Maisha Vs Muda,...Unatosha?!

I am a failure when it comes to balancing my time..... All blames to TBL/SBL. Why on earth are they brewing this kind of drinking liquid? ...When I get out of my office the only thing in my addicted mind is Beer......... and only Beer!

hahahah umenichekesha kwa nguvu sana. unaishije? inawezekana unawaza beer ukiilekea kuinywea nyumbani au bar? Try now.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
asante mdau uliyeanzisha mada hii. kwa kweli jamani kuwa na muda na familia zetu na hasa wenza wetu ni muhimu sana. utakuta mtu yuko busy 24 hrs a day, 7days a week, 365 days a year. kinachofuata ni wenza wetu kuchakachuana na ma-house boy au ma-housegirl. sometimes hawapendi iwe hivyo ila circumstances zina-force iwe hivyo. nani hapendi kupata 'ile kitu roho inapenda'?
 
Dah Mbu umeniumbua vibaya weye mie sina mpangilio kabisa ngoja nisome na kukariri kha!! mpaka naona aibu kabisa.........................
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Dah Mbu umeniumbua vibaya weye mie sina mpangilio kabisa ngoja nisome na kukariri kha!! mpaka naona aibu kabisa.........................

lol,...waendesha maisha yako kwenye auto pilot mode ee?... tahadhari, kuna siku switches zina disengage zenyewe, wakati huo hata mayowe ya 'mayhem mayhem!' yatagoma kutoka kooni kwa tahayari zake!...
Mw'mungu akuepushie bana, usiudharau muda...kila dakika na sekunde ina maana yake duniani.

Maisha ni kipimo,...

Hata mapigo ya moyo wako (normal rate) ni baina ya 60-100/dakika...
Ukiachia yajipigie yatakavyo madhara yake ni makubwa kwa afya yako.
art-1.jpg

Muda muhimu...
 

MwanajamiiOne,...
Tatizo la wengi wetu tufanyao hizi kazi za kuajiriwa tuna nidhamu ya uwoga!...
Kwanza ni haki ya muajiriwa kudai Job description!...msinambie eti Bongo hakuna hiyo....
Haya, hata kama wafanya kazi kwa mhindi... masaa ya kazi ni yale yale,...either 8- 4/5pm!
Hakuna Muhindi ambaye anataka kufanya kazi/biashara zake zaidi ya masaa nane...chunguza!

Kwa wakazi wa Dar, jioni mtawaona hawa wenzetu waasia wamejazana kwenye gari na wake zao na watoto haooo Coco Beach kula upepo wa bahari na madafu. Tukirudi kwa wabantu wenzangu na mie,...waajiriwa tukishatoka maofisini/vibaruani, wengi wetu tunaishia 'vikaoni' na washkaji kupoozea mbili tatu kabla ya kurudi nytumbani. Tena usipoonekana kikaoni utaulizwa, unakimbilia nini nyumbani?!

Kuhusu hizo worrk overloads,...kiukweli kuna kila dalili nasi twachangia kujitwisha hayo ma home work!....Hivi kuna raha gani upo nyumbani na mkeo/mumeo, badala ya kutumia masaa machache baada ya mihangaiko ya kutwa kuwasaidia watoto homework, kula pamoja, na kubembelezana kwenye kochi kabla ya kwenda kulala...wewe mke/mume unakuwa busy na mafaili yako ya ofisini? Hasta huo muda wa kubadilishana mawazo unakuwepo kweli?

By the time mke/mume huyo anakwenda kulala, tayari mwenziwe anakuwa keshaboreka...keshajilalia zamani. Au kama mume ndio ana roho ndogo, atajionea bora akazurure nje...awe anarudi nyumbani kulala tu. There's alimit kwa kila kitu,...kuna kazi za dharura, hizo ni kawaida kufanyika nyumbani,...lakini si vizuri kujenga mazoea Monday to monday mke/mume yupo busy na mafaili ya ofisi,...au nakosea jamani?

Binafsi, I can tolerate baadhi ya kazi, lakini zile nionazo mke wangu anazidiwa kiasi kwamba huko kazini wanahataraisha maisha ya ndoa yangu, maisha ya mke wangu, na watoto wetu...sitasita kumjengea tabia ya kuanza kuacha mafaili huko huko ofisini. Tena akirudi nyumbani na simu zizimwe. Haiwi ati bosi yupo Kempinski na mkewe, anampigia mamsapu eti a submit report by 6am... unless mke wangu nae ni mzito wa kumaliza kazi zake huko ofisini.... that's another case.

Duh yaani hapa umenichoma, ukanichoma na kunichoma..........yaani ni kama vile ninavyoishi huwa unaka-video kadogo unanimonitor mimi Mh sasaa dah hata sijui nisemeje Mbu

Hii wheel of life haina jinsi ya kutufundisha kujaribu basi kubalance?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mh.................................nahau hii Mbu.
Sasa nlikuwa nawaza kwa kuwa mtu kuwa buzy kikazi kunaoanishwa na kuwa na pesa nyigni. Je inawezekana ukugundua kuwa unafanya kazi saha, unakosa muda wa kubalance maisha lakini unapata pesa nyingi. Je haiwezekani mtu kureset targets zake ili apunguze muda wa kazi? Say anafanya kazi 28 hrs na anapata wastan wa dola 6,000 kwa mwezi but all the time yuko stressed up, familia inaishi maisha ya upweke ingawa they have everything but ndo hivyo vya story ya WoS ! but akijichunguza anagundua kuwa ili aishi maisha ambayo atapata muda wa kuishi na kupata quality time na familia yake, kurudisha uhusiano mzuri na MUNGU wake n.k then inambidi afanye kazi masaa hayo 8 kwa wastani wa Dola 2000 with opportunity cost $ 4000! je kuna ataewezasacrifice??
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
....khaaa? Mwj1 hapo juu umeandika kilugha gani bana, hebu fanya editing kidogo..
 
Duh yaani hapa umenichoma, ukanichoma na kunichoma..........yaani ni kama vile ninavyoishi huwa unaka-video kadogo unanimonitor mimi Mh sasaa dah hata sijui nisemeje Mbu

Hii wheel of life haina jinsi ya kutufundisha kujaribu basi kubalance?

eeehhh? kama hivyo ndivyo unavyoishi basi wahitaji reality check kwenye prioroties za maisha yako.
Kumbuka, kila siku ina masaa 24,...waweza yagawa hayo masaa 24/3?....hebu nipe mfano unavyogawa muda wako katika siku, tubadilishane mawazo....
 
ni kweli,ila dharura zinazotokea ktk aya maisha,ratiba iyo haipangiki
natamani sana ila siwezi mana nilishaona huo upungufu
Mungu anisaidie kwakweli!
 

eeehhh? kama hivyo ndivyo unavyoishi basi wahitaji reality check kwenye prioroties za maisha yako.
Kumbuka, kila siku ina masaa 24,...waweza yagawa hayo masaa 24/3?....hebu nipe mfano unavyogawa muda wako katika siku, tubadilishane mawazo....

Mh Mbu nayagawaje? kwani hata siku nyingine kukumbuka kuwa siku ina masaa 12 ya mchana huwa sikumbuki itakuwa hayo ya kugawanywa? Nayagawa kwa kigezo gani?
 
Nashkuru nilikuwa naumudu muda sana kabla kuijua JF, isipokuwa kuna kipindi flani hii JF ndio ikaja kuwa sumu ya muda wangu, lakini kuna mtu flani (jina tunalo) alinichimbia mkwala wa mchezo wa kihindi, nashkuru sasa nimerudi kwenye form.

Hii mada ni muhimu kuliko bajeti ya dodoma.
 
Mh.................................nahau hii Mbu. Sasa nlikuwa nawaza kwa kuwa mtu kuwa buzy kikazi kunaoanishwa na kuwa na pesa nyigni. Je inawezekana ukugundua kuwa unafanya kazi saha, unakosa muda wa kubalance maisha lakini unapata pesa nyingi. Je haiwezekani mtu kureset targets zake ili apunguze muda wa kazi? Say anafanya kazi 28 hrs na anapata wastan wa dola 6,000 kwa mwezi but all the time yuko stressed up, familia inaishi maisha ya upweke ingawa they have everything but ndo hivyo vya story ya WoS ! but akijichunguza anagundua kuwa ili aishi maisha ambayo atapata muda wa kuishi na kupata quality time na familia yake, kurudisha uhusiano mzuri na MUNGU wake n.k then inambidi afanye kazi masaa hayo 8 kwa wastani wa Dola 2000 with opportunity cost $ 4000! je kuna ataewezasacrifice??

MWJ1...kuna jambo niliwahi ambiwa na mzee wangu,...kila ninachofanya lazima niangalie lina faida/hasara gani na mimi. Nitakukumbusha pyramid ya maslow na ngazi zake;
Mazlow_pink.jpg

Inakukumbusha nini?...kila ngazi uipandayo hakikisha umeacha msingi mzuri huko nyuma. Kumbuka, kishindo cha muanguka kwa aliye juu ni mkubwa kulikoni yule aliye hatua za awali.

Wengi wetu tukishafikia self actualization, ambayo wengi twaitafsiri ni kazi yenye mshahara mzuri, ndipo tunapokuja gundua kumbe hilo sio kila kitu maishani. Inabidi ku balance na mengineyo kuanzia chini kwenye physiological needs.
Ili ku balance yote hayo kwa siku moja inakubidi u balance masaa yako 24 kwa siku. Kama hilo haliwezekani, angalau kwenye siku saba za wiki...! Kinyume na hapo...waweza bakia isolated kama mbu, ..."prisoner of circumstances"...
 
Mh Mbu nayagawaje? kwani hata siku nyingine kukumbuka kuwa siku ina masaa 12 ya mchana huwa sikumbuki itakuwa hayo ya kugawanywa? Nayagawa kwa kigezo gani?

nitakupa mfano wangu,...

(Approx)

5.15am ; naamka kupiga rakaa tein zangu, wajua tena sie wa mwambao salaa salaa ndio inatuamsha
5.45am ; naanza shoto kulia zangu kutoka huku uswazi kuelekea mjini.... ni mazoezi mazuri huku nikibana bajeti ya daladala
6.30am ; nakuwa nishafika maeneo ya kujidai 'sokoni kariakoo' kupapatuana ma agunia ya kauzu toka kigoma
1.00pm ; nakuwa sina mchezo wa mbali na mama lishe, wanaandaa menu yenye chakula bora wale...
5.00pm ; nakuwa nishafunga mahesabu yangu, kidogo kidogo naelekea msimbazi kutafuta usafiri
6.00pm ; mara nyingi mida hii huwa tayari nishafika kwangu, kujimwagia maji...nk
6.40-8.30pm ;nautumia muda msikitini kumshukuru mwenyezi mungu
8.45pm ; nakuwa tayari nyumbani na bi mkubwa (soulmate) tukihadithiana yaliyojiri mchana kutwa,
wakati huo nae anakuwa keshapakua vilivyopikwa, mashaallah bibi yule!
11.00pm ; mashaallah tunajilalia zetu sie, na huu mgao wa umeme kila siku aaahhh... shida ya nini!

Umenipata hapo? ...usinkodolee bana...au wataka doubt my story sasa?
 
Mkuu Mbu katika huo mduara wa "wheel of life" wengine wameuvunja vunja na kutengeneza kamduara kao kadogo kadogo katika yale mambo ambayo wanayaona yanastahili kupewa kipaumbele katika maisha yao.

Kwa mfano wengine hawaoni umuhimu wa kwenda kanisani/msikitini kwa masaa chungu nzima kwa wiki pamoja na kuwa wanaamini kwamba Mungu yuko. Husali kwa dakika chache nyumbani kwao kila siku inapoanza na kwisha kumshukuru kwa yale aliyowajalia na kumuomba mengine wanayoyahitaji. Wengune pamoja na kuwa wanayapenda maisha ya ndoa huamua kuoana lakini hawataki watoto kutokana na gharama za malezi zilivyo kubwa na pia "kuharibu" life style ya wanandoa pale watoto wanapohusika kama vile badala ya kujirusha saa yoyote ile wanayotaka au kulala masaa yoyote ile au kwenda vacation za nguvu katika vivutio mbali mbali duniani kama kwenye mbuga za wanyama :) ufukweni mwa bahari iwe East Africa, Carribean au kwingineko. Wengine wameshajijenga vya kutosha kwa hiyo mambo ya carrer na finance kwao hayana matatizo.

Ninachotaka kusema ni kwamba huo mduara original wa 'wheel of life" familia nyingi zinauvunja vunja na kutengeneza mduara wao mdogo kutokana na mambo yale wanoyaona yanastahili kupewa kipaumbele kila siku, kila wiki, kila mwezi na pia kila mwaka. Kwa hiyo si ajabu kukuta kwamba mduara mdogo wa "wheel of life" wa familia A umetofautiana kidogo/sana na ule wa familia B kutokana na kuwa vipaumbele tofauti katika maisha yao ya kila siku. Kwa wale ambao wanajitahidi kuufuata mduara huo mkubwa wa wheel of life, kwa maoni yangu ni kazi kubwa mno! na kama wapo wanaofanikiwa basi ni wachache sana.


Hiyo avatar mpya Mhhhhh! :) ndio kaichagua nanihii!? hahahahahah lol! naogopa kuchema :)

 
Last edited by a moderator:
kwa tanzania hii,kuna kazi sana kuendana na kasi ya mda,kuna mambo mengi ambayo yanachangia kutukwamisha,labda tuanze kuyatatua haya yanayotukwamisha,ndo tuweze haya mengne
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Mkuu Mbu katika huo mduara wa "wheel of life" wengine wameuvunja vunja na kutengeneza kamduara kao kadogo kadogo katika yale mambo ambayo wanayaona yanastahili kupewa kipaumbele katika maisha yao.

Kwa mfano wengine hawaoni umuhimu wa kwenda kanisani/msikitini kwa masaa chungu nzima kwa wiki pamoja na kuwa wanaamini kwamba Mungu yuko. Husali kwa dakika chache nyumbani kwao kila siku inapoanza na kwisha kumshukuru kwa yale aliyowajalia na kumuomba mengine wanayoyahitaji. Wengune pamoja na kuwa wanayapenda maisha ya ndoa huamua kuoana lakini hawataki watoto kutokana na gharama za malezi zilivyo kubwa na pia "kuharibu" life style ya wanandoa pale watoto wanapohusika kama bile badala ya kujirusha saa yoyote ile wanayotaka au kulala masaa yoyote ile au kwenda vacation za nguvu katika vivutio mbali mbali duniani kama kwenye mbuga za wanyama :) ufukweni mwa bahari iwe East Africa, Carribean au kwingineko. Wengine wameshajijenga vya kutosha kwa hiyo mambo ya carrer na finance kwao hayana matatizo.

Ninachotaka kusema ni kwamba huo mduara original wa 'wheel of life" familia nyingi zinauvunja vunja na kutengenza mduara wao mdogo kutokana na mambo yale wanoyayaona yanasyahili kupewa kipaumbele kla siku, kila wiki, kila mwezi na pia kila mwaka. Kwa hiyo si ajabu kukuta kwamba mduara mdogo wa "wheel of life" wa familia A umetofautiana kidogo/sana na ule wa familia B kutokana na kuwa vipaumbele tofautu katika maisha yao ya kila siku. Kwa wale ambao wanajitahidi kuufuta mduara huo mkubwa wa wheel of life, kwa maoni yangu ni kazi kubwa mno! na kama wapo wanaofanikiwa basi ni wachache sana.

Hiyo avatar mpya Mhhhhh! :) ndio kaichagua nanihii!? hahahahahah lol! naogopa kuchema :)

looool! ha ha ha, ....nilimpa kapu la picha zangu, mwenyewe kaipenda hii,...eti inamkumbusha siku aliyokuwa ananifanyia Interview baada ya kumkabidhi CV (Resume) na Application ya Kuwekeza mapenzi yangu kwake.

Anyway,...hiyo wheel of life yaweza kuongezwa au kupunguzwa. Inapopunguzwa ndio kheri zaidi.
Tuseme tumeipunguza na kubakia na sehemu tatu.

1. Kazi na fedha
2. Mapenzi na familia.
3. Marafiki, na burudani.

Hapo bado mtu atakwambia hana muda,....!
The more you trim it, the more wajinyima muda! ...Chunguza!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom