Majaji aliowateua Kikwete: Pre-emptive strike?

Wakuu,

Hoja nzuri imetolewa na malumbano mazuri yametokea (isipokuwa machache yaliyotaka kuharibu utamu wa hoja ya msingi). Nimependezewa na majibu mengi lakini ninalokumbuka zaidi ni la Chief Kahangwa.

Hili jambo la checks and balances tumekuwa tukiliimba kwa kipindi kirefu sasa. Rais ana madaraka makubwa sana na hakuna wa kumfunga kengele. Inawezekana ikawa kweli (au sio kweli) kuwa uteuzi wa majaji ulikuwa ni strategic kwa upande wa Rais. Hii ni hoja nzuri ya kulumbana lakini the big picture ni kuwa, Rais hana spidi gavana!!! That's the main point. Hii sio kwa uteuzi wa majaji pekee, bali kwa watendaji wote wa serikali. Hali ya sasa inaruhusu Rais kuteua yeyote atakayeridhia bila kujali ujuzi wa mtu huyo (once again, let's check on how Mkulo got his MBA) na hii ndio hoja aliyeigusia Mkuu Kahangwa.

Hivi tujiulize, how do the presidential appointees get vetted? Nobody knows! One can argue that we know what's the procedure (like sending TISS people etc) but everything is so secret and the public does not have a clue. Hivi kama kweli Rais angetamka au kupendekeza kwa Bunge kuwa Mh. Masha awe Waziri wa Mambo ya Ndani, si watu wangeanza kuchungua kuwa Mh. Masha ana uwezo gani wa ujuzi, uhusiano gani na watu wanaoshukiwa kuwa wahalifu, alikwepa kodi gani, na vitu vyoote vinavyomfanya akose sifa ya kuwa waziri wa serikali yetu (by the way vyote nilivyotaja ni mfano tu).

Kwa upande mwingine, waheshimiwa hawa wanaweza kuteuliwa kwa strategy za mtu au kundi moja huku wakiwa na uwezo na haki ya kuteuliwa. Kwa mfano, Mh. Yona ana uwezo na sifa ya uchumi. Na alikuwa ni mfanyabiashara kabla hajaingia kwenye siasa. Na kama mtanzania, ana haki ya kufanya biashara yoyote iliyo halali. Je, ilikuwa ni sawa pale alipojisaidia (yeye na bosi wake) umiliki wa Kiwira? Huu mfano ni jibu kwa swali lilioulizwa (nina paraphrase) kuwa je ni vipi Mh. Masha asiwe candidate wa uwaziri wa mambo ya ndani pale MMK alipohoji uhusiano wa Masha na IMMMA.

Mwisho ningependa nimalizie kwa mfano wa kampuni moja ambayo wanaJF walio na ufahamu wa siasa za karibuni za Marekani watatambua. Haliburton!!! Je IMMMA ndio Haliburton yetu huku Kikwetes (JK and Ridhiwani) are the Cheneys while Masha is the Rumsfeld? Yangu Macho!!
 
Kada, muda uliopotea nilidhani umekupa hekima ya kutolalamikalalamika. well nadhani kuna vitu mtu hawezi kubadili..

hapana. hii ni sooo simpo, kama alitumia "authority" yake kurule out alichosema before(mtiririko wa mada, na watu watakuwa banned), why not apply his authority hapa pia ? ndicho ninachouliza,NA SI VINGINEVYO, au kukosolewa ni kwa viongozi wa serikali tu na sio mods wa JF ??
 
hapana. hii ni sooo simpo, kama alitumia "authority" yake kurule out alichosema before(mtiririko wa mada, na watu watakuwa banned), why not apply his authority hapa pia ? ndicho ninachouliza,NA SI VINGINEVYO, au kukosolewa ni kwa viongozi wa serikali tu na sio mods wa JF ??

sawa nimekuelewa nilidhani umeanza kulia tena, kitu ambacho kingeuvunja moyo wangu!
 
