Majambazi wavamia hoteli serengeti na kuua mzungu na meneja!

Simchezo

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
445
345
Kundi la majambazi wamevamia hoteli iitwayo Ikoma Bush Camp na kuwapora wageni wote mali zao then wakamuua mzungu mmoja na meneja wa hiyo lodge ambaye ni mtanzania, imetokea usiku wa kuamkia leo.
 
Kundi la majambazi wamevamia hoteli iitwayo Ikoma Bush Camp na kuwapora wageni wote mali zao then wakamuua mzungu mmoja na meneja wa hiyo lodge ambaye ni mtanzania, imetokea usiku wa kuamkia leo.

Wameua Mzungu na Meneja au wameua watu wawili?
 
Kundi la majambazi wamevamia hoteli iitwayo Ikoma Bush Camp na kuwapora wageni wote mali zao then wakamuua mzungu mmoja na meneja wa hiyo lodge ambaye ni mtanzania, imetokea usiku wa kuamkia leo.

Ni habari ya kusikitisha katika tasinia ya utalii ya Tanzania. Hoteli zizopo katika maeneo ya ushoroba zinatakiwa zipewe ulinzi wa kutosha kama hifadhi za taifa.

Mungu aweke roho za marehemu mahali pema (RIP).
 
Toka wamewasimanisha kazi askari wa hifadhi ya serengeti kupisha uchunguzi wa nani iliua faru matukio ya kuvamiwa watalii ndani ya hifadhi hiyo yameshamiri kwa kasi.huwezi kuwasimamisha kazi askari 28 bila kiziba nafasi zao then kusitokee ujambazi
 
Mheshimiwa Balozi Kagasheki hakujua athari za kumsimamisha Mhifadhi wa Serengeti na askari 28. Hata hivyo, askari wasingeweza kuwazuia majambazi kwa kuwa walishindwa kuwazuia majangili waliowaua wale faru.
 
Wakuu.
Fahamuni kwamba Ikoma bush camp yalikotokea mauaji ni nje ya Hifadhi ya serengeti.Ikoma bush camp iko katika kijiji cha ujamaa Robanda na kuna uangalizi wao wa hizo campsites kupitia Wildlife Management Areas (WMA)
Hivyo wachangiaji ambao mnazungumzia kusimamishwa askari waliolinda faru mnakosea mazima.Maoni yenu si sahihi hata kidogo.
 
Campsite ilovamiwa yaitwa Moivaro na si Ikoma

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Campsite ilovamiwa yaitwa Moivaro na si Ikoma

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

inamilikiwa na Moivaro....jina ni Ikoma bush camp....
hilo eneo hatari sana....mwaka huu pia walivamia camp ya Thomson iliyopo eneo hilo hilo....ila hawakuuwa....
 
Tuangalie tunavyo ripoti habari hizi cause zina haribu biashara yetu ya utalii Tanzania. Kesho utaona nchi jirani lazima taarifa hii waipe heard line. Tuviache vyombo husika vifanye kazi yake.
 
Hii ni habari mbaya sana kwa Taifa letu!
Wote wale waliopatwa na msiba nawapa pole nyingi na MUNGU akawalaze marehemu mahala pema peponi.

NB
Ile camp hawakuwa na ulinzi wowote ule?
 
Tungalie tunavyo ripoti habari hizi cause zina haribu biashara yetu ya utalii Tanzania. Kesho utaona nchi jirani lazima taharifa hii waipe heard line. Tuviache vyombo usika vifanye kazi yake.

Unatakiwa kufahamu hao unaowaita nchi jirani kuwa wako open sana ndio maana wanasonga mbele. Kwa vile ufahamu tu ni kwamba tukio kama hilo likitokea kwa wageni balozi zao huwa za kwanza kuwa na taarifa hata kabla ya askari wetu wa landrover. Nadhani ulitaka vyombo husika viripoti labda waseme wamekufa kwa malaria? Pole sana unafiki kamwe hautaisaidia nchi yetu kusonga mbele...
 
Hii ni habari mbaya sana kwa Taifa letu!
Wote wale waliopatwa na msiba nawapa pole nyingi na MUNGU akawalaze marehemu mahala pema peponi.

NB
Ile camp hawakuwa na ulinzi wowote ule?

kambi ipo nje ya hifadhi....na ni sehemu karibu na barabara.....ishu kama hizi huuzwa na wafanyakazi wasio waaminifu....ndio hutoa ramani nzima....kama sio mwenyeji wa eneo husika.....huwezi kufahamu lini wageni wapo na yapi mahema yenye wageni...
 
Hii ndo njia pekee ya kurudisha jasho letu linalo liwa na mafisadi
 
Hii ndo njia pekee ya kurudisha jasho letu linalo liwa na mafisadi

hapana....hapa napingana na wewe.....jaribu kufanya utafiti kujua umuhimu wa utalii nchini.....ndio uje useme kauli yako hii.....
 
hapana....hapa napingana na wewe.....jaribu kufanya utafiti kujua umuhimu wa utalii nchini.....ndio uje useme kauli yako hii.....
Hii sekta inawanufaisha watu wachache sana
 
  • Thanks
Reactions: Aza
Back
Top Bottom