Majambazi yapora PESA Muhimbili National Hosp

Wabongo bwana! wameshawahukumu wahasibu masikini ya Mungu! Ndo maana nchi haiendelei kila kitu tunafanya kwa hisia tu bila evidence yoyote, ovyo kweli. As is kuwepo kwa pesa ni some sort of Top Secret.
 
hakuna askari hapo na swai ndo alileta kampuni hiyo kwa kueleza kuwa walinzi waliokuwa wanamilikiwa na muhimbili hawawezi kazi .kwa bahati nzuri japo walikuwa hawawezi kazi hakuna uwizi wa style hii uliwahi kutokea.......kama mimi binafsi siwezi kuajiri walinzi wa makampuni kama haya kwani mishahara yao ni kichekesho afu wanalinda mamilioni ya pesa au vitu vyenye thamani mara trioni ya mishahara hivyo kuchonga deal kama hilo ni kawaida sana sana tu ila namsikitikia kama walimshirikisha afu wamemuua maana majambazi hawana dhamana hasa wakifanikisha azma
 
kingine hao walinzi sijui kama wanajua kama kweli nini wanalinda magetini kwani nakumbuka siku moja nimekwenda kumuona mgonjwa wangu kipindi hicho ndo walikuwa wameanza kazi walikuwa wanawazuia hata madaktari waliokuwa hawana vitambulisho magetini .......nakumbuka dactari mmoja akawa anawatukana akampigia mkurugenzi wa ulinzi muhimbili akawa anamuuliza sasa hawa ndugu mliowaweka hapa kama sina kitambulisho nirudi nyumbani kwa nini kabla ya kuwakabidhi hii kazi wasifanye na wenyeji??????????????
 
kingine hao walinzi sijui kama wanajua kama kweli nini wanalinda magetini kwani nakumbuka siku moja nimekwenda kumuona mgonjwa wangu kipindi hicho ndo walikuwa wameanza kazi walikuwa wanawazuia hata madaktari waliokuwa hawana vitambulisho magetini .......nakumbuka dactari mmoja akawa anawatukana akampigia mkurugenzi wa ulinzi muhimbili akawa anamuuliza sasa hawa ndugu mliowaweka hapa kama sina kitambulisho nirudi nyumbani kwa nini kabla ya kuwakabidhi hii kazi wasifanye na wenyeji??????????????

Ndo tatizo la wabongo! Security mnataka, security procedures hamtaki kufuata! Sasa kila mlinzi amkumbuke kila mfanyakazi wa muhimbili? si upuuzi huo, sytem ya vitambulisho ndo yenyewe. Matokeo yake ndo haya.
 
Wabongo bwana! wameshawahukumu wahasibu masikini ya Mungu! Ndo maana nchi haiendelei kila kitu tunafanya kwa hisia tu bila evidence yoyote, ovyo kweli. As is kuwepo kwa pesa ni some sort of Top Secret.

Mkuu wizi wa aina hii lazima kuna mtu anavujisha siri tuu. Jambazi hawezi panga tukio kama hilo bila kuwa na uhakika. Lazima anapwewa data zote; kuna sh ngapi, nani atabeba, ulinzi wake ukoje, msafara utakuwaje, nk nk.
Nilishawahi fanya kazi kwenye kampuni moja ambayo tulikuwa tunapeleka hela nyingi bank lakini kwa sababu ilikuwa ni siri ya watu watatu hatukuwahi kuvamiwa mpaka tulipoanza kutumia huduma ya cash in transit ya security group.

RIP marehemu, bahati mbaya hukujua kitu ulichotakiwa ufanye.
 
Breaking news ya Radio one ilikuwa hivi:

Majambazi yamemteka mhasibu wa muhimbili hosp na kuua mtu mmoja na kujeruhi mwingine kwa risasi kisha kutokomea na Mamilioni ya shilingi!

Ni kweli kuna mtu alitekwa na imekuwaje??
 
Ngoja tuwe wakali kidogo. Upuuzi wao ndo unawagharimu, hawana detailed examination ya kila kiingiacho na weakness hiyo imewagharimu!
 
WATU wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, leo asubuhi walivamia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam,wakampiga risasi na kumuua mlinzi wa hospitali hiyo, Juma Nagungu, kisha kupora fedha kiasi cha zaidi ya Sh milioni 12.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Hospitali hiyo, Aminiel Eligaesha tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili asubuhi jirani na eneo la mapokezi na kusababisha hofu kwa watu mbalimbali wakiwemo wagonjwa, kufuatia risasi zilizofyatuliwa na majambazi hao.

Eligaesha alisema, awali Nagungu na wafanyakazi wawili wanawake wa Idara ya Fedha hospitalini hapo, walikuwa wakizihamisha fedha hizo ambazo ni makusanyo ya siku za mwisho wa wiki kuanzia Ijumaa kutoka mapokezi kwenda idara ya uhasibu.

Amesema walipokaribia kufika huku wakiwa ndani ya gari aina ya Nissan lenye namba za usajili SU 36713, ghafla walishambuliwa kwa risasi ambayo mojawapo ilimpiga sehemu za mbavuni mlinzi na wao kuzipora fedha hizo zilizokuwa kwenye mkoba kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi waliokuwa wametoka kuzichukua kisha kutoweka nazo.

“Lengo ilikuwa wazikusanye fedha hizo na zingine zilizokuwamo ndani ya idara ya uhasibu ili wazipeleke benki kwa pamoja, lakini kwa bahati mbaya kabla hawajafika nazo tukio hilo likatokea,” amesema Eligaesha.

Kwa mujibu Eliegesha, mlinzi huyo alifariki dunia muda mfupi wakati wakimuwahisha kitengo cha dharura kwa ajili ya matibabu na kuongeza kuwa majambazi hao walikimbia kwa kutumia mlango wa kawaida wa kutokea magari.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Faustine Shilogile, alisema hakuna mtu anayeshikiliwa kufuatia tukio hilo huku upelelezi ukiendelea.

Alisema hadi Polisi wanafika katika eneo hilo majambazi hao walikuwa tayari wameshakimbia na bila kujua mahali walikoelekea.
 
Ndo tatizo la wabongo! Security mnataka, security procedures hamtaki kufuata! Sasa kila mlinzi amkumbuke kila mfanyakazi wa muhimbili? si upuuzi huo, sytem ya vitambulisho ndo yenyewe. Matokeo yake ndo haya. Kang nimefanya kazi ya ulinzi /nimeenda course fupi ya ulinzi DPSST(Department of public safety standards and training) kulinda ni kuzuia uhalifu sasa kama walihisi huyo dr. ni mtu hatari japo alijeleza vizuri sana kwa nini wasiwasiriane na wenzao wakaona nyendo za dr. zikoje huko ndani? mbinu za ulinzi kwanza unapaswa kuwa effective kutambua yupi mtu hatari na yupi si mtu hatari then unapunguza ukubwa wa kazi yako nani anatakiwa kuangaliwa muda wote na nani wa kumuangalia baada ya muda flani kwa mfano ma bodyguards wa viongozi ulaya na usa wapo makini sana na ulinzi wao na usipokuwa makini waweza usijue nani ni mlinzi hata sisi tujifunze sio walinzi wooote wanatakiwa kuvaa sare hiyo ni rahisi kwa majambazi kujua pivot ya kuanzia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom