Maisha Yangu na VVU mwilini

Jamaa smart sana,kheri yako uliyepima na kujua status yako na kuikubali,maana kuwa na HIV sio mwisho wa maisha.
Nakushauri usiharakishe kutafuta mwenza,ongeza nguvu katika biashara zako,fikiria zaidi kuhusu kuwa na mafanikio makubwa.Ukishatulia kidogo then ndo umtafute mwenza.Ukifuata masharti ,utaishi hadi uzeeni,wengi wana HIV lakini hawajijui.
 
kauli yako haijawa na mwisho mwema.kwamba kuoa/kuolewa ndio kutatue tatizo lao??la hasha...usijidanganye royna kwamba hukokwenye ndoa ndio u will be more safe 100%..hapana.chance zote are posible...full solution ni lifetime abstainance...otheryz utakua unaninyanyapaa mimi na wewe mwenyewe.
....Funguo inahitajika watu kama wewe kufanikiwa na mapambano dhidi ya UKIMWI.hatuwezi kuushinda UKIMWI kwa kuwa wanafiki na wenye unyanyapaa. Maisha lazima yanedelee, na UKIMWI au bila UKIMWI. Watu mlio katika ndoa, mnapaswa kujiangalia sana, takwimu kila kona ya Afrika zinaonyesha sasa maambukizi yanaenea zaidi miongoni mwa wanandoa, au watu waliokatika mahusioano yenye " uaminifu" kwa muda mrefu. Sababau zake ziko wazi; hawa ndio wasiotumia Kondomu. Wale "vicheche" na watu wa "hit and run" wanajijua kuwa ni watu wanaochukua risk, hivyo wanatumia Kondomu. Ndigu, Ufunguo, kwa kuwa umeshajitambua, umepiga hatua muimu ya kuaza kukabiliana na UKIMWI. Nikutie moyo, kwa dawa na huduma zillizopo, huna tofauti na wengi wetu. Nawajua watu wanaoishi maisha ya furaha, na yenye afya kwa zaidi ya 15 yrs. Nakutakia kila la heri kumpata mwenzako!
 
naamini katika miujiza ya mungu na kuwa hakuna linalomshinda mungu,jipe moyo,ishi kwa furaha na kusali,the future holds a surprise for you
 
baada ya kupimwa na kupewa majibu nimegundulika nina VVU mwilini mwangu.............

mwanzoni ilinipa tabu kidogo ila nilijikaza kiume kuukubali ukweli..huwa ni mtu nisiyependa kuregret in life hasa inapotokea nimeshapoteza kitu.................bado ni kijana; mwanaume mwenye sifa zote.educated.nina biashara zangu zinazoniingizia kipato cha kawaida...........

ila nawaasa ndugu zangu kwamba muda wowote siku yeyote you can be a victim........hakuna anayejipa ugonjwa huu...

nilikua na mtu niliyemrespect na kumuamini kupita kiasi....tulijenga utaratibu wa kucheki afya zetu kila baada ya miezi sita na hii ilisaidia sana kujua afya yangu mapema....mwenzangu alianza kuweka sababu na visingizio nikawa napima peke yangu hadi nilipoujua ukweli...sikumwambia!! huyu mwenzangu tayari tumetengana baada ya kuwa tunapishana sana kauli na vitendo lakini si kwa sababu ya status niliyo nayo maana sikumwambia.......

naendelea na biashara zangu happily n healthier wala hakuna anaefahamu.....

nafeel guilty kuingia kwenye new relationship na binti ambaye ni negative....natumai wote wangekua kama mimi huu ugonjwa tungeutokomeza kabisa...lakini haipo ivyo...........

ombi langu mwisho kabisa ni kuweza kumpata binti anaenikubali na hali yangu hii preferably positive!!

usinipe pole......
Mkuu takugongea like nikiingia kwa lap,una moyo wa kishujaa , Mungu yu pamoja nawe mkuu! Salute..
 
Heko kwa kupima kamanda. Nina mwaka wa 3 bado napangua tu tarehe za kupima. Nikifikiria tu huko naishiwa nguvu.
 
....ishu kama hii inabid uweke ur real name....
Kinyume na hapo ni vumbi tu...
 
Dauhhh
Yule wa kwanza ungemjulisha tu maana
Kama anao ataenda kuusambaza huko ....

Anyway
kila lakheri kumpata mtakae pendana....
 
Hebu tuulizane jamani,hivi ni wana jf wangapi tumepima? Kupima mchezo? Watu kibao wanapima na hawaendi kuchukua majibu.Ufunguo nikupongeze kwa busara yako ya kupima mara kwa mara,i can tell you it has saved your life.
Ushauri wangu:Tafuta daktari mmoja TU awe confidant wako,usitumie madaktari wengi,kazi yake ata monitor progress yako na kukupa ushauri wa mara kwa mara.Don't touch ARV's mpaka dokta akwambie.Kula vizuri , tumia multivitamins.
Kuhusu kuoa hilo wala sio tatizo mbona zipo dating agencies na websites where you can get hooked up na mrembo atakayekubali hiv status yako?
 
all the best kwani huu ugonjwa sio mwisho wa maisha..
Ni vema umejitambua na kuamua kuoa wengine.
Kama wote tungekuwa hivi...hali isingekuwa mbaya
 
Hebu tuulizane jamani,hivi ni wana jf wangapi tumepima? Kupima mchezo? Watu kibao wanapima na hawaendi kuchukua majibu.Ufunguo nikupongeze kwa busara yako ya kupima mara kwa mara,i can tell you it has saved your life.
Ushauri wangu:Tafuta daktari mmoja TU awe confidant wako,usitumie madaktari wengi,kazi yake ata monitor progress yako na kukupa ushauri wa mara kwa mara.Don't touch ARV's mpaka dokta akwambie.Kula vizuri , tumia multivitamins.
Kuhusu kuoa hilo wala sio tatizo mbona zipo dating agencies na websites where you can get hooked up na mrembo atakayekubali hiv status yako?


Bishanga wewe umepima??maana wewe Baba Koku lol.
 
Mimi sikupi pole kaka yangu nakupa HONGERA kwa kupima na kuikubali hali yako. Wewe ni shujaa pengine kuliko wengi wetu humu. I salute you for that. Na kuonyesha ukomavu wako hukupenda kujificha, kwa kuwa unajua ungewaambukiza wengi. MUNGU akubariki kwa hilo na kukukirimia hitaji lako.
 
Kawaida tu ndugu yangu, wala si hatari kihivo!
Cha msingi zingatia masharti yote chini ya hali hiyo, kamwe usimwingize mtu kwa kutarajia, katika shida kama yako.
Ushindi wakwanza ulioufanya ni kukubaliana na hali hiyo...yanayofuata yote yanakuwa ni maisha ya kawaida!
 
Naweza kukuita jasiri, na unaonesha utaishi maisha marefu yenye amani inshallah. Ni wachache wanaojikubali walivyo, na wakachukua hatua za kuwalinda wengine.

Ushauri:
Si lazima umpate aliye positve pia, unaweza kumpata mke mwenye mapenzi ya kweli, UKAPATA USHAURI WA KITAALAMU mkaendelea kufurahia na mwenzi wako salama na mkapata mtoto/watoto wasio na maambukizi. Nasisitiza, hilo linawezekana baada ya kupata ushauri/maelekezo ya kitaalamu.
 
Back
Top Bottom