Hili jambo la checks and balances tumekuwa tukiliimba kwa kipindi kirefu sasa. Rais ana madaraka makubwa sana na hakuna wa kumfunga kengele. Inawezekana ikawa kweli (au sio kweli) kuwa uteuzi wa majaji ulikuwa ni strategic kwa upande wa Rais. Hii ni hoja nzuri ya kulumbana lakini the big picture ni kuwa, Rais hana spidi gavana!!! That's the main point.[p]



Hivi tujiulize, how do the presidential appointees get vetted? Nobody knows!
[p]
Mkuu naona tuangalie lile azimio la Arusha linasemaje kuhusu viongozi na biashara. Kama kuna mtu ana nakala yake aipost ili tuwe na reference. Kwa sababu wengi tunalijua la Arusha, hivyo inatuwia vigumu kuwa na minofu kwenye maoni yetu kuhusu viongozi wa kileo.

Sasa hivi ni wakati muafaka wa kuangalia upya katiba ya nchi ili madaraka makubwa ya rais katika kuchagua timu yake ya kufanya kazi iwe kwa manufaa zaidi kwanza kwa Taifa halafu Chama chake(Kingunge upo!!!). Ni wazi rais hupata mapendekezo kwa watu wake wa karibu na vyombo husika juu ya wateule wake, lakini hilo halimfungi kumteua anayemtaka. Na pia hao wanaopendekeza wanaweza kabisa kutoa majina wasiyoyataka, hata kama wana sifa stahili, kwenye shortlisting. Kwa kuanzia labda wizara muhimu fulani fulani zinazounda, the so called inner cabinet,mawaziri wake wathibitishwe na Bunge mmoja mmoja,kama ifanywavyo kwa waziri mkuu, badala ya utaratibu wa sasa ambapo baraza zima la mawaziri huthibitishwa. Katika hili pia majaji wawemo ili kuzuia hili swala la coflict of interest.
Tuangalie uteuzi wa majaji kutoka kwenye sekta binafsi wakiwa si tu waajiriwa bali pia wamiliki. Je wanauza hizo biashara au hisa zao kwa watu wasio na uhusiano nao kidamu au kibiashara ili kujiengua kabisa? Maana kampuni hizo nyingi hazijawa listed as public entities. Inafahamika wazi pamoja na kuruhusu wataalamu kuwa na private practices, ethically kuna taaluma ambazo haziwezi kufanya hivyo bila kutokuwa na muingiriano wa maslahi. Mahakimu hawaruhusiwi kuwa na ofisi za uwakili wakiwa bado waajiriwa wa mahakama, nisahihishe kama siendi na wakati. Je hawa majaji walioteuliwa kwa nini wanaruhusiwa? Sabbatical leave pekee haitoshi. Ni wazi watetezi wa uhuru wa rais kuchagua watu wa kufanya naye watasema hata awamu iliyotangulia walifanya hivyo. Je kosa halisahihishiki inapodhihirika kuwa ni kosa. Rais anao uhuru huo lakini si vema kwake kuutumia vibaya.[p]
Mwisho ningependa nimalizie kwa mfano wa kampuni moja ambayo wanaJF walio na ufahamu wa siasa za karibuni za Marekani watatambua. Haliburton!!! Je IMMMA ndio Haliburton yetu huku Kikwetes (JK and Ridhiwani) are the Cheneys while Masha is the Rumsfeld? Yangu Macho!!

Waanzilishi wa IMMMA wengi wao wamekutana vyuoni au pale NDC na makampuni yake, tunawasifu kwa kuunda kampuni hiyo ila tu sasa inaonekana kuwa wamekuwa kama Halliburton ya Cheney kwa kutumia influence zao kushika uwakili wa makampuni yote makubwa. Imewafanya kuwa mlango wa kuingilia mafisadi. Kwa jinsi ya uajiri na historia yao wao sasa ni lobbying company for concerned multinational. Cha msingi wajifunze kuwa kama Cheney, ambaye na kelel zota kuhusu mikataba na tenda za Halliburton Iraq amekaa kimya. Kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala.
 
Back
Top Bottom