Majambazi Wawili na Mchina Kupewa Kesi Ya Dr. Ulimboka...Ahmed Msangi Kusafishwa

Habari za kuaminika toka ndani ya polisi zinasema kwamba, kuna majambazi wawili na mgeni mmoja anayesadikiwa kuwa raia wa China, tayari wameshachukuliwa kutoka katika gereza moja mkoa jirani kwa ajili ya kuwabambikizia kesi ya utekaji nyara Dr. Ulimboka. Pamoja na hao raia wa Tanzania, yupo pia mchina mmoja ambaye inasemekana ni jambazi pia kuhusishwa. KOVA atatoa taarifa akisema kwamba kuna jambazi wawili bado wanasakwa na inasadikiwa wamevuka mpaka wa tanzania kwenda zambia Haya yote yakiendelea, uongozi wa juu Ikulu imekuwa ikipewa taarifa kila baada ya muda mfupi

Wote watakiri kufanya kazi ya utekaji wakiwa na Mkenya feki. Gari la Szuki Eskudo jeusi lililokuwa Central police nalo limehamishwa kwa na kupelekwa kwenye pori kibaha ili ionekane kwamba hao majambazi wanamaficho kibaha. Wazalendo ngoma ndio inaanza. Mpango mzima unasukwa wiki mbili sasa kwa lengo la kulisafisha serikali na jambazi SUGU Ahmed Msangi. Kuna mbinu nyingine mbili ambazo zinaratibiwa na TISS. Mtu wetu wa ndani atatuletea habari kamili ikikamilika. Kha hii nchi imeoza
Mkuu ccm mama,hebu endelea kushusha vitu,hizi nondo noma,yani nimeamini alikuwa anahitajika ulimboka ili watanzania tuondokane na hii serikali ya kihuni
 
Jukwaa la utabiri lianzishwe ili hizi threads zihamishiwe huko.
 
Magwanda mmefulia kudakia hoja za watu!

Uli, vipi hajambo?
anarudi lini?
akirudi ataendeleza migomo?

Mkiwasiliana nae mpeni pole sana, mwambieni ndio ukubwa na umaarufu huo, huwa unapatikana kwa njia nyingi, moja ni kama hiyo.

Hivi Ulimboka alikuwa ni chadema?
 
Enyi wana-JF wenzangu,

Onyesho la kwanza laa sakata la kumtoa Dk Ulimboka roho inasadikiwa kuazia pale Leaders Club na kuishia Mabwepande Tegeta.

Wahusika walioonekana tu mwishoni mwa picha katika onyesho hilo ni pamoja na Mama Bishimba, Mwanakijiji, Mdhurika Dk Ulimboka paamoja na wanakijiji maahali pale.Onyesho la pili likawa ni timu ya Ahmed Msangi, Afande Kova, Nabii Mkuu naa Mtume Askofu Gwajima pamoja na 'Joshua' Muyungi.

Onyesho la tatu ya filamu hii ni pale mahakamani Kisutu ambapo kunadaiwa wahudhuriaji karibu wote walikua ni watu wa KUFIKIRIKA tu.

Baada ya kona hizi zote na mzaha uliopita kiwango, je ni nani kati yetu hapa anayeweza kututabiria ONYESHO LA NNE litakavyokua katika filamu hii mara baada ya kutathmini onyesho zilizotangulia, je?

1. Kuna uwezekano filamu ikaishia hapa hapa?

2. Kuna uwezekano filamu ikaanza upya?

3. Yawezekana Staringi Dr Ulimboka akaibuka upya na kuipa nguvu zaidi picha hii?

4. Kuna uwezekano steringi Dr Ulimboka akanunuliwa kwa kupewa KIFUTA DAMU (Mganga Mkuu wa Serikali Wizarani) na picha zima kupata taswira mpya?

5. Yawezekana, kwa mara ya kwanza katika historia ya ulimwengu wa filamu duniani, huyu Steringi Dr Ulimboka wakamkolimba huko huko ili kinachodaiwa mezani hivi sasa ndicho kibakie ukweli na ukweli mtupu wa mambo (Afande Kova et al 2012)?

Katika onyesho la nne, watatafutwa watu wengine ambao watabebeshwa huu mzigo wa nani mhusika, maana ili picha iishe salama lazima watafute mtu watakayemtwisha mzigo walioubeba maana unawaelemea nisawa na kubeba gunia la mavi usipolemewa litakunukia, Inavyoonekana mkuu wa kaya amewapa muda wafanye haraka kumsafisha
 
Habari za kuaminika toka ndani ya polisi zinasema kwamba, kuna majambazi wawili na mgeni mmoja anayesadikiwa kuwa raia wa China, tayari wameshachukuliwa kutoka katika gereza moja mkoa jirani kwa ajili ya kuwabambikizia kesi ya utekaji nyara Dr. Ulimboka. Pamoja na hao raia wa Tanzania, yupo pia mchina mmoja ambaye inasemekana ni jambazi pia kuhusishwa. KOVA atatoa taarifa akisema kwamba kuna jambazi wawili bado wanasakwa na inasadikiwa wamevuka mpaka wa tanzania kwenda zambia Haya yote yakiendelea, uongozi wa juu Ikulu imekuwa ikipewa taarifa kila baada ya muda mfupi

Wote watakiri kufanya kazi ya utekaji wakiwa na Mkenya feki. Gari la Szuki Eskudo jeusi lililokuwa Central police nalo limehamishwa kwa na kupelekwa kwenye pori kibaha ili ionekane kwamba hao majambazi wanamaficho kibaha. Wazalendo ngoma ndio inaanza. Mpango mzima unasukwa wiki mbili sasa kwa lengo la kulisafisha serikali na jambazi SUGU Ahmed Msangi. Kuna mbinu nyingine mbili ambazo zinaratibiwa na TISS. Mtu wetu wa ndani atatuletea habari kamili ikikamilika. Kha hii nchi imeoza


Nasikitika sana na shangaa raisi aliitisha baraza la usalama wa taifa na waziri mkuu akathibitishia bunge.Hivi ni kwanini,hilo baraza lisikubali kuteua tume huru ya uchunguzi kuliko hizi comedi, kila mtu anashangaa ni serikali gani babaishaji namna hii?dunia si ya wajinga namna hii hakukuwa na haja ya serikali kutafuta kujisafisha na kuwakimbiza watu mahakamani kibabaishaji na kuacha watu wakiguna.Nakumbuka drama ya kwanza ilikuja hivi hivi na kova sijui huwa haiingiii JFakaifuata hivyohivyo wakati tayari tulikuwa tunaifahamu.CCM na ujinga huu utawaharibia kwa kung'ang'ania mamabo ya kizamani ambayo hayakubaliki.
 
kwa hiyo ule mpango uliosemwa humu na yule member de'levis ni huo ndo wanataka kuufanya.....ile thread sijui iko wapi!!
Sehemu husika hii hapa Edson Mkuu kutoka post hii ya de'levis: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...rikali-kuficha-ukweli-juu-ya-dr-ulimboka.html
2. Kamanda wa polisi kova ameelekezwa KUHAKIKISHA anailinda serikali katika jambo hili na afanye awezalo kuonyesha umma wawatanzia kuwa serikali haihusiki na jambo hili.katika kuficha na kuilinda serikali kova, mwema na maafisa wa wajuu wa usalama wa taifa walishauliana ili kuilinda serikali na kadhia hii mahabusu 5 wenye makosa ya ujambazi wanahitajika kutoka katika magereza yaliyopo mwanza, songea, tabora, tanga na kigoma waletwe dar ili hao waweze kuonyeshwa kwenye vyombo ya habari kuwa ni majambazi yaliyomteka ulimboka na kumpiga. wakishapatikana wataonyeshwa kwenye vyombo vya habari na umma wa watanzania utaambiwa kuwa wale ndio walifanya unyama huo wako chini ya ulinzi na kuwa maohojiano yanaelendelea na uchunguzi ukikamilika watapelekwa mahakamani na hapo ndipo utakuwa mwisho wa mchezo.

3. mbinu nyingine ni kuwa mahabusu hao wasafirishwe hadi pwani na wauwawe wote na taarifa itoke kuwa ndio waliomteka dr ulimboka na wamekamatwa wakiwa mkoa wa pwani katika msako mkali wa jeshi la polisi. Na katika kujibizana risasi polis ilifanikiwa kuwaua majambazi hayo. Na hapo ndo itakuwa mwisho wa swala hili na serikali itakuwa imenawa mikono na kujisafishaKwa sasa kinachofanyika ni kuwasiliana na magereza husika ili kila gereza litoe mtu mmoja (mahabusu) atakayesafirishwa hadi dar/pwani na wataunganishwa kisha kuonyeshwa kwenye vyombo vya habari wakiwa hai au maiti ili kuuaminisha umma kuwa wao ndio walimvamia dr.ulimbokaUpelelezi na uchunguzi unaofanyika sasa ni changa la macho kwa watanznai na hiyo tume aliyoiunda kova nayo ni changa la macho ,na kama ulimboka alifanikiwa kuwaona vizuri na kuzishika sura zao ,mmoja wao yupo katika kamati hiyo. hakuna uchunguzi wowote utakaofanyika wenye tija kwa taifa juu ya kilichotokea.Kamanda Kova anasimamia operation hii na ameambiwa HAKIKISHA serikali inasafishika.
 
Last edited by a moderator:
Nchi imekwisha,tuna amini Mungu wetu atazidi kuwaumbua watu wote wa serikali wenye mpango wa kuwadhuru watu wanaopigania haki za watanzania wanyonge.
 
yaani kama ni kweli basi tayari wameshabadilisha mbinu hawatakuja na habari hiyo maana imeshavuja, dah jf ni zaidi ya usalama wa taifa. hivi kuna watu wako wanafanya kazi ikulu na polisi hawapendi mambo yanavyoenda sio??
 
Hatuna tena vyombo vya dola vinavyoaminika. Na tanzania imeoza utadhania haina rais na serikali.Mungu tuhurumie taifa letu linazama kwa kukosa maarifa na watu wazalendo
 
Nimeamini Dr.Slaa alivyosema serikali ni weupe kama karatasi, kila kitu kinavuja.Safi sana
 
Back
Top Bottom