Majaliwa: Ajira mpya za Walimu ni Julai 2016

Status
Not open for further replies.

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,783
66,962
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa anaongea na Wazazi mkoani Ruvuma katika ziara yake ya Serikali mkoani humo. Amesema serikali itamaliza tatizo la uhaba wa waalimu na hasa wale wa sayansi pindi itakapowaajiri Julai mwaka huu.

Chanzo: Dira ya Mchana Tbc1
 
Kweli nimemsikia akisema hivyo, japo Julai ni mbali vijana wajipange kutafuta mbadala wa maisha kwa miezi takribani 7
 
Waache mchecheto mwezi wa saba mbona karibu tu, kuna watu hawajui hata mwezi wa ajira
 
acheni kuwatania wenzenu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa anaongea na Wazazi mkoani Ruvuma katika ziara yake ya Serikali mkoani humo. Amesema serikali itamaliza tatizo la uhaba wa waalimu na hasa wale wa sayansi pindi itakapowaajiri julai mwaka huu.

Source: Dira ya Mchana Tbc1
watu wamechoka kukaa kitaa,waliexpect kuajiriwa between jan to april leo unawaongezea miezi tena?hahaaa.naona kama na jkt inawahusu hawa vijana.teh teh!walimu kasimu anawatania tu ajira mwezi feb
 
Wakalijenge sasa kwa huo muda ili waweze kuyakabili maisha ya vituo watakavyopangiwa ambavyo vingi ni vijijini


Vijana maua popote huchanua,twendeniii tukalijenge taifa
Mama walile walileee mama walile walile mama walileee mama walile
 
Wakomae tu kujiajiri kwa mda itawasaidia sana kuliko kusubiri ajira mwisho wa siku unaajiriwa bila hata sent ya kuanzia maana pesa yenyewe ya kujikimu n kizingumti kupata
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom