Maiti yasafirishwa kwa pikipiki Bukoba

Lakini sidhani kama hili ni la kulaumu serikali. Sijawahi kuona mahali ambapo serikali inasaidia kusafirisha miili ya marehemu katika mazingira ya vifo vya kawaida (I stand to be corrected), familia, jamaa na ndugu ndio wanawajibu huo.

hujasoma vizuri maelezo ya jamaa au umakini wako unapungua mkuu!!!!!! Kasema ugumu wa maisha. Hilo nalo linaubishi? Nani amekodi pikipiki kama si ndugu? Mimi kwetu, Muleba, hospitali teule ya wilaya, inayomilikiwa na mission, ya Rubya, miaka 15 iliyopita maiti na wagonjwa waliozidiwa walikuwa wanasafirishwa bure!!!!! Hapo utasema nini? Gari hizo zilijulikana kama 'Tomushange' (hutamkuta)!!! Leo kulingana na ugumu wa maisha maiti inafungwa kwenye ubao na kufungwa kwenye baiskeli!!! Wakati mwingine kamba zinakatika inanadondoka chini!!! Tunaenda mbele au nyuma!!!!

Leo hii ni hatari, serikali imeweka miundombinu pale walipo na maslahi au kuna mianya ya wizi na ufisadi. Inauma sana.
 
Mbona maiti mwenyewe anaonekana kama anaongea na simu, hii picha ina mashaka kidogo. Lakini hata hivyo serikali ina majukumu mengi zaidi ya kusafirisha maiti, hata Yesu aliwaambia '' waacheni wafu wawazike wafu wenzao''.......MATHAYO 6:12

haaaah haaah haaah dah ww kweli umepinda lol, mana nilikua na huzuni kuona hii picha bt nilipofia ur comment nimecheka mpaka machoz yamenitoka.
Jifunze ustaarabu maiti hadhihakiwi.
 
........................................

"Kweli nimesikitika sana kuona hali ya kwetu Bukoba bado tuko nyuma mpaka maiti inabebwa kwa pikipiki yaani thamani ya utu inaishia hapo kweli nimesikitika sana. Sasa tufanyeje kwa walio mbali na Bukoba na walioko Bukoba wenyewe tunatakiwa kujikomboa kununua vifaa viwasaidie ndugu zetu walioko vijijini nakumbuka zamani kama unatoka Kyaka pale mlima katoma lazima ukutana na watu wamebeba maiti kwenye baiskeli wanapelekwa vijini kila mtu anaona sioni wakati wa sasa jamani.

Pikipiki ikiwa mwendo wa kasi inatoka Ndolage Hospitali kuelekea Ichwandimi kupitia Nyakigando maeneo ya Rubale.

EMT bora hata huko bukoba Huna haja ya kusikitika. Kama mtu akiwa mzima anapanda piki piki hiyo hiyo sembuse maiti. Tena bora piki piki ni mendeleo zamani unaweza kukuta ilkuwa ni baislei au vijana wa kijiji mgonjwa akifariki ndio kwa mguu wanafuta hiyo maiti. Sasa imagine may be kilometer zaidi hata ya tano

Mimi sioni shida kutumia pikipiki katika mazingira hayo.maaa inoa sana muda na nguvu za vijana. Utaona tatizo kama hilo linatokea kinondoni au hata bukoba mjini. Lakini kama umewai kukaaa kijiji hata watu wenye baiskeli wanahesabika na wnajulikana Magari ndio hakuna kabisa. Gari likiingia kijijini kwa wanakijijini breaing news
 
Ndio maana waislam tunaamini kua wakipatikana waislam kadhaa wakukuzika basi wakuzike tu ulipo fia.
Hii inasikitisha sana kwa kweli. Naamini kabisa kua hata marhem angejua kua itakua hivi angekataa kusafirishwa.
 
Mkuu sio mimi niliyesikitika. Kama umeangalia vizuri hiyo sehemu nimenukuu.
 
Da, nimengalia hiyo picha imeniuma sana, ebu imagine kama ni mama yako anasafirishwa hivyo amekosa nini kwenye dunia hii. Yote yana mwisho
 
inasikitisha na inavyoonyesha ni mama mjamzito aliyefariki pengine kwa kukosa huduma za haraka
 
Sijaelewa mantiki ya kusema kuwa"inasikitisha" na kwamba marehemu angekataa kusafirishwa wakati akiwa hai ni mwendo mdundo?!, mimi sijaona tatito hapa hasa unapozungumzia mazingira ya vijijini.
Ndio maana waislam tunaamini kua wakipatikana waislam kadhaa wakukuzika basi wakuzike tu ulipo fia.
Hii inasikitisha sana kwa kweli. Naamini kabisa kua hata marhem angejua kua itakua hivi angekataa kusafirishwa.
 
Sijaelewa mantiki ya kusema kuwa"inasikitisha" na kwamba marehemu angekataa kusafirishwa wakati akiwa hai ni mwendo mdundo?!, mimi sijaona tatito hapa hasa unapozungumzia mazingira ya vijijini.

Hii imetokea mijini sio kijijini. Kusafirisha maiti kwa pikipiki au baiskeli kijijini ni la kawaida. Hata kama hili lilikuwa limetokea kijijini basi tuendelee kusafirisha maiti kwa staili hiyo kwa sababu huoni tatizo? Kwa hali inavyoonekana hii itasambaa pia mijini. Tutaanza kuwaona bodaboda bize barabara ya muhimbili wakisafirisha maiti. Ikifikia wakato huo utasema pia hakuna tatizo?
 
Hapo kwenye red:Ndolage ni Muleba vijiji na Nyakigando-Rubale ni Bukoba vijiji na ni mbali sana na Bk mjini.Kwa hiyo ni vijijini huko kote
 
Mnaoshangaa Nawashangaa sana , mbona pikipiki ya nchina ni maendeleo sana kwa kusafirisha maiti, miaka 10 iliyopita walitumia toroli au baiskeli, mie niliwahi kubeba maiti ya mtoto wa miaka kumi na mamake kwenda KM 15, na hakukuwa na tatizo. Tushukuru wachina kutuletea maendeleo kwa sh. million 1.5
 
hapo ni lutenge-akitokea kamachumu kuelekea nyakahama to rubale hadi ichwandimi kwenye maziko.
Kutoka ichwandimi hadi nyakabanga kwao na kwake naziri karamagi-aliyekua mbunge ni km 1..tu! Inasikitisha kuona huyu mchumia tumbo anashindwa kuwapa hata kipikapu chake,huyu karamagi ni mtu wa ajabu sana.!
Alafu 2015 utasikia ameomba tena kura na kutawanya pesa... Hana maana kabisa! Watu wa namna hii ndio kikwazo kwa maendeleo ya bukoba.
 
1417977607330.jpg
 
Back
Top Bottom