Vituka
JF-Expert Member
- Nov 9, 2011
- 2,257
- 1,246
sijaoa na nilishaapa,siwezi oa mwanamke ambaye amelelewa na single mother. Bora aliyelelewa na baba
Nyalotsi unaweza kutupa sababu ya wewe kutooa mwanamke alolelewa na single mother?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
sijaoa na nilishaapa,siwezi oa mwanamke ambaye amelelewa na single mother. Bora aliyelelewa na baba
Naandika post hii nikiwa sijui pa kuanza, il a kwa kifupi tu, nimeanza maisha mapya ya kuwa single mother.
mimi na baba mtoto havijawork out kwa kweli na imenibidi nifanye maamuzi magumu. ni mwanaume nimekuwa nae kwa muda wa miaka saba ila hatujaoana, tumefanya mambo mengi ya maendeleao pamoja,ila gafla tabia yake ikabadilika akawa ni mtu wa kunigombeza bila sababu, chochote nikifanyacho kwakwe ni kibaya,lugha anayotumia kwangu akiwa na hasira ni mbovu, ila at the same time anasema ananipenda,nimekuwa ni mtu wa kuumia moyo kwa muda wote huo,najiuliza ni kupenda gani kwa namna hiyo.
Hivi karibuni nimeamua isiwe tabu kila mtu aendelee na ustaarabu wake,yeye amekuwa akitumia mtoto kunisema nina roho mbaya, sina huruma na maneno kedekede,ila kusema ukweli nimevumilia vya kutosha na sasa nimeona basi inatosha, ninampenda ndio na ingetokea miujiza abadilike ningemrudia ila ndo hivyo.kwa hasira amegoma hata kumuhudumia mtoto anasema akifika miaka saba nimpe sasa hivi akimuona atasikia uchungu kisa mimi simtaki.
Kwa wenye uzoefu jamani naanzaje kuishi maisha ya usingle mother wakati kila siku lazima mtoto aulizie daddy au hata akilia atalia daddyyy dadyyy,nitakuja kumwambia nini akiwa mkubwa?na je nikija kuanza mahusiano mengine mtoto atanionaje?
Ili kudumu lazima uvumilie, kuachana si suluhu ya matatizo ni mwanzo wa kupata matatizo mengine. Lugha chafu za mumeo zinajadilika kwakuwa ktk miaka saba umekuwa nae unaweza kumbadilisha kwa kumpa upendo na kuonyesha wewe ni mama bora kuliko wanaompa kiburi na dharau huko nje.
Dhambi ya utengano ni mbaya itaendelea kukufuata popote uendapo hutoweza kutulia na mwingine kwa kuwa sababu za utengano haziishi.kuwa mvumilivu na simama imara usiyumbe.mshirikishe mungu nae atalinda usijiamini kupita kiasi tambua na mpe mungu akupe busara na hekima nawe utashinda.
Ndoa haivunjiki? hata itangazwe ndoa mwanamke kama huyu will end up in the same situation!!! ni design ya wale wanawake wa beijing ''tunaweza" "naweza type"
rate ya single mothers inakua kwa sababu wadada wamekuwa liberated wanasahau nini maana ya mwanaume
Wapendwa, asanteni kwa michango yenu.
Kusema ukweli mpaka nimefikia maamuzi haya nimevumilia sana.Ndani ya miaka hiyo saba kwa miaka mitatu mimi nimekuwa ni mwanamke wa kunung'unika tu mara nikutane na texts za ajabu akiandikiana na wanawake,pale napomuhitaji siku zote amechoka au amelewa,kugombezwa,kupigwa pasipo sababu za msingi halafu the next day ataomba msamaha eti alisikiliza maneno ya kijiweni kuwa mwanamke akipigwa ndo anakuwa na heshima.
Na pia katika muda wote huo hatujawahi kuishi pamoja,kila mtu anaishi kivyake ila tu numba tulisaidiana kujenga na anaishi yeye kwa sasa.najiona mwenye mkosi kwa maana haonyeshi mapenzi kwangu na amekuwa akisema kuwa yeye hapendi ila anatamani. kila akinipigia simu kw amfano sijaisikia akipiga tena ni ugomvi nilikuwa wapi na nani?najiuliza kwnaini aniwazie vibaya yawezekana ayawazayo niyo ayafanyayo. kwetu wanamjua na kwao wananijua,na kila siku akiulizwa maswala ya ndo anapeleka mbele akisema bado hajaaccomplish mambo mengi.
Kuna aliyesema kuwa mimi ni design ya wale wanawake wa 'beijing' la hasha, mimi ni mwanamke ninayependa nisipopendwa, kipindi cha nyuma tuliwahi kuachana kwa muda wa mwezi mmoja kwasababu ya maneno yake ya kejeli na kuniambia kuwa hakunipenda alikuja kwangu to prove a point to his friends but akajikuta yupo tuu..ila mimi kwa kumuwaza mtoto nikaona nimrudie,lakini naumia,sijui nielezeje mjue kuwa nina machungu kiasi gani yanayosababishwa na mapenzi haya. kila nikisema simtaki ananiambia wimbo wa taifa na sina ujanja wa kumuacha eti nisipompenda yeye nitampenda mwanaume gani. ni mambo mengi sana yanayonipelekea nifanye maamuzi haya,naandika post hii machozi yananitoka maana hata asubuhi hii binti yangu kataka kuongea na daddy kwenye simu.sijui ni jinsi gani nitacope na situation hii kwa kweli.
Asante BD,
Kuhusu kumuhudumia mtoto nitaweza bila kumpeleka ustawi wa jamii,ingawaje itabidi tu nimuhamishe shule mana aliyopo kwa sasa ni expensive kidogo sitoweza kuafford peke yangu. Nitajitahidi kumlea malezi yaliyo bora ila ninapata mawazo mengi sana baadae nitamjibu nini akiniuliza what happened between me and teh daddy, she is only 3 yrs now ila anampenda sana baba yake,tangu nifanye maamuzi haya sasa ni wiki mbili na nimekuwa nikimdanganyadanganya tu sitaki amchukie baba yake. na amekuwa akinitext kuwa ameanza relationship nyingine na blabla kibao mi sijamjibu.
Naomba Mungu anisaidie kwenye hili.Mapenzi yanauma jamani asikwambie mtu,mmh.
Nyalotsi unaweza kutupa sababu ya wewe kutooa mwanamke alolelewa na single mother?
Nyalotsi unaweza kutupa sababu ya wewe kutooa mwanamke alolelewa na single mother?
wengi wao wamezoea kusikia mama zao wakilalamika,aah,mwanaume kitu gani? Mbona mi nimewalea mwenyewe? Na maneno mengine ya aina hiyo ambayo yana negative atitudes towards wanaume. Hivyo akiingia kwenye taasisi ya ndoa ukimkosea kidogo tu, anajua, ohooo..ndo wale wale! Hata kwa kosa ambalo ni la kurekebishana. Wengi wao ukikaa karibu nao utasikia kauli zao za kuonesha dharau kwa wanaume wakirefer kwamba mbona mama zao waliwalea peke yao hivyo mwanaume siyo chochote. Kuna wadada kama wawili nimesoma nao ambao nilikuwa karibu nao sana nilikuja gundua baadaye kwamba mama zao waliachana na baba zao na kuwalea wao as a single parent. Wana dharau mpaka hata we unayeongea nao muda mwingine unawakwepa.