Majaji watano sasa kusikiliza rufaa ya Lugora

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,336
MVUTANO wa kisheria ulioibuka katika rufaa iliyofunguliwa na Chiriko Haruni, aliyekuwa mgombea wa kiti cha ubunge wa Mwibara kupitia tiketi ya Chadema dhidi ya mbunge wa jimbo hilo, Kangi Lugora umesababisha mahakama kuona umuhimu wa kuongeza jopo la majaji kutoka watatu hadi kufikia wanne.

Rufaa hiyo ilitarajiwa kuanza kusikilizwa jana na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, Jijini Dar es Salaam, linaloundwa na Jaji Edward Rutakangwa, Jaji Bernard Luanda na Jaji Katherine Oriyo.

Hata hivyo ilikwama baada ya kuibuka kwa mvutano wa kisheria, ambao ulisabibisha wakili wa mrufani, Hubert Nyange, kuomba suala hilo likaamuliwe na jopo la majaji watano, jambo ambalo lilikubaliwa.
“Tumekubali suala hili lipelekwe katika jopo la majaji watano na usikilizwaji utapangwa na Jaji Mkuu,” alisema Jaji Rutakangwa wakati akiahirisha rufaa hiyo.

Mvutano huo uliibuka baada ya Lugora kupitia kwa wakili wake, Melikzedeck Lutema kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, iliyotolewa na Jaji Chocha, Novemba 21 mwaka 2011, kuhusu utaratibu wa kulipa gharama za kufungua kesi za uchaguzi.

Awali, Haruni alikata rufaa kupinga hukumu hiyo iliyompa ushindi Lugora katika kesi ya msingi namba saba ya mwaka 2010, lakini mbunge huyo naye alikata rufaa kupinga hukumu hiyo na hivyo kuwapo kwa rufaa mbili kutoka kila upande.

Katika rufaa yake, Lugora pamoja na mambo mengine, anadai kuwa Haruni alilipa gharama za kufungua kesi dhidi yake bila kuiomba mahakama imkadirie kama inavyoelezwa katika katika kifungu cha 111 (3) cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010.Anadai kuwa kutokana na hali hiyo, Haruni alikiuka sheria na kwamba hata mwenendo wa kesi hiyo ya msingi ulikuwa batili.

Lugora pia anarejea uamuzi wa Mahakama ya Rufani, katika rufaa ya Katan A. Katan dhidi ya Mbunge wa Tandahimba, Juma Njwayo Abdallah, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo.
Katika rufaa hiyo namba 115 ya mwaka 2011, jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani waliitupilia mbali kutokana na kutokuwepo kwa mwenendo wa maombi ya kupangiwa gharama za kufungua kesi hiyo.

Wakili wa Haruni, Nyange alidai kuwa utaratibu alioutumia mteja wake kulipa gharama hizo bila kuwasilisha maombi ili mahakama impangie ni sawa na kwamba hauna tatizo.

Kutokana na mvutano huo Nyange aliomba suala hilo liamuliwe na jopo la Majaji watano badala ya jopo hilo la majaji watatu, kuwa tayari jopo hilo lilishatoa uamuzi katika kesi nyingine inayofafana na hiyo.

Upande wa wajibu rufaa, Wakili wa Serikali Mkuu, Obadia Kameya kwa niaba ya mjibu rufaa wa pili (Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mwibara na mjibu rufaa wa tatu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali) hawakuwa na pingamizi kwa maombi hayo ya Nyange.
 
Wednesday, 26 September 2012 21:38
Majaji watano sasa kusikiliza rufaa ya Lugora

James Magai

MVUTANO wa kisheria ulioibuka katika rufaa iliyofunguliwa na Chiriko Haruni, aliyekuwa mgombea wa kiti cha ubunge wa Mwibara kupitia tiketi ya Chadema dhidi ya mbunge wa jimbo hilo, Kangi Lugora umesababisha mahakama kuona umuhimu wa kuongeza jopo la majaji kutoka watatu hadi kufikia wanne.

Rufaa hiyo ilitarajiwa kuanza kusikilizwa jana na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, Jijini Dar es Salaam, linaloundwa na Jaji Edward Rutakangwa, Jaji Bernard Luanda na Jaji Katherine Oriyo.

Hata hivyo ilikwama baada ya kuibuka kwa mvutano wa kisheria, ambao ulisabibisha wakili wa mrufani, Hubert Nyange, kuomba suala hilo likaamuliwe na jopo la majaji watano, jambo ambalo lilikubaliwa.

"Tumekubali suala hili lipelekwe katika jopo la majaji watano na usikilizwaji utapangwa na Jaji Mkuu," alisema Jaji Rutakangwa wakati akiahirisha rufaa hiyo.

Mvutano huo uliibuka baada ya Lugora kupitia kwa wakili wake, Melikzedeck Lutema kukata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, iliyotolewa na Jaji Chocha, Novemba 21 mwaka 2011, kuhusu utaratibu wa kulipa gharama za kufungua kesi za uchaguzi.

Awali, Haruni alikata rufaa kupinga hukumu hiyo iliyompa ushindi Lugora katika kesi ya msingi namba saba ya mwaka 2010, lakini mbunge huyo naye alikata rufaa kupinga hukumu hiyo na hivyo kuwapo kwa rufaa mbili kutoka kila upande.

Katika rufaa yake, Lugora pamoja na mambo mengine, anadai kuwa Haruni alilipa gharama za kufungua kesi dhidi yake bila kuiomba mahakama imkadirie kama inavyoelezwa katika katika kifungu cha 111 (3) cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010.Anadai kuwa kutokana na hali hiyo, Haruni alikiuka sheria na kwamba hata mwenendo wa kesi hiyo ya msingi ulikuwa batili.

Lugora pia anarejea uamuzi wa Mahakama ya Rufani, katika rufaa ya Katan A. Katan dhidi ya Mbunge wa Tandahimba, Juma Njwayo Abdallah, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo.
Katika rufaa hiyo namba 115 ya mwaka 2011, jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani waliitupilia mbali kutokana na kutokuwepo kwa mwenendo wa maombi ya kupangiwa gharama za kufungua kesi hiyo.

Wakili wa Haruni, Nyange alidai kuwa utaratibu alioutumia mteja wake kulipa gharama hizo bila kuwasilisha maombi ili mahakama impangie ni sawa na kwamba hauna tatizo.

Kutokana na mvutano huo Nyange aliomba suala hilo liamuliwe na jopo la Majaji watano badala ya jopo hilo la majaji watatu, kuwa tayari jopo hilo lilishatoa uamuzi katika kesi nyingine inayofafana na hiyo.

Upande wa wajibu rufaa, Wakili wa Serikali Mkuu, Obadia Kameya kwa niaba ya mjibu rufaa wa pili (Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mwibara na mjibu rufaa wa tatu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali) hawakuwa na pingamizi kwa maombi hayo ya Nyange.
 
Jamani CDM mwacheni Kangi hilo jimbo maake mkimtoa magamba yatafrahi sana maana huwa anawachana live bila chenga.
 
Kazi imeanza, rufaa juu ya rufaa. Bora ya Lema Jaji Mkuu kaamua kujitosa mwenyewe ila kuhamishia kesi Dar hapana. Yaani anataka watu wa arusha wasafiri kuja dar kusheherekea? Poa hata Dar CDM ipo tena majimbo yote ni kwa vile tu chakachua inaharibu.
 
Back
Top Bottom