Majambazi yapora PESA Muhimbili National Hosp

Muhimbili sehemu gani? Ndani ya hospitali au maeneo ya muhimbili?

Kwenye hospitali ya Muhimbili, kwa maana ya ndani. Baada ya uporaji huo walinzi walifunga geti la kutokea magari
ili kuwadhibiti majambazi ambao siamini kama wana akili finyu ya kuingia na gari.
 
Taarifa za kuaminika zinabainisha kuwepo uporaji wa mamilioni ya pesa kwenye hospitali ya Taifa
ya Muhimbili leo asubuhi ambapo majambazi hayo yamemuua askari polisi aliyekuwa akilinda baada
ya 'kukomaa'. Baada ya tukio hilo na majambazi na kisha kutoweka, ulinzi mkali umewekwa eneo hilo.

Wanaimarisha ulinzi baada ya mamilioni kukwapuliwa!!!!! kwa nini wasiyafukuzie au nao wanamgao nini hapo?
 
Pole sana kwa polisi aliyeuawa. Huyu inawezekana ni mmoja ya polisi wachache waaminifu kwenye kazi yao. Hayo mamilioni yameporwa hospitalini au bank? Hospitali mamilioni yametoka wapi? Na huo ulinzi mkali unawekwa kwa ajili ya nini na hali majambazi washakwenda?

Kwani hospitali haifanyi biashara? Mbona wanakusanya pesa kila siku ambazo baadaye huzipeleka benki!
Majambazi wamewataimu kabla hawajazipeleka benki
 
wamepora kama m.12 hivi, na walikua watatu, wakikuja na pikipiki...wameua m2 mmoja ( askari ) na kumjeruhi mama mmoja mfanyakazi wa maabara mnh....kwa taarifa zaidi wil uptodate u soon.
 
Poleni wafiwana wahanga wa tukio hilo,

Polisi wakaweke ulinzi bungeni amabapo jamaa wanapora kiulaini bila silaha.

Wamechukua hela zao, hi halali yao kama ambavyo kila mtu anavyovuna kwenye shamba la bibi
 
Majambazi yamemteka mhasibu wa muhimbili hosp na kuua mtu 1 na kujeruhi mwingine kwa risasi kisha kutokomea na mamilioni ya shilingi. RADIO1 STEREO
 
Ina maana pesa hizo hazikuwa hata kwenye "safe"? au ziliwekwa kwenye kabati tu???

Pole kwa marehemu na waliojeruhiwa - Polisi wenyewe wanaolinda wanaonekana "wachovu" hawana "afya" na "morale" ya kazi -
Lazima hao majambazi walianza - kustudy situation kabla ya kwenda kuvamia - waliona loopholes nyingi tu

ama kweli dunia imejaa "tabu" na "shida" :pray:
 
Wizi huo umetokea leo asubuhi ambapo mlinzi kauwawa na nesi mmoja kajeruhiwa katika paja alikuwa akipita kandokando ya Benki ya NMB wizi haukutokea Hospitali umetokea Benki!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom