwa unacomplicate issues... si lazima.
 
ukiangalia mchango wangu juu juu utasema nilikuwa nawaangalia walimu (kwa bahati mbaya sana umeenda mbele na kusema walimu walionacho na wasionacho, hicho sikukilenga hapa!) kumbe unasahau kwamba bila walimu kwenye sekondari literaly hakuna elimu hapo! Mimi nilimaanisha kwamba tutengeneze system ya kuyatathmini maeneo kutokana na sababu za kijiografia na tuyape alama maalum kwa vigezo hivyo ambavyo vitakuwa pre-determined, kisha walimu watapangwa na kuwa appropriated compensated kutokana na sababu hizi za kijiographia, kwamba wa mbali (remote) zaidi atapewa posho kubwa zaidi ukilinganisha na yule wa karibu zaidi na center. Hii itatufanya tuwa-retain walimu wazuri na wengi kwenye shule ambazo ziko kwenye maeneo yenye disadvantage kijiografia na hapo indirectly tutakuwa tumeinua ufaulu wa wanafunzi wa kwenye shule za remote areas(vijijini). assumption hapa ni kwamba, wanafunzi wanaosomea shule za vijijini na kadri unavyozidi kuingia ndani zaidi ndipo idadi ya walimu inapungua kwa sababu ya ukosekanaji wa huduma na umbali na ama ukosefu wa miundombinu, hivyo walimu wa kule wana high propensity ya kutoroka ama kuhama vituoa vya kazi na hata kuacha kazi serikalini kabisa. Maana kunakuwa hakuna sababu ya mwl kufanya kazi kijijini Sakasaka wakati angeweza kuhonga ama ku-lobby na akapangiwa Shinyanga mjini!

Mpango huu ukifanikiwa na tukawa na equal distribution ya walimu tutajikuta sasa tunatakiwa tuanzishe performance based paying system (pay4performance scheme) ili ku-reward wale watakaoenda an extra mile na kufanya vizuri kuliko wengine. hizi zote ni incentive schemes ambazo zingeleta tija na ufanisi wa hali ya juu kwenye systems zetu. Na systems hizi zinaweza kutumika kwenye Afya pia na huduma ungeona zinakuwa bora zaidi ya zilivyo sasa.
Asante Mh. Kigwangalla mimi sipingani na mawazo yako ingawa huja produce kitu kipya kwa vile ni yale yale yamekuwa yakiongelewa miaka nenda miaka rudi kuhusu kuboresha maisha ya walimu na elimu kwa ujumla. Nilichokuwa napinga ni presentation yako ya ile pragraph ilikuwa haijengi logic yeyote hadi ukapigiwa makofi kusema: kuwapa motisha walimu wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu ni kupunguza gap la walonacho na wasionacho, how? ina maana unataka kum define huyo mwalimu anayefanya kazi kwenye mazingira magumu ndiye asiyenacho? sidhani kama hiyo ndiyo maana ya asiyenacho.

Anyways, turudi sasa kwenye mada, system ya elimu yetu ni ya mapokeo ya kikoloni hatujaweza kujiundia system yetu tunayoimudu na sidhani kama kwa siku za karibuni tutaweza. Elimu yetu inategemea end-product tunachoangalia ni wangapi wame pass hatuangalii wangapi wamebaki (failures + dropouts). Kama kweli tunataka ku-foster equit kusaidia kupunguza gap la wasionacho na walionacho ni kuwasaidia hawa wanaobaki, kwa sababu wengi wa wanaobaki ndio kweli wasionacho, vinginevyo tutakuwa tutawajaza watoto mashuleni na baada ya kumaliza shule tunawaacha mitaani.

Mimi nafikiri Mh. Kigwangalla cha kufanya, badala ya wewe na wenzako kukakaa kwenye semina na kuzungumza yale yale wenzenu waliyo suggest zamani na pengine kufanyia utafiti, mngesema sasa tuanze na hiki. Ndio maana nikashangaa sana wenzako kukupigia makofi kana kwamba umeleta idea mpya kumbe ulikuwa unakariri mawazo na tafiti za wenzako.
 
Hapa sasa umejadili kisomi na mjadala unazidi kuwa mtamu na hii ndo ile maana ya JF kuwa jukwaa la great thinkerz. Hebu elezea vizuri jinsi unavyotaka kuhusisha Elimu na Ushirika: unamaanisha ushirika upi?

Swali la msingi Chikakatata
1. Ushirika tusiufunge kwa consumer and producer modals peke yake mkuu consider CBHI and CBHF kwa mfano hii ni mifuko ya afya inayotakiwa ku operate at a local level kwa michango ya wananchi sehemu husika kwa kiwango kinachokubalika na wote na kiwe significant. Kwa sekta ya elimu hususan shule za kata kama zitajuwa chini ya Co-operatives ukiongeza na ruzuku na ada ya wanafunzi hizi shule zinakuwa na wenyewe tayari (sense of ownership) hapo ndugu ubadhilifu huu tunaouna katika shule za kata kuanzia kwenye majengo utapungua sana tu mkuu. Hebu tufikirie beyond kwamba Co-op zaweza kwenda mbali zaid ya kuwa na duka.....it is possible

Add; Wakulima pesa zao ni za msimu na ni vigumu ku systematize matumizi yao kuliko muajiriwa so wakati wa mavuno ni wakati mzuri wa kupitisha michango yao kwa kupitia vyama vyao (in cash or crops terms) hata ada yaweza pia kulipwa kipindi hiki kuondoa usumbufu.....we need the system of our own which is context sensitive

Challenge; Is to have an adequate management on funds collected but mind you there are no angels to work for us and thus we need to design and establish systems, checks and balances so as to fulfil the set objectives

Advantage; The effectiveness and sustainability of these schools and education programmes is more expected when you get owners (community members) to be part of the development machinery

Capital; Wananchi kwa hivi tuna njaa ya maendeleo na tuko tayari kuvuka kipande hiki cha mkwamo so it is up to considerate leaders to invest on this willingness.....development can easily be processed when the concerned knows their problems and are exposed to the fact that if they do not act the status will remain quo NA HII NDIO ROHO NA SIRI KUU YA USHIRIKA


Wa hadha assalaam..................changanya na za kwako!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom