Maiti yasafirishwa kwa pikipiki Bukoba

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Juni mwaka jana, niliweka hapa jamvini habari na picha za kusikitisha kuhusu hali halisi ilivyo kwa baadhi ya sehemu za Tanzania ambapo kutokana na ukali wa maisha na kupanda kwa bei ya mufuta na vyombo vya usafiri, maiti hupakizwa juu ya pikipiki tayari kusafirishwa kwa ajili ya maziko. Hiyo ilikuwa katika kijiji kimoja mkoani Mbeya (https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/150148-maiti-yasafirishwa-na-pikipiki.html). Safari hii imetokea huko Bukoba ambapo maiti imebebwa kwa pikipiki tayari kusafirishwa kwa ajili ya maziko. Yafuatayo ni picha na maelezo kama yanavyopatikana kwenye blogu ya Bukoka (Bukoba).

Mwanzo kwa kunukuhu:

“Kweli nimesikitika sana kuona hali ya kwetu Bukoba bado tuko nyuma mpaka maiti inabebwa kwa pikipiki yaani thamani ya utu inaishia hapo kweli nimesikitika sana. Sasa tufanyeje kwa walio mbali na Bukoba na walioko Bukoba wenyewe tunatakiwa kujikomboa kununua vifaa viwasaidie ndugu zetu walioko vijijini nakumbuka zamani kama unatoka Kyaka pale mlima katoma lazima ukutana na watu wamebeba maiti kwenye baiskeli wanapelekwa vijini kila mtu anaona sioni wakati wa sasa jamani.

Nakumbuka kuna kampuni moja iko Dar es Salaam wanazo Bajaji nzuri zinaweza kubeba maiti, wagonjwa, wamama wajawazito tukiamua tunaweza kufanya harambee kwa ajili ya watu wa Bukoba tukanunua hizo bajiji kama tano tukapeleka kwenye kata ili mwanakijiji anapopatwa na shida kama hii anakodi kijijini na inasaidia hata kwa maendeleo. Kuna kijiji kimoja mtwara wanakijiji baada ya kupata shida walichanga wanakijiji wakainunua kwa 10,000,000/= inawasaidia sana na kijiji ndo kilichagua mtu atakayeindesha na kuitengeneza yaani wako sembuse sisi watu kutoka BK tunashindwa nini?” Mwisho wa kunukuhu.

SAM_4214.JPG





SAM_4207.JPG



Pikipiki ikiwa mwendo wa kasi inatoka Ndolage Hospitali kuelekea Ichwandimi kupitia Nyakigando maeneo ya Rubale.

SAM_4195.JPG


Picha na maelezo zaidi: Bukoba: ASEMAVYO MDAU ELEWA SABUNI KUHUSU USAFIRI WA MAITI;Hii ni kutokana na habari tuliotoa kupitia wadau wiki iliopita.
 
Duh!
Nchi ya ajabu sana hii imejaa viongozi wapenda sifa wasiojali kabisa masuala muhimu ya kijamii. Maiti inakalishwa kwenye kiti kwa urahisi wa usafirishaji? Hili linawezekana Tanzania tu, nchi inayoongozwa na sharo presidar jk kutoka ccm! Maisha bora hayawezekani, tuache kudanganyana!
 
maskini wa Mungu! wapiga kura nao hawa,na wanapanga mstari kabisaa!afadhali sie wa mbagala tungebeba na guta,sasa hawa hata barabara hawana!
 
Sijaona kitu kibaya kama hiki mwaka huu, kwani hao wanakijiji hawawezi kuchangia, duh.
 
Lakini sidhani kama hili ni la kulaumu serikali. Sijawahi kuona mahali ambapo serikali inasaidia kusafirisha miili ya marehemu katika mazingira ya vifo vya kawaida, familia, jamaa na ndugu ndio wanawajibu huo.
Inawezekana kuna tatizo la barabara pia ambalo linasababisha kupanda kwa gharama za usafirishaji, hivyo hata kama wanafamilia na jamaa wengine wangechangishana kupata usafiri wa gari lisingeweza kufika huko wanakopeleka hiyo maiti.
 
Lakini sidhani kama hili ni la kulaumu serikali. Sijawahi kuona mahali ambapo serikali inasaidia kusafirisha miili ya marehemu katika mazingira ya vifo vya kawaida, familia, jamaa na ndugu ndio wanawajibu huo.

Venezuela unapewa usafiri na sanduku bure!
 
Lakini sidhani kama hili ni la kulaumu serikali. Sijawahi kuona mahali ambapo serikali inasaidia kusafirisha miili ya marehemu katika mazingira ya vifo vya kawaida, familia, jamaa na ndugu ndio wanawajibu huo.
Mzee Mwanakijiji, tunapoilaumu serikali katika hili hatumaananishi wao ndio walitakiwa watoe gari kwaajili ya kubebea maiti... Ndiyo ni wajibu wa ndugu jamaa na marafiki kuchangia na kuusafirisha mwili wa marehemu. Ila ukumbuke sio watu wote wako katika financial position kama yako mkuu... Mi siamini kama ndugu wa huyo marehemu wamependa hali hiyo... Ugumu wa maisha ndo uliosababisha wakose hata hela za kukodi gari kwaajili ya kumsafirishia marehemu wao, na ndio maana tunailaumu serikali inayosema maisha bora kwa kila mtanzania... 'Think twice'
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Dahhhh kwa kweliInatia huruma sana..Na hiyo habari ya kusafirisha Wamama wajawazito na mabajaji.. Kwa kweli ni kitendo cha laana.. Yaani serikali yatu imeshindwa kuweka ambulance Kwa kila wilaya... kwa vitu ambavyo ni very Emergency ... Nadhani ni bora kuwa hata na moja kuliko 0...
 
Lakini sidhani kama hili ni la kulaumu serikali. Sijawahi kuona mahali ambapo serikali inasaidia kusafirisha miili ya marehemu katika mazingira ya vifo vya kawaida (I stand to be corrected), familia, jamaa na ndugu ndio wanawajibu huo.
Mkuu nadhani kinacho zungumziwa hapa ni ugumu wa maisha unaopelekea hali ngumu kwa kila kitu. Jamaa amezungumzia kuh kupanda kwa mafuta nk hakusema serikali ibebe jukumu.
 
Mbona maiti mwenyewe anaonekana kama anaongea na simu, hii picha ina mashaka kidogo. Lakini hata hivyo serikali ina majukumu mengi zaidi ya kusafirisha maiti, hata Yesu aliwaambia '' waacheni wafu wawazike wafu wenzao''.......MATHAYO 6:12
 
Let us be realistc wazee, sidhani kama serikali inapaswa kutoa/kuwawezesha wanachi kuzika ndugu zao. hili ni jikumu la society 100%. basi wameshindwa hata kubebe mwili wa marehemu ktk mkokoteni ukiwa umelazwa na kusitiriwa vizuri!!!!! then mkokoteni ukavutwa na pikipiki???? hata wewe ulieleta picha hii HUNA MAANA. sasa unachochea nini hapa????
 
MODS please iondoee hii post, ni udhalilishaji wa maiti huyu (kama kweli ni maiti) na sioni zaidi ya kujenga chuki dhidi ya serikali wakati jamii husika walipaswa kutimiza wajibu wao. Mods is it hard to see!!!!!! ( Hizo unazoziita hekima unazotumia ku BAN watu kwani huwezi kutumia hizohizo kujua hili ni baya na lisingepaswa kuwepo)!!!!
 
Lakini sidhani kama hili ni la kulaumu serikali. Sijawahi kuona mahali ambapo serikali inasaidia kusafirisha miili ya marehemu katika mazingira ya vifo vya kawaida (I stand to be corrected), familia, jamaa na ndugu ndio wanawajibu huo.

MMMJ Ondoa upupu wako...mbona kule Tarime serikali imeleta ugomvi kuhusu miili ya marehemu?? kifo ni kifo, hamna kifo cha kawaida!!
 
Lakini sidhani kama hili ni la kulaumu serikali. Sijawahi kuona mahali ambapo serikali inasaidia kusafirisha miili ya marehemu katika mazingira ya vifo vya kawaida (I stand to be corrected), familia, jamaa na ndugu ndio wanawajibu huo.

Suala sio serikali kusaidia kusafirisha, ni watu kukosa uwezo wa kujisaidia wenyewe. Kwanini? Barabara ni mbovu, mafuta bei juu, ukichanganya ubovu wa barabara na bei ya mafuta, sehemu ambayo ungetumia laki 1 utatakiwa kulipa laki 2 hadi 3. Sasa Serikali kwa nini isilaumiwe kwa uzembe
 
Sizinga wewe na upupu hamtofautiani, sasa serikali itazika maiti ngapi???? basi serikali isiishie hapo ianze kuoa condoms bure, iwalipie watu kodi za nyumba, hela ya kula daily!!!! acha akili za ujima waambie hao wenzio mfanye kazi bure aghali
 
4946384_orig.jpg



Ni jambo la kusikitisha lakini ndivyo hali halisi ilivyo katika baadhi ya maeneo ya Tanzania kutokana na ughali wa vyombo vya usafiri, hali inayochangiwa kwa kiasi kikubwa na bei ya juu ya petroli/dizeli. Picha zinazoonekana hapo zimepigwa na mdau mmoja wa afya, aliyeshuhudia maiti ikipakizwa juu ya pikipiki tayari kusafirishwa kwa ajili ya maziko katika kijiji kimoja huko mkoani Mbeya. Ndugu hawa wangependa kuupa stara ya mwisho mwili wa marehemu lakini kutokana na ukali wa maisha, imebidi kubuni njia mbadala itakayofanikisha shughuli hiyo.

Eti, zilizinduliwa Bajaj Ambulance kwa ajili ya kuwabebea wagonjwa kuwawahisha hospitalini, hasa zikiwalenga kwa wanawake wajawazito, vile vile Waziri Mkuu akazindua "Bajaj za kuzimia moto", seuze pikipiki kusafirisha maiti aliyeketi kitini, kiti kilichopachikwa juu ya pikipiki?

source: Wavuti - Habari

Kama ni kweli kwanza wafiwa poleni sana kwa msiba.

Pili narudi kwa mtoa mada, naomba nijue haya
1. hapo walikuwa hospitalini au nyumbani kwa marehem?
2.Huyo dereva ni askari au ni mwana chadema? nauliza hivi kwa sababu naona amevaa gwanda ambazo ni uniform za mgambo na chadema
3.katika mazingira ya kawaida hakuna msiba unaokosa presence ya wanawake hapo kwenye picha mbona kama ni isue ya watu wawili tu na watatu yuko anawashangaa kuonesha hayuko nao?
4. kama uwezo ulikuwa hauruhusu nini mantiki ya kusafirisha maiti? inamaana hapo alipofia ilikosekana sehemu ya kumzika?
 
Back
Top Bottom