Majaji wetu hii ni aibu kwa taaluma yenu

urasa

JF-Expert Member
Aug 12, 2010
434
2
nimesoma kwa masikitiko makubwa sana kwenye gazeti la majira la leo kuwa jaji anasema pingamiza la dr slaa kwa kikwete juu ya kukiuka sheria ya gharama za uchaguzi ni gumu kwa vile anapendwa na wengi,hapa ni udharirishaji mkubwa wa taaluma zao,hao watu wengi wanaompenda kikwete ni wakina nani?wezi wa epa?wauaji wa albino?wakwepa kodi wakubwa?anatoa taswira gani kwa mahakama zetu?
 
Sio pingamizi la Dr Slaa. Ni lile pingamizi la mwalimu Mhozya anae\yeendesha kesi yake binafsi na uteuzi wa Kikwete.
 
Kweli jaji kama amesema hivyo amekosea na lazima anyang'anywe ujaji

Ni kweli wengi bado wanampenda kikwete, wanaompenda Padri Slaa ni watufulanifulani, inabidi uombe radhi wa tanzania wanao mpenda Kikwete kwa kuwaita majina ya machafu kama wezi, wauwaji wakwepa kodi

Nasubiri uomberadhi kabla sijaendelea,,,,,,
 
Sio pingamizi la Dr Slaa. Ni lile pingamizi la mwalimu Mhozya anae\yeendesha kesi yake binafsi na uteuzi wa Kikwete.

Hivi Katiba si inasema kuwa Rais hawezi kushtakiwa akiwa madarakani isipokuwa kupitia Bunge kulingana na Ibara ya 46A? Au mimi sijaielewa Ibara husika wakuu?
 
Ndio sababu katika siku mia moja hili nalo linatakiwa liwe limeshughulikiwa. Hamna kinga kwa mwizi.
 
Hivi Katiba si inasema kuwa Rais hawezi kushtakiwa akiwa madarakani isipokuwa kupitia Bunge kulingana na Ibara ya 46A? Au mimi sijaielewa Ibara husika wakuu?

.
Hivi rais anachangisha bil 50 za kumwezesha kuwa rais?
TIA AKILI!
 
Hii siyo jinai -- hili la huyu Mwalimu Mhozya ni pingamizi tu kutokana na Sheria za Uchaguzi.
 
.
Hivi rais anachangisha bil 50 za kumwezesha kuwa rais?
TIA AKILI!

JK kachangisha hizo hela ni za kufanyia kapeni kama ilivyo Marekani na nchi nyigine,
Kumbuka hakuchangisha ili awe rais, na je ulitaka aibe au afanyeje?

Hillary Clinton alichangisha hela je zilimpa urais wa Marekani????
John "Macain" aliyegombea kupitia Republican dhidi ya Obama alichangisha hela je alipata urais. Mkuu Kiby usiweke hoja ili mradi umeendika ingawa hatukuzuii kuegemea pale unapotaka lakini tumia hoja zenye nguvu.
 
Hivi Katiba si inasema kuwa Rais hawezi kushtakiwa akiwa madarakani isipokuwa kupitia Bunge kulingana na Ibara ya 46A? Au mimi sijaielewa Ibara husika wakuu?
Mkuu anayeshitakiwa sio rais isipokuwa mgombea uraisi kupitia ccm.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom