Maiti Yazinduka Monchwari na Kuzua Kizaazaa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Maiti Yazinduka Monchwari na Kuzua Kizaazaa
5838950.jpg
Monday, July 25, 2011 4:34 PM
Mwanaume mwenye umri wa miaka 50 wa nchini Afrika Kusini ambaye alihisiwa kuwa amefariki na mwili wake kulazwa monchwari kwa masaa 21, alizinduka na kuwafanya wafanyakazi wa monchwari wakimbie wakidhani wameona mzimu.
Kelele za maiti akitaka atolewe toka kwenye chumba chenye baridi kali cha monchwari, ziliwafanya wafanyakazi wa monchwari watoke nduki wakidhani wameona mzimu.

Tukio hilo lilitokea jana jumapili nchini Afrika Kusini wakati mwanaume mwenye umri wa miaka 50 kuhisiwa kuwa ameiaga dunia na mwili wake kupelekwa monchwari wakati taratibu za mazishi zikiandaliwa.

Lakini baada ya mwili wa mwanaume huyo ambaye jina lake halikutajwa kuwekwa kwenye chumba chenye baridi cha monchwari kwa zaidi ya masaa 20, mwanaume huyo alizinduka na kujikuta yuko monchwari kwenye baridi kali sana.

Mwanaume huyo alipiga kelele akitaka atolewe toka kwenye chumba hicho lakini badala yake wafanyakazi wa monchwari walidhani wameona mzimu na kutimua mbio.

"Familia yake walidhani ameiaga dunia", alisema msemaji wa wizara ya afya, Sizwe Kupelo.

"Familia yake ikiamini kuwa ndugu yao amefariki iliwaita waandaaji wa mazishi ambao waliuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka monchwari lakini kwenye majira ya saa 11 jioni jana jumapili, mwanaume huyo alizinduka na kupiga kelele atolewe toka kwenye chumba cha baridi", alisema msemaji huyo wa wizara ya afya.

Tukio hilo lililotokea kwenye mji mdogo wa Libode lilisababisha wafanyakazi wawili wa monchwari waliokuwa zamu waamue kutimua mbio wakidhani wameona mzimu.

Baada ya kupiga kelele za kuomba msaada na baadae kurudi monchwari na kumkuta mwanaume huyo yuko hai, waliita ambulansi ambayo ilikuja kumchukua mwanaume huyo na kumuwahisha hospitali.

Msemaji huyo wa wizara ya Afya aliwataka wananchi kutojichukulia majukumu ya kuwaita watu wa monchwari wanapodhani ndugu zao wamefariki.

"Ni madaktari, watoa huduma za afya au mapolisi ndio wenye haki za kuwachunguza wagonjwa na kutoa taarifa kama wamefariki au la", alisema msemaji huyo wa wizara ya afya.

Taarifa iliyotolewa leo na wizara ya afya ilisema kwamba mwanaume huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa asthma na ndugu zake walidhani amefariki alipokutwa amezimia nyumbani kwake.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa mwanaume huyo alilazwa kwenye toroli ndani ya chumba chenye baridi kali cha monchwari kwa masaa 21 kuanzia siku ya jumamosi jioni mpaka alipozinduka siku ya jumapili.
 
south Africa hamna utaratibu wa kuthibisha kwanza what is thought to be dead body kabla ya kuingizwa mortually? Hii mm naiona kama dalili ya ubabaishaji katika utendaji kazi.
 
Back
Top Bottom