Majambazi yakamatwa yakipanga kuiibia benki

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
POLISI mkoani hapa inawashikilia watu wanne akiwemo aliyekuwa mfanyakazi wa Benki ya Afrika (BOA), waliokuwa kwenye jaribio la uporaji wa benki hiyo, iliyopo katika Mtaa wa Kaluta, jijini Mwanza.

Watuhumiwa hao walikuwa wamepanga kufanya uporaji katika benki hiyo Desemba 21, mwaka huu kabla ya mipango yao kuharibika baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za siri juu ya uvamizi huo uliopangwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Donald Charles (28) aliyekuwa mfanyakazi wa benki hiyo kabla ya kuachishwa kazi, Henry Juma Salehe (32, Emmanuel Masanilo (27) na Wachu Kaloboka, mkazi wa Shinyanga ambaye silaha yake ingetumika siku ya uporaji.

Akifafanua Sirro alisema baada ya Polisi kupata taarifa za uporaji huo, iliweka mtego na kumkamata mfanyakazi wa zamani wa BOA, Donald Charles na kufanya mahojiano, na alikiri kutaka kufanya uporaji.

Sirro alisema katika mahojiano hayo, Charles aliwaeleza Polisi kuwa baada kuachishwa kazi, alianza kuwasiliana na majambazi ili washirikiane kufanya uporaji katika benki hiyo na hivyo kuwezesha polisi kuwapata watuhumiwa hao.

Alisema upelelezi ukikamilika watuhumiwa hao, watafikishwa mahakamani, huku akiwashukuru na kuwapongeza wananchi wema walitoa taarifa juu ya kutaka kufanyika kwa uporaji huo.

Alisema iwapo uporaji huo ungefanyika, ingekuwa ni aibu kwa Jeshi la Polisi ambalo linaendelea kupambana kwa nguvu zote kuhakikisha linawatia nguvuni majambazi.

Amewaomba wananchi kuendelea kuwapatia taarifa za siri zitakazosaidia kukomesha vitendo vya ujambazi katika Mkoa wa Mwanza.
 
Hao nao walikua wazembe kweli!Yani wanakamatwa wakipanga na sio tayari wameshaiba?
 
Back
Top Bottom