Maisha yetu yapo mikononi mwa nani?

Pax

JF-Expert Member
May 3, 2009
268
87
Serikali imeamua kwa makusudi kukandamiza haki za wananchi walioiweka madarakani, imeamua kuwapora haki zao, maisha yetu yapo mikononi mwa nani? Mwizi wa kuku yupo Segerea anatumikia kifungo cha miaka 5, aliyeiba mabilioni yupo mtaani anafurahi.

Wenye madaraka wanashirikiana na mahakama kukandamiza demokrasia na haki, wanaamua kila kitu kwa matakwa ya serikali. Sheria walizotunga kumbe sio kwa ajili yao, ila kwa wananchi wasio na chochote. Nauliza tena maisha yetu yapo mikononi mwa nani? Haki itapatikana wapi? mahakamani-hapana? tume ya uchaguzi?-hapana, polisi-hapana?

Serikali inatumia kila mbinu kulazimisha kukaa madarakani, inatumia rasilimali za wananchi ili iwatawale kwa mabavu zaidi. We will pay high price for this, dalili zipo wazi.


Some ignorance's are genetically determined, cant be changed by learning.
 
Mikononi mwa MUNGU wa MBINGUNI kupitia YESU KRISTO BWANA WETU
mix with yours
 
Back
Top Bottom