Majaji aliowateua Kikwete: Pre-emptive strike?

Acha kujifanya huwajui viongozi wa Tanzania, unategemea, hata akipewa mwingine unategemea jaji mmoja kujaji Kesi ya jaji mwenzake kwa umakini na kwa maslahi ya Taifa?? kwa taifa lenye kwenda kwa kuangaliana kama letu??
Na nafasi ya Masha kama waziri katika hii kesi kama yeye ni mmoja wa wahusika wakuu??
Kweli kazi hipi

Viongozi, wawe wa nchi hii au nyingine, aidha nawajuwa au siwajui, hiyo si hoja. Hilo la pili naomba ujibu wewe mwenyewe.

Maslahi ya Taifa ni matokeo ya hao wenye Taifa lao, la ki-demokrasia, wamemchaguwa nani awe ndie mwenye uwezo wa kuwateuwa kina nani ambao yeye (alie chaguliwa na wananchi) anaona kuwa hawa ndio wennye uwezo wa kuliendesha taifa kwa nyanja zao.

Laiti ingelikuwa mteuaji wa hao walioteuliwa, amejitekea madaraka bila ya kuchaguliwa na kukubalika na wananchi, basi hapo tungelikuwa na shaka na hasima zote za kutokuwa na imani na uchaguzi wa huyo aliejipachika madaraka kwa mabavu.
 
Lunyungu,

Mimi nimeshalalamika mara 2 huyu jamaa afungiwe angalau kwa wiki 2!

JF tuna reguraltions zijui kwa nini Adm saa ingine hawataki kuzitumia!

Huyu jamaa yuko hapa JF just to cause disraction ktk almost kila thread!

Je kwa nini asifungiwe ili akitoka kifungoni awe na ustaarabu kidogo?

Kwenye kila post,kuna kidude juu mkono wa kulia chenye maneno REPORT.Nadhani tukikitumia ipasavto kinaweza kutufanya tujadili issues za msingi without hawa wenzetu wenye ajenda zao binafsi za ku-derail process of change tuliyoianzisha hapa JF
 
Mimi pia mara 2 nilishatoa hoja afungiwe angalau kwa wiki 2 ktk thread ile ya Ndoa ya Mac! Hebu tena iangalia ile thread Painkiller!

Tafadhali msimcheleweshe aendelee kuharibu zaidi!

Mimi naona kuna hoja hapa

Ujaji si elimu tuu, bali pia lazima uwe na uwezo uliothibitika na kuonekana wa kutafsiri sheria, hii haipatikani "overnight"!!! (Warioba alishawahi kuwa mfano...)

Kutishana kufungiwa, huu ni umangi meza, kujaribu kunyima watu haki ya "free speech" Mzalendo unatakiwa kuomba msamaha na kufuta hoja yako!

Nadhani umefika wakati wa madaraka ya Rais kutea majaji yaangaliwe upya, kuzuia uteuzi huo usiwe wa kisiasa au zawadi baada ya ....
 
Inategemea na vigezo vilivyotumiwa na rais katika kufanya uteuzi huo. Ingawa katiba inampa rais mamlaka ya kumteua mtu yeyote kuwa jaji, haitegemewi kuwa atatumia mamlaka hayo kumteua mtu ambaye hana rekodi yoyote na sifa za kuendesha kesi za aina inayoweza kufika mahakama kuu. Kuwa na digrii ya sheria tu hakutoshi kumfanya mtu awe jaji wa mahakama kuu. Sifa za mtu kuteuliwa kuwa Jaji wa mahakama kuu zimetolewa katika Sheria ya Mawakili, hata hivyo, kifungu 109(9) cha Katiba kinamruhusu Rais ku-overide sheria hiyo. Kifungu hiki kimeacaha nafasi ya wazi kwa rais kumteua mtu kuwa jaji wa mahakama kuu kwa sababu zake binafsi bila kujali uwezo wa mteuliwa.

Bado tuna njia ndefu sana.
 
Sheria ya Mawakili, hata hivyo, kifungu 109(9) cha Katiba kinamruhusu Rais ku-overide sheria hiyo. Kifungu hiki kimeacaha nafasi ya wazi wa rais kumteua mtu kuwa jaji mkuu kwa sababu zake binafsi bila kujali uwezo wa mteuliwa.

Very strong point.
 
Sileti fujo, ila ifahamike kuwa hapa ameongelea majaji ambao ni muhimili mmoja wapo wa himaya yetu. Ukiwa na shaka au shauku ya majaji inabidi uwe bayana na mkweli wala usiwe wa kuleta shauku na mafumbo kama muimba mipasho. Ambae hutaka kila asikiae ayatilie maana yeye mwenyewe. La, hasha. katika suala nyeti kama hili haiwezekani tukawa na nyodo.

Ikiwa kuna ukweli ambao unataka kuuweka wazi katika chombo ambacho kina kila hisia na kugusa kila mwananchi wa nchi hii au ambae si wa nchi hii, ambapo hata huyo Raisi anaweza kushitakiwa na mwingine yeyote kwenye chombo hicho, halafu unakiletea utaaradhi na sudfa na kinyongo kisich-oeleweka, unakuwa ni kama yule anaeitwa "fitina mbaya wala hana haya".

Wewe, Lunyungu kiliochokuuma ni nini mpaka ukaona kuwa mimi katika hili sina cha kuongea?

Aiseee, kweli wewe umekurupuka. Mleta hoja kaleta hoja nzuri na ya maana sana. Kama kuna mtu mwenye 'nyodo' ni wewe hapo. Kama wewe unaona mafumbo katika hayo yaliyoelezwa hapo juu, si yaweke wazi tu?
Inaelekea mawazo yako unataka kuyalazimisha ndio yawe mawazo ya Mkjj; hiyo itawezekana kweli?

Mkjj:
Lililo baya zaidi katika utaratibu wa nchi yetu, hakuna anayeweza kupinga uchaguzi alioufanya rais. Majaji hawapitishwi bungeni ili wapimwe katika misimamo yao na mstakabali wa nchi. Akishachaguliwa, basi ameukata huyo; bila kujali maamuzi yake kwa mambo yaliyo muhimu kwa wananchi wengi.

Nadhani pana umuhimu wa watu kama hawa ambao maamuzi yao yanawagusa wananchi wengi, lisiwe jambo la mtu mmoja tu kutua na kupitisha.
 
Nadhani pana umuhimu wa watu kama hawa ambao maamuzi yao yanawagusa wananchi wengi, lisiwe jambo la mtu mmoja tu kutua na kupitisha.

Mkuu Kalamu,

Heshima mbele, hapa sasa ndio kwenye point ambayo tumeisema siku nyingi sana hapa JF, yaaani mapungufu ya katiba yetu,

ingawa pia hata huko USA, rais wao anaweza kui-subiri Congress iko likizo akamchagua jaji kwa mwaka mmoja bila kupitishwa nao, kama alivyomchagua Bolton kuwa balozi wao UN.
 
Mkuu Darsalama,

Hakuna mwenye chuki na wewe hapa, isipokuwa pungza munhali na jazba, tone ya hoja zako sio za kistaarabu, hukatazwi kusimamia hoja zako, lakini jaribu kuwa na heshima pia kwa wengine, ingawa pia kuna wengine hapa JF wenye hizo tabia pia, za kurusha rusha lugha mbovu hapa kama tuko sokoni lakini inapokuja wewe hawajioni, lakini still lazima tuheshimiane mkuu, maana mijadala hapa ni muhimu sana kwa sisi wananchi, sitaki kuwa mnafiki kwenye hili maana kati ya tunaokushambulia pia tuna tabia kama hiyo ya kurusha lugha mbovu ni suala dogo sana la kupitia post zetu, kwa hiyo wote tunaohusika tuache hii tabia, kabla ya kumshambulia Dar, hebu tujiangalie pia,

Ingawa pia ninashangazwa na Mods, kwani sheria zetu hapa JF si zinafahamika, sasa inakuwaje watu wanazikiuka lakini hakuna lolote? Wananchi wanatajwa majina lakini hakuna lolote? Majuzi kulikuwa na ishu ya Mafia, I am shocked mpaka leo yametajwa majina ya watu hapa, hajafungiwa mtu, wala majina hayajafutwa, mimi nilifikiri after what we went through sheria zitakuwa-enforced in a serious note, lakini nashangaa kuona bado kuna abuse everywhere hapa, kwa kweli inasikitisha sana sasa very soon tutarudia tena yale yale,

Wananchi hatuwezi kuheshimu sheria ambazo haziwi enforced wakuu!
 
Mkuu Kalamu,

Heshima mbele, hapa sasa ndio kwenye point ambayo tumeisema siku nyingi sana hapa JF, yaaani mapungufu ya katiba yetu,

ingawa pia hata huko USA, rais wao anaweza kui-subiri Congress iko likizo akamchagua jaji kwa mwaka mmoja bila kupitishwa nao, kama alivyomchagua Bolton kuwa balozi wao UN.

Naam, Bolton - lakini si uliona baadae yaliyotokea? Bolton hayupo tena huko UNO, au sio!

Angalau pawepo na vikelele vya hapa na pale basi katika mjadala wa mtu huyo, ili wananchi wamjue huyo mteuliwa mambo yake yakoje.
Lakini sisi Rais akishachagua, basi tumemaliza.
 
Nimekupata mkuu, lakini kwenye ule mwaka mmoja Bolton, aliifanyia Congress a lot of damages kule UN, lakini tuko wote kwenye rais kuwa na power kubwa mno, sometimes inakuwa kama king!
 
Nafikiri kama damu kumwagika, ishamwagika, na sasa watu hawaisikii ikinuka hivyo hawana time yoyote kupangusa ! kwa kifupi sasa naona watu wamecreate "kamchezo" fulani kwamba kila sehemu ya uongozi under JK since elected inanuka. Hivyo ni rahisi sana kuangukia kwenye huo mkumbo kwa maana kwamba hata kama kuna kosa dogo la kiufundi, au normal problem basi watu watataka wabenefit wao binafsi au vyama vyao kwa kusingizia UFISADI !

Lakini kumbukeni kwamba leo nyinyi kesho wao ! Hii tabia kwa kweli sio nzuri, maana mindset ya mtanzania "ikitengenezwa" basi jua kwamba kweli imetengenezwa, bila kutojali nani yupo madarakani au la, ! sasa since kila mtu anajua kwamba ni kweli kuna baadhi ya watu hapa JF wanatakia mema nchi yetu lakini pia vile vile tukubali kwamba mumu humu JF pia kuna watu hawaitakii mema nchi yetu kwa kujifanya wanataka kusawazisha mambo, sasa sijui kwamba wanataka kuharibu nchi yetu in the long run and indirectly kwa kuwa hawajui au sijui vipi, but in my thinking in kwamba wanajua ! Yaani wanaiua nchi kwa kutupiga ganzi kusema kwamba wanaipenda na kuitetea kwa kila njia which to a lot might seem to be true lakini angalia kiundani zaidi and you will agree with me kwamba there is more than achieving the success of our country !

haya sasa tuendeleeni na mjadala !
 
Kama unataka kutaja ovu au uovu wa alieteuliwa kuwa jaji, inabidi uwe wazi na kwerere, usituletee mafumbo kama yale ambayo mnasema kuwa hawezi mtu kuyajua mafumbo haya ila awe kafunuliwa.

Wakili Binafsi Mujuluzi toka kampuni ya Uwakili ya IMMA ambayo imepokea fedha za wizi toka makampuni ya Tangold na Deep Green na ambako mtoto wa Rais anafanya kazi ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Mojawapo ya makampuni hayo wakurugenzi wake ni Waziri wa Miundo Mbinu Bw. Andrew Chenge aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wakati wizi ule wa Tangold na Deep Green unatokea.

Weka bayana na uwache unoko, na fitna. kuwa mkweli, kama kuna ambalo unalijuwa kuhusu jaji yeyote aliechaguliwa ambalo huridhiki nalo, ikiwa unashindwa kulipinga kidhahiri, huko mahakamani, basi lipinge kisiri hapa JF.

nimetolea mfano hapo juu, inatosha?
Lakini usiwe na fitna na chuki na dharau na hiyana. Una nini wewe?

ndio matatizo hayo tukismama kuuliza tunaambiwa ni fitna na chuki, tuwazirie nchi ili mfanye mpendalo?
 
Sileti fujo, ila ifahamike kuwa hapa ameongelea majaji ambao ni muhimili mmoja wapo wa himaya yetu.

Kwanza, Tanzania hatuna himaya! Haya mawazo ya "himaya yenu" ndio chanzo cha matatizo tulinayo. Kwa sababu mnafikiri kwamba sisi wengine ni watwana kwenyi himaya ambayo wewe na "wenzako" mnajiona mabwana msiohojika, na msiohojiwa! Hilo tunawapinga. Tanzania ni Jamhuri - utawala ambao msingi wake ni watu wake!

U
kiwa na shaka au shauku ya majaji inabidi uwe bayana na mkweli wala usiwe wa kuleta shauku na mafumbo kama muimba mipasho. Ambae hutaka kila asikiae ayatilie maana yeye mwenyewe. La, hasha. katika suala nyeti kama hili haiwezekani tukawa na nyodo.

Kama somo ni gumu nyosha mkono darasani uliza; ukipitwa na jambo omba ufahamu utafahamishwa. Maana sasa nimetambua kumbe kuna haja siyo tu ya kukutwangia mawazo, inabidi nikutafunie, na kukumezea; wewe ushibe tu!
Ikiwa kuna ukweli ambao unataka kuuweka wazi katika chombo ambacho kina kila hisia na kugusa kila mwananchi wa nchi hii au ambae si wa nchi hii, ambapo hata huyo Raisi anaweza kushitakiwa na mwingine yeyote kwenye chombo hicho,

Kama hujui sheria usichangae mada za sheria. Rais hawezi kushtakiwa Mahakamani hata akimbaka mtu!

halafu unakiletea utaaradhi na sudfa na kinyongo kisich-oeleweka, unakuwa ni kama yule anaeitwa "fitina mbaya wala hana haya".

Sasa nani anaimba mipasho!?
 
Miiko ya ujaji ni ipi? udogo unahusiana nini na elimu?

Kwa nini usifanye utafiti wewe mwenyewe? Kama hujui miiko ya Ujaji fanya utafiti usisubiri maswali yako yajibiwe na watu wengine ndio maana Mwenyezi Mungu katupa kitu kinachoitwa "ubongo"!
 
Huna sababu ya msingi. Msilete kutishana kufungiana hapa kwa kuwa tuu, tunajibu hoja na tunayeweka bayana ambayo hamtaki kuyasikia.

tatizo ni kuwa hujibu hoja umebakia kushambulia watu kama hoja zinakuzidi kimo. Ila nakubaliana na wewe, mawazo yako hata kama ni mabovu kiasi gani yana haki ya kusikilizwa. Endelea mzee kutoa mawazo hayo.
 
Jee, huyo wakili alieteuliwa kuwa jaji, ndie huyo ambae ataamuwa kuhusu hiyo kesi ya deep green?
Unajuaje hatokuwa yeye? Nini kitamzuia?

Waziri wa Mambo ya ndani ana husika nini na majaji?

Anahusika na Polisi na Magereza! Je Polisi na Magereza vina uhusiano gani na mahakama. Ukishindwa uliza tu mzee nitajaribu kukunyambulishia na kukubainishia! with gratitude.

Nioneshe wapi nimetoa lugha mbaya kuhusu hili. Wala sina hasira, ila tu, najaribu kuweka bayana. Sijaghafilika kwa hili na wala halina walakin.

sasa kama hata hukumbuki ulichosema wewe mwenyewe huoni kwamba unatupa kazi ya kukumbusha wewe mwenyewe?
 
