Majambazi yaua segerea

elimukwanza

Senior Member
Dec 27, 2010
168
23
LEO jioni kwenye mida ya saa 12 pale segerea kituo cha sanene majambazi mawili yakiwa na pikipiki yamevamia duka la kuuza vocha la jumla na kumpiga risasi kichwani muuzaji na kumuua papohapo.

Inasemekana majambazi hayo yalifika mapema na kuelekea saloon iliyopo karibu na duka hilo huku yakitegea muuzaji afunge duka mara yakamuwahi akifunga na kumuelekezea bastola kichwani yakimwambia toa fedha, aliposema hana papo hapo yakamuua.

Imesikitisha sana watu wamefunga biashara zao n wanaomboleza MUNGU AMLAZE MAHALI PEMA MAREHEMU AMIN.
 
inasikitisha sana. yote hii ni kwa sababu ya utofauti wa kipatao.

Wadau nipo nchi ambayo mfagizi halipwi tofuati sana na mkufunzi wa chuo hii ni kutaka kila mwananchi aishi maisha mazuri hata sisi wageni tunaheshimika pia na watoto.

Nina mda mrefu sijawahi silkia kuna wizi umetokea mahali au ujambazi hata kulala usiku hata usipofunga mlango hakuna woga.

Tanzania bila kuwa na mfumo unaojali maisha ya wananchi wake, ufisadi ukakoma, maisha yakaboreshwa kwa kuongeza pato la nchi , uwezo tunao tuna rasilimali nyingi tu kama madini na gesi mpya iliogunduliwa na ambayo huuzwa gali sana kama sio ufisadi na 10% uchumi ungekuwa,watu wangekuwa na vipato,umeme ukaboreshwa watu wakajiajiri zaidi wizi ungepungua.

Nawashauri hao majambazi wawaibie hao mafisadi papa na wahindi wanaoutibia kila siku wawaache ndugu zetu wanaojituma. Poleni sana wafiwa.Tuanhitaji mabadiliko ya utawala kukomesha hali hii.
 
Yamechukua chochote au yameua tu? Pole zao kwakweli. Inaonekana leo wameamua. Maana asubuhi tumesikia Mhimbili, saa hizi tena segerea? hii ni balaa mbaya sana.

Nchi ya amani hii according to CCM, watu wanauana hivyo hadharani kabisa bado hawa jamaa wanaendelea kujinadi eti ni nchi ya amani? Bado tuna safari ndefu kwakweli.
 
nina best wangu,mpiga box sweden,ana kiwanja segelea.bora tu aendelee kukaa huko stockholm,maana huku ni ushenzi tu
 
Aisee poleni mliofikwa na msiba, naona majambazi nao wako busy kutafuta "sitting allowance" zao..
 
bad news,it's due to kipato na serikali haina miundo mbinu ya detect uhalifu kama huo save for maandamano. R.I.P mpendwa.
 
pumzik akwa amani muuza vocha wangu na bwana akuangazie mwanga wa milele
 
Haaa jamani majambazi yamerudi tena kwa kasi ya kupaa maskini muuzaji wa wt, na nyie majambazi kwanini mtumie silaha za motooo! af ukute hela yenyewe mliyoiba mmegawana laki 3 af mmetoa roho ya mtu looool shame on you! najua humu pia majambazi yamo
 
hawa majambazi mara chache kufanya mauaji hasa maeneo ya mafisadi...huko ndiko kunaimarishwa ulinzi wa kufa mtu that's y mafisadi hayaamin kama hayo hutokea.
Ila ingekua yanafanyika mara kwa mara maeneo yao japo wangejali.

Ukienda polisi ya msimbaz ofisin kwa ocd utaona maeneo ya matajiri na mafisad yamechorwa...nahis likitokea tatizo itaulizwa ''hapo ni sehem gan?''

Kama si kweli hizo raman kuonesha watu matajir za nin? Sijui na vituo vinginevyo?
 
naona sasa mbinu ya pikipiki imegunduliwa au ndio hayo hayo? maana siku moja matukio mawili na kote wameua na wametumia pikipiki
 
Tanzania ya leo.... Inasikitisha sijui tunaenda wapi....
May the deceased R. I. P
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom