Majambazi yapora PESA Muhimbili National Hosp

Dreamliner

JF-Expert Member
Jan 17, 2010
2,034
213
Majambazi wenye silaha za moto, wamepora kiasi kikubwa cha pesa Muhimbili National Hospital muda mfupi uliopita.

Wakiwa na bastola 2 na pikipiki, walifyatua risasi 2 hewani karibu na mgahawa uliopo ndani jirani na wards za Mwaisela na Kibasila na kuondoka na kitita hicho cha pesa kwa ulaini na kuwaacha wananchi waliokuja kuwaona wapendwa wao wengine wakizimia na wengine wakilia.

Tunachojiuliza, je walinzi wa magetini wanafanya kazi gani? Maana majambazi hao wamepita kwa ulaini kama kwao.
 
Hi wadau!

Kwa taarifa za uwahika nilizonazo majambazi wamevamia mapokezi ya Muhimbili asubuhi hii kwa lengo la kuiba fedha zilizokuwa zinapelekwa bank. Mwenye taarifa zaidi naomba utujuzi.
 
Inawezekana ni mpango uliosukwa mahususi ukihusisha hadi walinzi na watu wanao jua kuwa pesa zipo hapo.

Pia inawezekana hayo majambazi yaliona weakness ya getini
 
Wamemua askari mmoja, lakini siyo police, ni wale askali wa mhimbili.

Wametoka napikipiki ikiwa na watu watatu, anayeendesha na wengine wamebebwa.

Wale askali wa getini wamestuka pikipiki inatokea ndani walikua hawajui kama kuna wizi unaendelea ndani.
 
Majambazi yenye silaha za moto, yamapora kiasi kikubwa cha pesa Muhimbili National Hospital muda mfupi uliopita. Yakiwa na bastola 2 na pikipiki, yalifyatua risasi 2 hewani karibu na mgahawa uliopo ndani jirani na wards za Mwaisela na Kibasila na kuondoka na kitita hicho cha pesa kwa ulaini. Na kuwaacha wananchi waliokuja kuwaoa wapendwa wao wengine wakizimia na wengine wakili. Tunachojiuliza, je walinzi wa magetini wanafanya kazi gani? Maana majambazi hao wamepita kwa ulaini kama kwao.

kazi kweli kweli
 
aiseee......mahali pengi sana walinzi wa magetini ni kama mapambo tu...hakuna lolote......sasa wameua askari na kupora pesa......
 
Inasemekana wamepora makusanyo ya weekend baada ya kutonywa na watu wa uhasibu. Ni inside job.
 
Ni habari za kweli ambazo zimetokea mihimbili,na kuna mlinzi mmoja amepigwa risasi yupo ICU,ila lazima kutakuwa na taarifa zilivuja kabla ya tukio maana jamaaa awawezi kukulupuka tu.
 
Taarifa za kuaminika zinabainisha kuwepo uporaji wa mamilioni ya pesa kwenye hospitali ya Taifa
ya Muhimbili leo asubuhi ambapo majambazi hayo yamemuua askari polisi aliyekuwa akilinda baada
ya 'kukomaa'. Baada ya tukio hilo na majambazi na kisha kutoweka, ulinzi mkali umewekwa eneo hilo.
 
Taarifa za kuaminika zinabainisha kuwepo uporaji wa mamilioni ya pesa kwenye hospitali ya Taifa
ya Muhimbili leo asubuhi ambapo majambazi hayo yamemuua askari polisi aliyekuwa akilinda baada
ya 'kukomaa'. Baada ya tukio hilo na majambazi na kisha kutoweka, ulinzi mkali umewekwa eneo hilo.

Sasa ulinzi mkali ulihitajika kabla ya tukio au baada ya tukio?
 
Muhimbili sehemu gani? Ndani ya hospitali au maeneo ya muhimbili?
 
Pole sana kwa polisi aliyeuawa. Huyu inawezekana ni mmoja ya polisi wachache waaminifu kwenye kazi yao. Hayo mamilioni yameporwa hospitalini au bank? Hospitali mamilioni yametoka wapi? Na huo ulinzi mkali unawekwa kwa ajili ya nini na hali majambazi washakwenda?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom