Shantel
JF-Expert Member
- Feb 7, 2011
- 2,018
- 1,129
halafu tulizo.................Mkuu nakubaliana na wewe….
Lakini ukiacha wale ambao wanaona majukumu ya kusaidia ni moja ya kulipa fadhila.. Pia kuna wale ambao majukumu hayo ni moja ya sehemu ya maisha yao mfano wale ambao tumetokea kwenye familia zilizopitia misukosuko ya ndoa.. Mkuu, mimi binafsi nikiwa kiumbe wa kwanza, nilisha-crash na kutaka ku-surrender kwa Mola baada ya majukumu kufika shingoni, ila namshukuru sana rafiki yangu wa Kike ambaye alibaini njama zangu na kunipiga stop..Anyway, huyu bint siwezi kumsahau na ndio maana nilikataa kumwoa na kuwa mke kwani niliogopa majaribu ya kuvunja Moyo wake hapo baadaye. Naamini huyu bint alishachukua nafasi ya Mama kunirudisha duniani kwa mara ya pili… Anyway…
Kama nilivyosema hapo juu.. Ukiacha fadhila ambayo unaweza kuipumzisha kwa muda kama Wazazi wana uwezo. Kuna historia ya maisha ya nyuma ambayo inafanya majukumu kuwa automatically part n' parcel ya maisha.. Si unakumbuka hata Baba wa Taifa alisema Tanzania haitakuwa huru hadi Afrika yote iwe huru.. Lakini hapa yataka uangalifu kwani unaweza kumaliza rasilimali kuwasadia wengine wawe huru nawe binafsi kurudi kwenye umasikini kama ilivyotokea kwa Tanzania.. Ndiyo maana nilisema wema usizidi uwezo…
Fadhila hizo Mkuu..lakini angalia pia na utamaduni wetu.. Kwani huko nyumbani Jamii haina sehemu za kutunza wastaafu (Wazee) kama ilivyo kule ulaya ambako Wastaafu wao wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatunzwa kwenye viota maalumu ambavyo vinatusaidia sisi wengine kupata vibarua.. Lakini mkuu Je? Utawezaje kupata usingizi wakati umepata ajira ya kubadilisha mboga na unajiandaa kuama chumba kimoja lakini yule mstaafu ambaye alikubali kutukanwa na baniani ili mimi nipate ugali na mlenda anaangaika kuomba ulanzi na Komoni kule Ileje nyanda za juu.. Nadhani utajitahidi kumfungulia ka- baa ka ulanzi na komoni ili kiasi fulani anywe na kingine apate hela ya kutambia wenzake wakati wanakunywa ulanzi..
Ni kweli yataka moyo..hasa ikiwa kati yenu mmoja ameishi maisha ya Magharibi na mwingine ameishi maisha ya Mashariki… Lakini Pia..kuna asilimia chache ya wapenzi ambao wanahisi machungu ya wapenzi wao..
Tutamsaidia kumwambia wengi tumeishi hayo maisha.. Tulishataka kutafuta Shortcut..Lakini tukarudi njiani na kuendelea kupigika na kumwomba Mola aepushe kikombe chake na Majaribu… Mola ametusikiliza lakini sometime Yes..usione tuna smile usoni..Lakini bado tunaugulia moyoni.. Misekule ya dhiki inaendelea kutuandama wakati tunafikiri wenzetu wengi wanaendelea kuteseka na majukumu ambayo hawawezi kuyatua!