Majambazi yatikisa Dar, Yapora milioni 46/- bila upinzani

May 8, 2013
40
6
Majambazi yatikisa Dar
• Yapora milioni 46/- bila upinzani


na Abdallah Khamis




WATU wanaoaminika kuwa ni majambazi ambao idadi yao haijafahamika, wamepora sh milioni 46, huku polisi wakishuhudia bila kutoa upinzani kukabiliana nao.

Fedha zilizoporwa ni mali ya mfanyabiashara wa bia za jumla jijini Dar es Salaam, Ivon Urio, wa wilayani Temeke.

Wakati majambazi wa Temeke wakipora kiasi hicho bila upinzani, tukio lingine la ujambazi limetokea jana asubuhi katika mtaa wa Sayansi na Kijitonyama wilayani Kinondoni ambapo walipora sh milioni 40, majira ya saa nne asubuhi.

Katika tukio la ujambazi la Temeke ambalo linadaiwa kuwa la nane kwa mwezi huu, lilitokea juzi kati ya saa nne na tano asubuhi katika eneo la Mbagala Rangi Tatu, wakati mfanyabiashara huyo akijiandaa kupeleka fedha hizo benki.

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo kabla ya majambazi hao kupora fedha hizo, polisi wanaokadiriwa kufikia 10, walifika eneo hilo wakiwa wanalifuatilia gari lililokuwa linashusha mafuta ya kula katika moja ya maduka yaliyo jirani na eneo palipotokea wizi huo.

Mmoja wa mashuhuda hao, Humphrey Mwakalinga, aliiambia Tanzania Daima kuwa walianza kutilia shaka mienendo ya baadhi ya watu katika eneo hilo na kupeana taarifa ya kuchukua tahadhari.

Humphrey alisema wakati wanahimizana kuchukua tahadhari hiyo, walimuona mmoja wa watu waliowatilia shaka akizungumza kwa simu na muda huohuo gari la mfanyabiashara huyo wa bia likavamiwa.

“Kulikuwa na askari wapatao 10 ambao walikuwa wamekuja kwa ajili ya gari lililokuwa linashusha mafuta, tukawaambia waangalie watu wanapora na muda huo ndio tukio linatokea lakini hawakufanya lolote; walikuwa kama hawaoni tukio hilo,” alisema Mwakalinga.

Alisema hata baada ya majambazi hao kuondoka kwa pikipiki, walibaki majambazi wengine wakiwa na bastola na raia wakawa wanawaambia askari wakawadhibiti pasipo askari hao kuitikia wito huo wa raia.

“Kama kwenye tukio la mafuta waliweza kuja kwa wingi halafu ujambazi unatokea mbele yao na hawafanyi jitihada kudhibiti, sisi wananchi lazima tuwatilie mashaka polisi,” alisema raia mmoja ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke Englibert Kiondo alipoulizwa juu ya tukio hilo alikiri kutokea huku akikanusha askari kuwa karibu na tukio hilo.

Alipoelezwa sehemu waliyokuwa askari na tukio lilipotokea kuwa halizidi mita 20, Kiondo alisema askari hawakuwa katika maandalizi ya kupambana na majambazi.

“Muhimu ni kwamba kwa sasa tunawashikilia majambazi wawili na silaha moja huku tukiendelea kuwatafuta wale waliokimbia na fedha; hili la kuniambia askari walikuwa eneo la tukio bila msaada ni kwa sababu hawakuwa na maandalizi ya kupambana na majambazi wakati huo, walikuwa pale kwa kazi nyingine,” alisema Kiondo.

Tukio la ujambazi la eneo la Kijitonyama, wilayani Kinondoni, lilitokea jana, baada ya majambazi hayo kumfyatulia risasi dereva wa gari aliyekuwa akisubiri taa za barabarani ziruhusu.

“Majambazi hayo yalikuwa kama manne hivi, yalikuwa yamepanda pikipiki mbili tofauti, ghafla yakasimama na kulizunguka gari aina Vitz lenye usajili wa namba T929 CCX kwa haraka, mmoja wao akiwa na ‘mashine gun’ na wengine bastola,” alieleza shuhuda huyo.

Shuhuda huyo alieleza kuwa watu hao walifyatua risasi hewani na kumtaka dereva asimame na ashushe vioo vya gari yake, lakini alikaidi ndipo wakalifyatulia risasi kadhaa gari hilo upande wa dereva na kumjeruhi begani dereva huyo.

Baada ya shambulizi hilo, majambazi hayo yaliondoka na begi linalosadikiwa kuwa lilikuwa na sh milioni 40.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, aliahidi kulizungumzia zaidi tukio hilo leo.
 
Hatuna jeshi la polisi hapa kama utaratibu wenyewe ndo huu wa kujiandaa kwanza kwenda kupambana na majambazi utadhani huwa yanatoa taarifa kama yanaenda kuiba,hakuna maana ya jeshi la polisi kuwepo
 
Polisi ni mpaka wapewe hela na wakati mwingine mpaka wawe na taarifa ya msamaria mwema ndo utasikia majambazi 6 wameuwawa baada ya kurushiana risasi na hakuna polisi aliyejeruhiwa, wakati wamewavizia na kuwaua wote kwa mstukizo.
 
Na support 100% jeshi la polisi kuwa chini yaJWTZ!hìi imezidi hapo kwenye mafuta tena ya kula itakua wameusindikiza mzigo toka mbweni hapo walikua wanasubiri mshiko tuu!yani yale ma defender wanayatumia kukusanya rushwa tuu
 
huyo RPC kachemuka! Huo ni mchongo anaujua!! Tanzania yetu ni kujirinda mwenyewe!
 
Duuuh huu mwezi tangu uanze sijui hii ni story ya ngapi ya ujambazi...majambaz nayo yashapima na kujua kuwa polisi hawana mda nao..zaidI ya kuwa na mda na maandamano
 
Hao ndio Polisi wa Tanzania bhanaaa...kuna uwezekano hao waliokuwepo eneo la tukio walikua ni wale polisi wenye vitambi vikubwaaaa...
 
Mambo yameanza tena taratibu, si unajua 2015 inakaribia? Aliyewekwa na shemeji nao muda wake wa kazi unakaribia mwisho, 60 years!!! Kova naye sijui!!! Kwa hiyi kila rangi itaonekana!!! Tanzania tunusuru Mungu wetu.
 
Hivi hizo 46 M, ni mauzo ya siku moja tu?

Mkuu kwa duka la jumla la bia hizo ni kidogo sana. Pale Riverside kwa wale wa Dar ni zaidi ya hapo. Imagine kama unauza bia watu wa bara wanafika kununua kwako na wale wa sherehe za jumla. Crate say 20 kwa mnunuzi mmoja ni shilingi ngapi? Imagine kwa siku una wateja kama kumi na wao wanachukua over 20 crates of beer!!!! Pesa kubwa japo faida inakuwa si kubwa sana. Kwa hiyo 46m kwa bia za jumla ni ndogo sana. Sema kule ni mbagala ila maduka ya jumla ya beer mitaa mingine say kama kinondoni na Ilala ambako ---- michanganyiko ya watu na wanywaji wengi ni over that my friend.
 


hawakuwa na silaha za moto! ... ulitaka wafanye nini..?
Hapo ndio kuna tofauti ya askari na raia wa kawaida

kuna mbinu za kumkabili adui hata kama umeishiwa risasi

kuna kufuatilia gari maana hata wao walikuwa na gari

kuna kuwasiliana kwa radio na wenzao ili kuweka vizuizi na kukamata wahusika


hata kupiga filimbi ni mbinu
 
Hapo ndio kuna tofauti ya askari na raia wa kawaida

kuna mbinu za kumkabili adui hata kama umeishiwa risasi

kuna kufuatilia gari maana hata wao walikuwa na gari

kuna kuwasiliana kwa radio na wenzao ili kuweka vizuizi na kukamata wahusika


hata kupiga filimbi ni mbinu


jeshi la polisi lina vikosi vingi mno! huwezi jua kikosi kilicho kwenda pale ni kuhusu mafuta obvious walijitayarisha na paper work and ofcoz lazima waliwasiliana na kituo kilicho karibu ... angalia FACT weka siasa pembeni ... sina silaha ya moto wataka nikabiliane na jambazi.. least i can do ni kutoa taarifa

 
Mpaka wajirembe kwanza wapige kwata ndio wawe tayari kukabiliana na Majambazi, lakini cha kushangaza wangekuwa wameyaona maandamano ya CHADEMA basi wangechakarika katika speed ya ajabu na virungu vyao na hata silaha za moto na kuomba nguvu zaidi za "kukabiliana na adui."

Hivi kumbe askari kukabiliana na tukio mpaka wajipodoe kwanza...only in danganyika
 
Back
Top Bottom