Mkuu MMJ,

Unatakiwa kuwa bigger than what you wrote,

Inategemea umekisoma vipi nilichosema. Ninapoandika hoja kama hizi mzee sikurupuki. Ninapima kila sentensi na kila neno ninalotumia. Sasa naweza kurahisisha kila kitu na kukiandika kwa lugha nyepesi nikitumia maneno rahisi na kujibu kila swali ambalo laweza kusimama. So, sijui kama unanitaka niendeke kila kitu kinabaga kwa sababu inakuwa vigumu kwa watu kama kina DAR kufuatilia. Nitajihidi mkuu.

Masha ni mbunge wa kuchaguliwa na wananchi, na sheria zetu zinasema waziri lazima awe mbunge, kitu ambacho Masha anakitimiza,

Mzee hakuna mahali popote nilipohoji kuchaguliwa kwa Masha kuwa Mbunge na sijahoji suala la yeye kuteuliwa kuwa Waziri kwa vile ni Mbunge. NItakusaidia. NImehoji kuwa aliyekuwa Wakili katika kampuni ya IMMA ambayo imethibitisha kupokea mabilioni ya shilingi yaliyofujwa Benki Kuu ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na rafiki yake ameteuliwa kuwa Jaji. Na hayo yamefanyika wakati mtoto wa RAis anafanya kazi kwenye kampuni hiyo hiyo. Maadili yasihojiwe mkuu? Na hiki kitendo cha yeye kuzungumzia suala hili akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ni uthibitisho tosha kabisa wa tatizo langu.

Hivi, Kesho Polisi wakitaka kwenda kufanya search and seizure kwenye ofisi za Imma kufuatia uchunguzi wa Tangold na Deep Green, Masha atasimama kuwaruka wenzake? au atajitoa kusimamia suala hilo?


Uchunguzi umefanyika wamepatikana patner wawili wa IMMA, kuhusika na Deep Green, sasa tatizo la Masha liko wapi asiwe mbunge au waziri?

Mzee uchunguzi gani umefanyika ndugu yangu kuhusu Deep Green? Hadi hivi sasa serikali ya RAis Kikwete haijakubali kufanya uchunguzi wa Tangold, Deep Green or Mwananchi Gold. Sijui ni upi unaouzungumzia.? I might have missed this.
Nini vigezo vya katiba yetu kuhusu rais kuchagua majaji? Maana hata huko USA, sio majaji wote wanaopita senate hata kama wamechaguliwa na rais,

Ndiyo lakini tunafahamu kuhusu senate recess appointments, lakini tunajua ugumu wake. Si umeona walivyomchezea Bush mwishoni mwa mwaka jana? Walihakikisha anabakia angalau Seneta mmoja kumzuia Bush asifanya recess appointments. Kaka Rais wetu hana vizuizi hivyo!

unless jaji aliyeteuliwa na rais Tanzania, hatimizi masharti, mkuu huna argument kabisa,

Nimekupata mzee, kama unafikiri sina "argument kabisa"..

hata huko USA mbona inaeleweka kuwa rais anaweka majaji anaotaka wakubali sera zake? Sasa hiyo inakuwaje tofauti na rais wa bongo aliyechaguliwa na wananchi kwa kuuza sera zake kwenye kampeni, yes ili atimize sera zake huenda akahiataji majaji wenye kufuata itikadi kama zake kisasa, je kuna tatizo hapo kweli?

Hilo ndilo jambo jingine kwa sababu siku moja ataingia Rais toka chama kingine na ataanza kuingiza majaji wanaofuata sera na mtazamo wake, au watakaomsaidia kutimiza haja zake na hapo ndipo utaelewa kwanini mada hii na hoja yangu ina uzito wa pekee. Ingawa kwa sasa labda ni vigumu kuiona.

Kama vinavyofanywa Marekani ndivyo vilivyo bora, tufuate basi safeguards zao. Kwanini basi tusihakikishe mawakili wanaopendekezwa kuwa majaji wanaitwa kwenye Kamati ya Sheria na Katiba ya Bunge na wanapigiwa "up and down" vote. Kama Bunge linaweza kuwa impeach majaji, kwanini halishikiri katika uteuzi wake?
 
Back
Top Bottom