Majaji hawa 7 ndiyo adui wa demokrasia TZ

Their tym is approaching to the moribund bse they ar in vegetative state at this particular juncture!!
 
Majaji hawa 7 wa Mahakama ya Rufaa wakiongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu Augustino Ramadhan,akisaidiwa na majaji wenzake 6 ambao ni Eusebio Munuo, Januari Msofe, Benard Luanda, Mbarouk Mbarouk, Nathalia Kimaro na Sauda Mjasiri;hapo Juni 16, 2011 walikataa TZ isiwe na mgombea binafsi tena wakitupilia mbali andiko ndani ya katiba linalosema kuwa"Kila mtz ana haki ya kupiga na kupigiwa kura";Kama kupiga kura hatuhitaji kuwa na udhamini wa chama cha siasa iweje kupigiwa kura lzm udhaminiwe na chama cha siasa?

Bado nitazidi kuwaheshimu hadi siku yangu ya kufa Majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo kwa kuruhusu mgombea binafsi kabla ya majaji wengine 7 wa Mhakama ya Rufaa kuhujumu demokrasia yetu!

Tuseme ukweli na wala kutoa maoni yako huru kusichukuliwe kama ni kuingilia uhuru wa mhimili mwingine wa dola!Kama mgombea binafsi angeruhusiwa unahisi hii fukuza fukuza ya wabunge na madiwani tunayoishuhudia sasa hivi ingekuwepo?
kuuliza si ujinga hivi mgombea binafsi ataendesha vipi shughuli zake na kupitisha vipi sera zake katika bunge la muundo uliopo? maana at times nadhani kama vile tunalilia mvua wakati visima vya kuhifadhia maji atujajenga.
 
Kama sikosei, ktk jopo la majaji saba waliotoa hukumu,mmoja alikubaliana na hoja ya mgombea binafsi,sita walikataa.
 
hivi haiwezekani kufungua tena hii kesi ya kudai mgombea binafsi, au kuna hamakama ya kimataifa tunayoweza kwenda kufungua tena hili shauri wataalamu wa sheria tujuzeni. na ikiwa inawezekana je mnaonaje sasa tukajiunga kama watanzania tukawawezesha wanasheria makini kama mtikila wenye kuweza kufungua na kutete kesi tukapata ushidi na hatimae haki ikatenda?

Mtikila alishafungua hiyo kesi katika African Court on Human and People's Rights! Click HAPA!
 
Tanzania inaongoza kwa majaji kujikomba kwa watawala!!!
wenzetu kenya wametuzidi............
Uganda wametuzi, hawa walifikia kufuta kezi zote za DR Besigye na kudai kuwa ni njama tu za kisiasa dhidi yake..... Tanzania hakuna anayeweza kuamua hivyo hakuna!! nchi hii imekufa idara zote!! wana waramba makalio watawala!!
Maskini Tanzania!
 
kuuliza si ujinga hivi mgombea binafsi ataendesha vipi shughuli zake na kupitisha vipi sera zake katika bunge la muundo uliopo? maana at times nadhani kama vile tunalilia mvua wakati visima vya kuhifadhia maji atujajenga.

Kazi ya Mbunge ni kutunga sheria;Kulindaji rasilimali zetu kwa kuipa serikali hela zile tu ilizoomba;then kuisimamia serikali kwenye mgawanyo wa keki ya Taifa ili kuwafikishia wana jimbo lake kile walichogawiwa na serikali kutoka kwenye bajeti kuu(Kumbuka kuwa kuthibitisha uteuzi wa Rais sio kazi ya bunge la TZ)!Sidhani kufanya hivyo kunahitaji lzm uwe na chama!
 
Majaji hawa 7 wa Mahakama ya Rufaa wakiongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu Augustino Ramadhan,akisaidiwa na majaji wenzake 6 ambao ni Eusebio Munuo, Januari Msofe, Benard Luanda, Mbarouk Mbarouk, Nathalia Kimaro na Sauda Mjasiri;hapo Juni 16, 2011 walikataa TZ isiwe na mgombea binafsi tena wakitupilia mbali andiko ndani ya katiba linalosema kuwa"Kila mtz ana haki ya kupiga na kupigiwa kura";Kama kupiga kura hatuhitaji kuwa na udhamini wa chama cha siasa iweje kupigiwa kura lzm udhaminiwe na chama cha siasa?

Bado nitazidi kuwaheshimu hadi siku yangu ya kufa Majaji watatu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Amir Manento, Salum Massati na Thomas Mihayo kwa kuruhusu mgombea binafsi kabla ya majaji wengine 7 wa Mhakama ya Rufaa kuhujumu demokrasia yetu!

Tuseme ukweli na wala kutoa maoni yako huru kusichukuliwe kama ni kuingilia uhuru wa mhimili mwingine wa dola!Kama mgombea binafsi angeruhusiwa unahisi hii fukuza fukuza ya wabunge na madiwani tunayoishuhudia sasa hivi ingekuwepo?

Bado kufukuzwa kwa madiwani na wabunge kugekuwepo, kwani huyo diwani na mbunge walikubaliana na masharti ya chama wakakubali kugombea, sasa wakikosea kwenye chama kwanini wasifukuzwe?
 
Jamaa ameweka wazi kuwa hawa ndiyo majaji walioruhusu mgombea binasfi ambao uamuzi wao ulibadilishwa na hao wa mahakama ya rufaa.

Hivi TZ hatuna constitutional court??

Itoke wapi? si ndio sababu twataka katiba mpya sio ya kurekebisha kama alivyosema Kikwete jamani

Nadhani tunakosea sana kuwahukumu watu waliutumia taaluma yao ya kisheria na kutimiza wajibu wao kikatiba leo kuwaona kuwa ni watu waliofinya demokrasi.
Process ya kesi ya Mtikila ilikuwa ndefu na iliyochukuwa muda mrefu katika mahakama kadhaa.Katika kesi ya msingi MTIKILA alishinda kesi ili katika hukumu iliyosomwa na jaji Mwalukasa katika mahakama kuu ya Dodoma. Baada ya uwamuzi ule serikali haikuridhika ikakata rufaa kupinga uamuzi ule.
Hapo mbaya wako ni serikali na sio mahakama.
 
siyo kila kitu lazima kiwe na uhusiano na magamba. Issue zingine ni za kitaaluma tu. Katika maamuzi mbalimbali ya kimahakama utakuta baadhi ya majaji wanakubaliana ("concur") na wengine wanapingana ("dissent") juu ya suala la kuamua linalokuwa mbele yao ...
 
Article 107A "Mahakama ndiyo chombo cha mwisho ktk utoaji haki" Majaji wakasema "...suala hili lipelekwe bungeni..." Kazi ipo!!!!!!!!!!!
 
Article 107A "Mahakama ndiyo chombo cha mwisho ktk utoaji haki" Majaji wakasema "...suala hili lipelekwe bungeni..." Kazi ipo!!!!!!!!!!!

Hawa Majaji waliotoa uamuzi huu wa Suala hili ambalo ni moja katika haki za msingi za Binadamu, kurudishwa Bungeni ,
Hawaitakii mema kabisa Nchi hii.
Wapo hapo kwa masilshi yao binafsi , si kwa kupigania haki za Raia.
 
Back
Top Bottom